Ndugu zangu napenda kuchukua nafasi hii kwa mtu yeyote aliye karibu na washauri wakuu wa mambo ya kisiasa hapa Tanzania afikishe ujumbe wangu kwa wahusika. Kwanin nasema mama Maria agombee? 1.watanzania wengi wanampenda kwasababu ya busara,utii,na eshima yake wakati wa uwongo zi wa baba wa taifa. 2.MAMA MARIA NYERERe ndiye mwanamke pekee mwenye mvuto na ataweza kuwa raisi wa kwanza mwanamke tanzania 3.namshauri awe raisi kwa muda wa miaka mitano tu! Kwasababu umri umekwenda sana. 4. Ataweza kutuunganisha upya watanzania wote na kusahau chuki na ubinafsi wetu ktk maswala ya muungano,ukabila,dini, na kisiasa,aliyenacho na asiye nacho. Tafadharini wadau fikirieni kwa makini sana jambo hili kwa maslai ya taifa.
Watu wengine bana ni wa hovyo sana
uraisi siyo kuwa na safari za ulaya bali ni kukaa kitako ktk kiti cha kifarume(kiraisi) then unatoa na kupokea mawazo ya washauri wako. Unawaunganisha wananchi wako kwa vitendo.Naanza kukubaliana na mtoa hoja kwa kiasi fulani. Kazi ya Rais huwa ni nyepesi sana kama katiba ya nchi inaeleweka. Kuna mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema kuwa hata kuku anaweza kuingoza America. Alikuwa anamaanisha kuwa katiba nzuri ya America inarahisisha utendaji wa Rais yeyote atakayechaguliwa. Nchi za kiafrika zimekuwa kwenye migogoro ya uongozi siyo kwasababu ya kukosa marais wazuri ila kwasababu ya kukosa mpangilio mzuri wa KATIBA. Kwahiyo ni kweli kuwa hata Mama Maria, pamoja na uzee wake na kukosa elimu kwake bado anaweza kumshinda MKWERRE kama akipewa uongozi kwa KATIBA inayoeleweka.
Saa nyingine kama huna la maana la kusema afadhali ukae kimya!Ama kweli tunao ma "great thinkers", alipotufikisha mumewe ulikuwepo wewe> au unasikia tu?
Ndugu zangu napenda kuchukua nafasi hii kwa mtu yeyote aliye karibu na washauri wakuu wa mambo ya kisiasa hapa Tanzania afikishe ujumbe wangu kwa wahusika. Kwanin nasema mama Maria agombee? 1.watanzania wengi wanampenda kwasababu ya busara,utii,na eshima yake wakati wa uwongo zi wa baba wa taifa. 2.MAMA MARIA NYERERe ndiye mwanamke pekee mwenye mvuto na ataweza kuwa raisi wa kwanza mwanamke tanzania 3.namshauri awe raisi kwa muda wa miaka mitano tu! Kwasababu umri umekwenda sana. 4. Ataweza kutuunganisha upya watanzania wote na kusahau chuki na ubinafsi wetu ktk maswala ya muungano,ukabila,dini, na kisiasa,aliyenacho na asiye nacho. Tafadharini wadau fikirieni kwa makini sana jambo hili kwa maslai ya taifa.
Kupitia chama gani? Au mgombea binafisi. Ina maana hakuna mtanzania mwingine mwenye sifa hizo? Mwacheni mama wa watu apumzike. Matatizo yenu myamalize wenyewe.