Mama maria nyerere tunakuomba gombea uraisi tanzania

Dec

Member
Jul 13, 2011
66
26
Ndugu zangu napenda kuchukua nafasi hii kwa mtu yeyote aliye karibu na washauri wakuu wa mambo ya kisiasa hapa Tanzania afikishe ujumbe wangu kwa wahusika. Kwanin nasema mama Maria agombee? 1.watanzania wengi wanampenda kwasababu ya busara,utii,na eshima yake wakati wa uwongo zi wa baba wa taifa. 2.MAMA MARIA NYERERe ndiye mwanamke pekee mwenye mvuto na ataweza kuwa raisi wa kwanza mwanamke tanzania 3.namshauri awe raisi kwa muda wa miaka mitano tu! Kwasababu umri umekwenda sana. 4. Ataweza kutuunganisha upya watanzania wote na kusahau chuki na ubinafsi wetu ktk maswala ya muungano,ukabila,dini, na kisiasa,aliyenacho na asiye nacho. Tafadharini wadau fikirieni kwa makini sana jambo hili kwa maslai ya taifa.
 
Hii ndo itakuwa zawadi tosha kwake na kwa familia yake. Hapendi majigambo thats way hakujenga hata nyumba moja. Nyumba walizo nazo walijengewa bure na jeshi la kujenga taifa tanzania. Atawaunganisha upya watu wote wa mikoa ya arusha,kilimanjaro,mara,mwanza,kigoma,zanzibar.
 
Kupitia chama gani? Au mgombea binafisi. Ina maana hakuna mtanzania mwingine mwenye sifa hizo? Mwacheni mama wa watu apumzike. Matatizo yenu myamalize wenyewe.
 
Zaidi ya kuwa mke wa Mwl JK Nyerere, ana sifa gani nyingine iliyokufanya umuone anafaa kuwa Rais?
 
Ndugu zangu napenda kuchukua nafasi hii kwa mtu yeyote aliye karibu na washauri wakuu wa mambo ya kisiasa hapa Tanzania afikishe ujumbe wangu kwa wahusika. Kwanin nasema mama Maria agombee? 1.watanzania wengi wanampenda kwasababu ya busara,utii,na eshima yake wakati wa uwongo zi wa baba wa taifa. 2.MAMA MARIA NYERERe ndiye mwanamke pekee mwenye mvuto na ataweza kuwa raisi wa kwanza mwanamke tanzania 3.namshauri awe raisi kwa muda wa miaka mitano tu! Kwasababu umri umekwenda sana. 4. Ataweza kutuunganisha upya watanzania wote na kusahau chuki na ubinafsi wetu ktk maswala ya muungano,ukabila,dini, na kisiasa,aliyenacho na asiye nacho. Tafadharini wadau fikirieni kwa makini sana jambo hili kwa maslai ya taifa.

Ama kweli tunao ma "great thinkers", alipotufikisha mumewe ulikuwepo wewe> au unasikia tu?
 
siungi mkono hoja 1. Mama keshazeeka zake mwacheni alee vi2kuu 2. Hana sifa za kutosheleza kuongoza nchi iliyoharibika km TZ 3. Hana nia wala sabb ya kuwa rais wa tz
 
Naona kama mtoa maada ana jitihada za makusudi za kumuua huyu mama kwa mawazo. Nchi iliyovurugwa hivi umkabidhi huyo bibi ataiweza kweli? Kama baadhi ya wachangiaji walivyokwisha sema mwacheni huyo mama apumzike. Hata yeye mwenyewe hiyo ndoto hana na hajawahi kuiota.
 
Ikulu hawabebi zege nyinyi...alafu raisi siyo mtendaji bali ni mshauri tu. Ndomana kunakuwa na makatibu wakuu.
 
Sijui umeandika hii post ukiwa na njaa. Soma kwa makini ulichoandika, jaribu kufikirisha ubongo then uandike tena.
 
Naanza kukubaliana na mtoa hoja kwa kiasi fulani. Kazi ya Rais huwa ni nyepesi sana kama katiba ya nchi inaeleweka. Kuna mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema kuwa hata kuku anaweza kuingoza America. Alikuwa anamaanisha kuwa katiba nzuri ya America inarahisisha utendaji wa Rais yeyote atakayechaguliwa. Nchi za kiafrika zimekuwa kwenye migogoro ya uongozi siyo kwasababu ya kukosa marais wazuri ila kwasababu ya kukosa mpangilio mzuri wa KATIBA. Kwahiyo ni kweli kuwa hata Mama Maria, pamoja na uzee wake na kukosa elimu kwake bado anaweza kumshinda MKWERRE kama akipewa uongozi kwa KATIBA inayoeleweka.
 
uraisi siyo kuwa na safari za ulaya bali ni kukaa kitako ktk kiti cha kifarume(kiraisi) then unatoa na kupokea mawazo ya washauri wako. Unawaunganisha wananchi wako kwa vitendo.
 
Ndugu zangu napenda kuchukua nafasi hii kwa mtu yeyote aliye karibu na washauri wakuu wa mambo ya kisiasa hapa Tanzania afikishe ujumbe wangu kwa wahusika. Kwanin nasema mama Maria agombee? 1.watanzania wengi wanampenda kwasababu ya busara,utii,na eshima yake wakati wa uwongo zi wa baba wa taifa. 2.MAMA MARIA NYERERe ndiye mwanamke pekee mwenye mvuto na ataweza kuwa raisi wa kwanza mwanamke tanzania 3.namshauri awe raisi kwa muda wa miaka mitano tu! Kwasababu umri umekwenda sana. 4. Ataweza kutuunganisha upya watanzania wote na kusahau chuki na ubinafsi wetu ktk maswala ya muungano,ukabila,dini, na kisiasa,aliyenacho na asiye nacho. Tafadharini wadau fikirieni kwa makini sana jambo hili kwa maslai ya taifa.

He jamani......lazima tuangalie upya taratibu za kusajili JF, siyo kuruhusu kila mtu aingie kwenye jukwaa. Vinginevyo....tutapata mambo ya ajabu kupindukia humu....
 
Naamini watanzania tunahitaji busara za wazee wetu wakina mama maria. Kwasababu yeye ndiye alikuwa mshauri mkubwa wa baba wa taifa mpaka tukawa pamoja.
 
Kupitia chama gani? Au mgombea binafisi. Ina maana hakuna mtanzania mwingine mwenye sifa hizo? Mwacheni mama wa watu apumzike. Matatizo yenu myamalize wenyewe.

sipendi kusema maswala ya vyama. Huyu mama ndiye atakuwa mwanamke wakwanza kuitawala tanzania. Tutakuwa na historia nzuri ktk afrika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom