Hivi kuna Mtanzania asiyejua sura ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere?

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,167
11,490
Hii serikali imelewa na madaraka! Ni viongozi vipofu wasiojua watanzania wanataka nini? Tukiwaambia taifa liko gizani hakuna umeme hawaelewi wala kusikia! Tuliwaambia maisha mitaani ni magumu hela hakuna pamoja na watu kupambana hawaelewi. Wafanyabiashara wakisema dollar hakuna hawaelewi!

Tukiwaambia nauli za mabasi na daladala hazikamatiki hawaelewi! Tukiwaambia kupanda kwa bei ya mafuta na sukari sasa hivi kilo ni 6,000 hawaelewi, tukiwaambia sasa hivi bima ya afya inakataliwa hospitali za binafsi kwasababu hamuwalipi hawaelewi!

Sasa cha kushangaza juzi imetengenezwa sanamu ya Nyerere chini ya uangalizi wa serikali tukawaambia hii sio sura ya Nyerere bado wanabisha! Sasa tunaiuliza hii serikali ya Bi Kidawa kuwa: Hivi kuna mtanzania asiyejua sura ya Nyerere? Mnatengeneza na kukosea kitu kilichowazi kabisa alafu mnapiga kelele na chapuo kutuaminisha kitu ndicho sio?

Mmetufanya watanzania misukule na mapunguani tusiokuwa na akili?

Kama mnashindwa kutengeneza sanamu yenye sura ya Nyerere mtawezaje kutatua changamoto za umeme? Ukosefu wa madawati shuleni? Maji hakuna! Umeme kila siku unakatwa ili kuuza magenerator ! Hakuna mradi wa maendeleo mpya!

Sasa tuwaeleweje?
 
Kuhangaika na mtu aliefariki ni kupoteza muda uwepo wake ulishafutika hakuna jipya tena
 
Kuhangaika na mtu aliefariki ni kupoteza muda uwepo wake ulishafutika hakuna jipya tena
Sijui nikuiteje? Kijana au mzee? Kila kitu kimejengwa juu ya misingi. Kama unanyumba jua imejengwa juu ya msingi! Hivyo hivyo taifa lolote lile limejengwa juu ya misingi ya watangulizi wake! Tanzania imejengwa juu ya misingi ya Nyerere! Ukimwondoa Nyerere hakuna Tanzania! Waasisi wa mataifa yote duniani walijenga misingi ambayo kwayo hayo mataifa yamesimama ama kwa uzuri au kwa mabaya! Nyerere kwa watanzania ni icon ya Tanganyika &Tanzania! Huwezi ukamwondoa Nyerere!
 
Back
Top Bottom