Mama mkwe amekuja na mwongozo mkali

Mama mkwe amekuja na mwongozo mkali

ashindwe huyo na hana akili busara ia hana...anaingilia mambo ya familia yako kama vipi zaa naye
 
Mamamkwe hana haki yakukwambia usizae tena na mkeo as llong as wewe ndio una provide familia yako mahitaji yote, ningekua mie nisngetaka hata kujua sababau kwake wala kwa mtoto wake sababu wote wamoja,sababau hawezi kutoka huko mama mkwe akaja kumwambia mumewangu
ujinga kama huo,kwanza mamangu mwenyezi mungu amrehemu hakai hata sehemu na Mume wangu zaidi ya salam amekwenda ndani
hata chakula hali na sie wala chumbani kwangu haingii huyo mama anatabia za wapi mpaka afike kote huko? wasikuumize kichwa usimjibu..
fanya yako huyo mama ndio adui wa ndoa ya huyo zezeta lake humo ndani wait a minute!!! au huyo mama mwanga anaona wajukuu wataliwa?
 
Wakwe wengine watata sana..Huyo kesho ataweza kukwambia hata uache kumgegeda mtt wake...Au kijana mkwe kakuona haujiwezi..Kaamua kukupunguzia majukumu
 
Hivi Juzi Juzi Mama Mkwe Wangu Alikuja Kunitembelea Hapa Kwangu Akitokea Huko Mbwinde. Nilifurahi Sana Kwa Kuwa Ni Muda Sana Umepita Hatujaonana.

Mama Mkwe Hakupoteza Muda Akanipa " Mwongozo " Mzito Na Uliotukuka Kuwa " Nisimzalishe " Tena Mwanae Kwani Watoto Wawili Tuliozaa Mpaka Sasa Wanatosha Na Ni Marufuku Kumzalisha Tena Mwanae Ambaye Ni Mke Wangu Kipenzi Wa Ndoa Na Akafika Mbali Zaidi Baada Ya Kusema Ole Wangu Nikiuke Mwongozo Wake. Hakika Ilikuwa Ni Surprise Ya Nguvu Kwangu Na Ambayo Sijaitegemea Ingawa Hajanieleza Sababu Za Kunizuia Kutafuta Mtoto Wa Tatu. Mama Mkwe Anataka Kucontrol Ndoa Yangu Kwa " RIMOTI " akiwa Mbwinde.

Wakuu Naombeni Msaada Wenu, Maana Mpaka Mama Mkwe Anakuja Mke Wangu Hakunishirikisha Chochote ( Kama Kweli Alikuwa Na Tatizo ) Yeye Akaamua Kumtumia Mama Yake, Sasa Nimekosa Imani Na Mke Wangu Na Nafikiria Kumuacha Ili Aweze Kuongozana Na Mama Yake Pindi Atakaporudi Mbwinde Maana Anaweza Hata Akaniua Kwa Mwendo Huu. Nifanyeje Wakuu Maana Alichofanya Mama Mkwe Mpaka sasa Anaongoza 3-0 Dhidi Yangu Yaani kwa Lugha Nyingine Amenikamata Pabaya Mno Kunakotukuka!!
Mkuu huyo mwanamke mtafutie mke mwenzie heshima itamkuja tuu yeye na mama yake!
 
Mbona simple mkuu mama mkwe atakua anataka mtoto mmoja na wewe halafu huelewi ndo maana kakataza usizae tena na mwanae
Mkuu Nitake Radhi...Yaani Nitembee Na Mama Mkwe?
 
Huyu ni GENTAMYCINE kaja na ID mpya.

Pole sana!!
Nakupa Masaa 24 Uniombe Msamaha Kabla Sijafungulia Silaha Zangu Za NYUKLIA kama SI Za Maangamizi Kwako, Huyo MTU Mimi Simjui Na Uache Kunifananisha Na VINYAGO wako!!
 
Hivi ni kweli Mama Mkwe wako bado anaye Baba Mkwe wako?
 
jipange kwanza ki finance ukiwa tayar mwache arud na mama yake,mama mkwe hawez kuja kukwambia ushenz km huo km kweli anakuheshim
 
Back
Top Bottom