Leo tarehe 15 August Wakristo Wanaadhimisha Sikukuu Ya Kupalizwa Mbinguni Bikira Maria

Joseph Gadiel

JF-Expert Member
Dec 23, 2022
374
629
images.jpg

Ufunuo 12:1
"Kisha, ishara kubwa ikaonekana mbinguni: Mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!"

Luka 1:26
"Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, kwa msichana mmoja bikira aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu, ewe uliyejaliwa neema na Mungu! Bwana yuko nawe!” Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: Maneno hayo yanamaanisha nini? Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu. Yeye atakuwa mkubwa na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu"

Utangulizi: Tafakari ya Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni Bikira Maria: Bikira Maria ni ishara na tumaini thabiti na ya faraja kwa taifa la Mungu linalosafiri. Tunaposherehekea Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni Mama Bikira Maria, tunajifunza kuwa, Mama wa Yesu, akiwa amekwisha tukuzwa mbinguni mwili na roho, ni sura na mwanzo wa Kanisa ambalo litapata utimilifu wake katika ulimwengu ujao. Kadhalika anang’aa duniani kama alama ya hakika ya matumaini na ya faraja kwa Taifa la Mungu lililo safarini, mpaka siku ya Bwana itakapokuja (taz. 2Pet 3:10; Lumen Gentium, n. 68). Somo la kwanza: Ufunuo 11-.19; 12:1-6.10. Somo la pili: 1 Wakorinto 15:20-26. Injili: Luka 1:39-56. Karibu mpenzi msikilizaji wa Radio Vatican katika tafakari hii, leo ambapo Kanisa linaadhimisha Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni Mama Bikira Maria Mtakatifu.

Tafakari: Moja ya mafundisho haya ya Kanisa ni kutoka katika somo la kwanza tulilosikia, kutoka kitabu cha Ufunuo wa Yohane 11:19; 12:1-6.10. Katika somo hili, Mababa wa Kanisa wanafundisha kuwa, kwanza somo linazungumzia mwanamke ambaye ni sura ya taifa la Mungu, ambalo ndilo Kanisa, ambapo pia Maria anawakilisha sura ya taifa la Mungu yaani Kanisa. Simulizi hili la joka linaturudisha kwenye kitabu cha Mwanza 3:15 ambapo Mungu aliweka uadui kati ya mwanamke na nyoka na kati ya uzao wa mwanamke na uzao wa nyoka ambaye ni shetani. Mwanamke aliyevikwa jua. Hii ni ishara ya kuwa mwanamke huyu amepambwa kwa neema za Mungu (salamu uliye jaa neema – salamu ya Malaika Gabrieli kwa Bikira Maria). Na mwezi chini ya miguu yake, maana yake kuwa mwanamke huyu hatapotea wala kuamgamia, bali ataishi milele. Na juu ya kichwa chake taji ya nyota 12, zinazowakilisha makabila 12 ya wana wa Israeli. Pia huwakilisha Mitume 12 ya Yesu, ikiwa na maana ya utawala wa Kanisa katika ulimwengu. Naye alikuwa na mimba akilia hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa. Hii li lugha ya picha inayoonesha mateso ya wokovu yaliyoletwa au kutimizwa na Kristo pale msalabani na hatimaye kufufuka kwa ushindi. Naye akazaa mtoto wa kiume – huyu ndiye Kristo Yesu Mkombozi wa ulimwengu, na mtoto huyu akanyakuliwa hata kwa Mungu, picha ya mateso, kifo, ufufuko na kupaa mbinguni kwa Kristo. Mwanamke akakimbilia nyikani, hii huwakilisha ukimbizi wa Wakristo wa kwanza kwa sababu ya mateso.

Tuhitimishe tafakari yetu kwa kusema kuwa tusihofu kumsifu Maria kwa sababu kila mara tunapomsifu Maria, yeye mara moja huzigeuza sifa hizo kuwa za Mungu. Ndio maana Elizabeti alipomsifu, mara moja Bikira Maria akasema “Moyo wangu wamtukuza Bwana...” Utenzi huu unaeleza hali ya kiroho ya Bikira Maria, na hakuna kitu kikubwa zaidi ya hali hii ya kiroho kwa ajili ya kutusaidia kupata uzoefu wa Fumbo la Ekaristi. Ekaristi imetolewa kwetu ili maisha yetu, kama yale ya Bikira Maria, yawe ya ukuu kabisa. Kwa maana “Mama anapoheshimiwa, Mwana hupata kujulishwa, kupendwa na kutukuzwa inavyostahili, na amri zake kushikwa, kwa kuwa katika Yeye vitu vyote viliumbwa (rej. Kol 1:15-16) na katika yeye ilimpendeza Baba wa milele utimilifu wote ukae (rej. Kol 1:19).” Tumtazame Bikira Maria, yeye anatufungulia matumaini ya wakati ujao uliojaa furaha na anatufundisha njia ya kuufikia: yaani kumpokea mwanaye kwa imani; daima tusipoteze urafiki wetu na mwanaye, bali tujiachilie ili, Mwanaye atuangazie mwanga wake na atuongoze kwa Neno lake; tumfuase mwanaye kila siku, hata nyakati ambazo tunahisi misalaba yetu kuwa mizito. Maria Sanduku la Agano Jipya aliye Mbinguni, anatuonesha kwa mwanga halisi kwamba tupo katika njia tukielekea katika nyumba yetu ya kweli, yaani ushirika wetu wa furaha na amani pamoja na Mungu. Hivyo, waamini wote wakristo wamsihi kwa nguvu Mama wa Mungu na Mama wa wanadamu, ili yeye aliyeusaidia mwanzo wa Kanisa kwa maombezi yake, pia sasa aliyetukuzwa mbinguni, juu ya Wenye heri na Malaika, awaombee kwa Mwanawe katika Ushirika wa Watakatifu wote, mpaka jamaa zote za Mataifa zilizopambwa jina la Kristo au zisizomjua bado Mwokozi wao, zikusanyike kwa furaha kuwa Taifa moja la Mungu katika amani na mapatano, kwa utukufu wa Utatu Mtakatifu sana usiogawanyika. Amina.

Tumsifu Yesu Kristu!
 
Ni vizuri ila Wakristo tuna pingana sisi wa Sabato tunaona wa Catholic kama wenye ile arama ya 666.
 
Ila hapo wakristo umejumuisha wote ungeweka tu wakatoliki..
Kama wanaamini kweli ktk Kristo Yesu aliyezaliwa na Bikira Maria akawekwa kati yetu kwa umbo letu la ubinaadamu siyo vibaya nao wakaungana na Wakatoliki kuadhimisha siku hii maalumu kwa heshima kwake.

Siyo kwa ubaya lakini,otherwise kwa hekima ya mods wanaweza rekebisha heading iseme tofauti!
 
Mimi ni Mkristo ila sikubaliani na fundisho la bikira Maria kuitwa Mama wa Mungu, au kwamba alipalizwa. Kwahiyo usijumuishe Wakristo wote kwenye huo utopolo.
Wewe huna imani ya ukatoliki mengi tunaamini tu ili ya ishe hicho ndo kinacho itwa imani wewe usilete logic zako hapa, Dini ya RC haina logic kabisa, wewe ulisha wahi kuona wapi 1+1+1=1!!!! Ila kwa imani ya kikatoliki ni sawa, Mungu baba+ Mungu mtoto+ Mungu roho mutakatifu =1mungu moja
 
Usikaze fuvu kuleta battle zisizokuwa na maana wewe elewa nilichokuambia kwamba simama ktk dini yako usia-act vitu ambavyo huwezi kuwa
Kuna free entry and free exit katika kila dini sihitaji membership card kua mkristo wala sihitaji kukutaalifu kwamba leo nimeingia ukristo acha watu watumie uhuru wao wa kuabudu wanavo taka.
 
Wewe huna imani ya ukatoliki mengi tunaamini tu ila yaisha hiyo ndo konacho itwa imani wewe usilete logic yako hapa wewe ulisha wahi kuona wapi 1+1+1=1!!!! Ila kwa imani ya kikatoliki ni sawa Mungu baba+ Mungu mtoto+ Mungu roho mutakatifu =1mungu moja

Mungu ni wingi katika umoja,ndio mana maandiko yanasema na tumfanye mtu sio nimfanye mtu. Manake ni wingi huo.

Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

Mwanzo 1:26
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom