Mama mkwe amekuja na mwongozo mkali

Mama mkwe amekuja na mwongozo mkali

Hivi Juzi Juzi Mama Mkwe Wangu Alikuja Kunitembelea Hapa Kwangu Akitokea Huko Mbwinde. Nilifurahi Sana Kwa Kuwa Ni Muda Sana Umepita Hatujaonana.

Mama Mkwe Hakupoteza Muda Akanipa " Mwongozo " Mzito Na Uliotukuka Kuwa " Nisimzalishe " Tena Mwanae Kwani Watoto Wawili Tuliozaa Mpaka Sasa Wanatosha Na Ni Marufuku Kumzalisha Tena Mwanae Ambaye Ni Mke Wangu Kipenzi Wa Ndoa Na Akafika Mbali Zaidi Baada Ya Kusema Ole Wangu Nikiuke Mwongozo Wake. Hakika Ilikuwa Ni Surprise Ya Nguvu Kwangu Na Ambayo Sijaitegemea Ingawa Hajanieleza Sababu Za Kunizuia Kutafuta Mtoto Wa Tatu. Mama Mkwe Anataka Kucontrol Ndoa Yangu Kwa " RIMOTI " akiwa Mbwinde.

Wakuu Naombeni Msaada Wenu, Maana Mpaka Mama Mkwe Anakuja Mke Wangu Hakunishirikisha Chochote ( Kama Kweli Alikuwa Na Tatizo ) Yeye Akaamua Kumtumia Mama Yake, Sasa Nimekosa Imani Na Mke Wangu Na Nafikiria Kumuacha Ili Aweze Kuongozana Na Mama Yake Pindi Atakaporudi Mbwinde Maana Anaweza Hata Akaniua Kwa Mwendo Huu. Nifanyeje Wakuu Maana Alichofanya Mama Mkwe Mpaka sasa Anaongoza 3-0 Dhidi Yangu Yaani kwa Lugha Nyingine Amenikamata Pabaya Mno Kunakotukuka!!
Rudisha mpira kwa kipa....ila kama umeshapigwa 3-0 tia mpira kwapani.
 
Kwan mkuu mahar uliyotoa umebakiza kias gan?
 
Inawezekana hata familia yako inaendeshwa na mama mkwe, una kazi ya ziada kukuza watoto hao
 
Kaa na mkeo muzungumze na akikubali kuengeza mtoto basi mlete wa tatu haraka iwezekanavyoh
 
Mtoto wake?alipokea mahali ya nini kama bado anataka kumuendesha?uncle mimi nime zaa mara tatu ila sijui niite bahati gani maana wamekuja sita ,tuliwaza watatu ila round ya pili tulijua atatumbukia mmoja wakaja wawili tena,naya tatu nilichezewa faulo kutokana na uzazi wetu wa mpango wakuhesabu siku wakaja tena wawili.lakini Mungu ameona na ametusaidia sana kwa suala la uchumi,tumejituma sana kufanya kazi mpaka sasa wameinuka kiasi chakusaidia hata kuweka maji bandani kwa kuku,rafiki mkeo hana akili tena sio team player!nyamaza uangalie move yao inapoishia wewe endelea na maisha yako ila pinguza stori be busy,wataisoma tu.
Mama yangu hakuwai kunikataza kuzaa zaidi yakuniambia nitumie condom maana nahesabu siku kuliko kumnyima kabisa baba wawili
 
Hivi Juzi Juzi Mama Mkwe Wangu Alikuja Kunitembelea Hapa Kwangu Akitokea Huko Mbwinde. Nilifurahi Sana Kwa Kuwa Ni Muda Sana Umepita Hatujaonana.

Mama Mkwe Hakupoteza Muda Akanipa " Mwongozo " Mzito Na Uliotukuka Kuwa " Nisimzalishe " Tena Mwanae Kwani Watoto Wawili Tuliozaa Mpaka Sasa Wanatosha Na Ni Marufuku Kumzalisha Tena Mwanae Ambaye Ni Mke Wangu Kipenzi Wa Ndoa Na Akafika Mbali Zaidi Baada Ya Kusema Ole Wangu Nikiuke Mwongozo Wake. Hakika Ilikuwa Ni Surprise Ya Nguvu Kwangu Na Ambayo Sijaitegemea Ingawa Hajanieleza Sababu Za Kunizuia Kutafuta Mtoto Wa Tatu. Mama Mkwe Anataka Kucontrol Ndoa Yangu Kwa " RIMOTI " akiwa Mbwinde.

Wakuu Naombeni Msaada Wenu, Maana Mpaka Mama Mkwe Anakuja Mke Wangu Hakunishirikisha Chochote ( Kama Kweli Alikuwa Na Tatizo ) Yeye Akaamua Kumtumia Mama Yake, Sasa Nimekosa Imani Na Mke Wangu Na Nafikiria Kumuacha Ili Aweze Kuongozana Na Mama Yake Pindi Atakaporudi Mbwinde Maana Anaweza Hata Akaniua Kwa Mwendo Huu. Nifanyeje Wakuu Maana Alichofanya Mama Mkwe Mpaka sasa Anaongoza 3-0 Dhidi Yangu Yaani kwa Lugha Nyingine Amenikamata Pabaya Mno Kunakotukuka!!
Samahani mkuu hii umeichukuliaje umeonewaa au umedhalilishwa?
Kwanza wewe kazi yako sio kuzaa kazi yako ni kugegeda kwa hiyo mama Mkwe mwambie tu akupe option Umtafute mbadala wa wife wako
 
Nakupa Masaa 24 Uniombe Msamaha Kabla Sijafungulia Silaha Zangu Za NYUKLIA kama SI Za Maangamizi Kwako, Huyo MTU Mimi Simjui Na Uache Kunifananisha Na VINYAGO wako!!
Yaani mnafanana hadi mikwara! khaaa kweli duniani wawili wawili[emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
ilikuwaje ukaruhusu hali ya yeye kukuongoza hadi kukosa amani, yaani 3 - 0 duh! kaa na mkeo mwambie mikwara yote aliyokupiga mama yake (mama mkwe) na mtume yeye wife aende akaongee na mama huko kijijini mbwinde kuwa hajapendezwa na namna anavyoingilia ndoa yake na mmewe na amwambie namna unavyokerwa na hiyo hali... lakini kama mkeo akikataa na kuonyesha ye yuko fine na hali hiyo basi mtishie kuvunja ndoa ili awe na uoga aweze kumkanya mama yake. kwanza jua je mke wangu na mama yake wamepanga huu mwongozo kwa pamoja? na kama jibu ni hawajapanga kwa pamoja, je mkeo anamtazamo gani juu ya huu mwongozo, yaani anaona its ok au anachukizwa? na kama anachukizwa anakubali mbinu zote ufaakazopanga ili urudishe control ya familia mkononi mwako? maana isije kuwa mkeo alienda kulalamika kwa mama yake ndo maana mama akaja na masharti hayo.... zaidi ya hayo hali ikiwa ngumu shirikisha wasimamizi wenu wa ndoa. ila usikurupe ukawaambia wazazi wako juu ya hili maana utawagombanisha wazazi wako na mkeo na itaathiri ndoa yako.
 
Angetoa kama ushauri na kueleza sababu za kuwashauri hivyo halafu akakuacha na mkeo mjifanyie uamuzi wa mwisho bila kuingiliwa na mtu, hapo mimi nisingekuwa na neno.
Lakini kitendo cha kutoa onyo kwako na vitisho hapo kwa kweli sio. Kama ni mimi ningemwambia bila kupepesa macho hivi: "Mama nashukuru sana kwa ushauri wako. Sasa tatizo langu mimi ni mdhaifu sitaweza kujizuia kuzaa mtoto mwingine.Kwa hiyo ili nisije nikakukwaza kwa kumpa mimba mwanao naomba uondoke naye uishi naye wewe ili awe salama"
 
Kwanini hukuuliza sababu ya kukukataza usimzalishe? Kama ni hivyo huenda wanakuona hujajipanga kuendesha familia.
 
Huyu POPOMA asiwapotezee muda na hizi chaii zake za kutunga, anapenda sifa kama bint/mwanamke anapotongozwa....
 
Hili neno -TUKUKA naona linatumika sivyo!!!!![emoji16]
 
Hahaha mimba ya tarehe 17 dec 2015 na mdogo mtu keshazaliwa? Mama mkwe inabidi awe mkali manake hadi dec hawakawii kuwa na watoto 8.

Sio kwa ada hizi elekezi za international skuli of tanganyika
View attachment 320814
Kumbe mshafunga ndoa hongera sana!!! Upo fasta na mtoto wa pili mshapata ndo maana ma mkwe kaingilia kati una speed sana
 
Hahaha mimba ya tarehe 17 dec 2015 na mdogo mtu keshazaliwa? Mama mkwe inabidi awe mkali manake hadi dec hawakawii kuwa na watoto 8.

Sio kwa ada hizi elekezi za international skuli of tanganyika
Kwa speed hiyo acha tu ma mkwe aingilie
 
Hivi juzi juzi mama mkwe wangu alikuja kunitembelea hapa kwangu akitokea huko Mbwinde. Nilifurahi sana kwa kuwa ni muda sana umepita hatujaonana.

Mama mkwe hakupoteza muda akanipa " mwongozo " mzito na uliotukuka kuwa " nisimzalishe " tena mwanae kwani watoto wawili tuliozaa mpaka sasa wanatosha na ni marufuku kumzalisha tena mwanae ambaye ni mke wangu kipenzi wa ndoa na akafika mbali zaidi baada ya kusema ole wangu nikiuke mwongozo wake.

Hakika ilikuwa ni surprise ya nguvu kwangu na ambayo sijaitegemea ingawa hajanieleza sababu za kunizuia kutafuta mtoto wa tatu. Mama mkwe anataka kucontrol ndoa yangu kwa " rimoti " akiwa mbwinde.

Wakuu naombeni msaada wenu, maana mpaka mama mkwe anakuja mke wangu hakunishirikisha chochote (kama kweli alikuwa na tatizo) yeye akaamua kumtumia mama yake, sasa nimekosa imani na mke wangu na nafikiria kumuacha ili aweze kuongozana na mama yake pindi atakaporudi mbwinde maana anaweza hata akaniua kwa mwendo huu.

Nifanyeje wakuu maana alichofanya mama mkwe mpaka sasa anaongoza 3-0 dhidi yangu yaani kwa lugha nyingine amenikamata pabaya mno kunakotukuka!

ongea na wife wako je yuko pamoja na mama yake kwa hilo? au amemtuma aseme hivyo? ongea naye tu vizuri mupange mambo yenu kama ataleta ujeuri, ujuba na yeye kuungana na mama yake basi angalia mustakbali wako wa maisha na zaidi kwa baadae ili ufanye maamuzi sahihi.
 
Back
Top Bottom