Mama mkwe amekuja na mwongozo mkali

Mama mkwe amekuja na mwongozo mkali

Huyo mama mkwe hana adabu kabisa.... Hivi amewezaje???
 
ong
Hivi juzi juzi mama mkwe wangu alikuja kunitembelea hapa kwangu akitokea huko Mbwinde. Nilifurahi sana kwa kuwa ni muda sana umepita hatujaonana.

Mama mkwe hakupoteza muda akanipa " mwongozo " mzito na uliotukuka kuwa " nisimzalishe " tena mwanae kwani watoto wawili tuliozaa mpaka sasa wanatosha na ni marufuku kumzalisha tena mwanae ambaye ni mke wangu kipenzi wa ndoa na akafika mbali zaidi baada ya kusema ole wangu nikiuke mwongozo wake.

Hakika ilikuwa ni surprise ya nguvu kwangu na ambayo sijaitegemea ingawa hajanieleza sababu za kunizuia kutafuta mtoto wa tatu. Mama mkwe anataka kucontrol ndoa yangu kwa " rimoti " akiwa mbwinde.

Wakuu naombeni msaada wenu, maana mpaka mama mkwe anakuja mke wangu hakunishirikisha chochote (kama kweli alikuwa na tatizo) yeye akaamua kumtumia mama yake, sasa nimekosa imani na mke wangu na nafikiria kumuacha ili aweze kuongozana na mama yake pindi atakaporudi mbwinde maana anaweza hata akaniua kwa mwendo huu.

Nifanyeje wakuu maana alichofanya mama mkwe mpaka sasa anaongoza 3-0 dhidi yangu yaani kwa lugha nyingine amenikamata pabaya mno kunakotukuka!
ongea na mke wako mpendwa,..kama watoto wawili wanawatosha au laah,,..wanandoa kuwen kitu kimoja mama mkwe hana haja ya kuwaingilia....the strength of a man ndo kila kitu
 
Mpaka mama mkwe amekuletea muongozo ndani ya ndoa yako,amekuona wewe ni mume bwege.kwahiyo hapo huna jinsi ni kuuendeleza ubwege tu.
 
Hugo mama Mkwe hana adabu kabisa, huwez mtamkia Mkwe wako hyo maneno pole sana
 
Back
Top Bottom