Mama Kijo Bisimba alaani kauli za Magufuli juu ya Mwanamke. Asema kauli zake hazimfai mtu aliyekalia kiti cha Ofisi ya Rais

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,506
51,111
Mwanamama mtetezi wa siku nyingi wa haki za binadamu hususan za wanawake mama Kijo Bisimba, amelaani vikali kauli za Rais Magufuli anazozitoa mara kwa mara juu ya wanawake.

Akihojiwa na redio moja ya nje, Mama Bisimba amesema, kauli hizo za Magufuli zisichukuliwe kimizaha mizaha kwa sababu hizo kauli zinaweza kupelekea unyanyasaji mkubwa na ubaguzi.

Mama Bisimba amesema, haifai mtu aliyekalia ofisi nyeti kama ya raisi kutoa kauli za udhalilishaji kama huo. Ameshangaa kuona Magufuli mara kwa mara akimgeuza Mwanamke kama chombo cha mizaha.

Akieleza kwa umakini mkubwa, Mama Bisimba anasema watu wengi wanashangazwa na tabia hii ya Magufuli hadi wanajiuliza, huyu mzee ana shida gani na wanawake?.

Mama Bisimba akatolea mfano, namna Magufuli alivyokuwa akielezea uamuzi wake wa kumchagua Mama Samia Suluhu kuwa mgombea mwenza wake alipotoa kauli kuwa kwanza huyo mama ni mweupe mweupe.

Maelezo haya ya mama Kijo yanafuatia kauli ya juzi ya Rais Magufuli aliposema kuwataka wananchi wamchague mgombea ubunge mwanamama mmoja wa Dar ambapo alisema yeye hutoa ushirikiano mzuri wa kikazi kwa wanawake weupe na siyo wanawake weusi.

Kabla ya hapo alipokuwa huko mkoani Magufuli alisikika kwenye mkutano wa kampeni akisema kuwa atafutiwe kasichana kadogokadogo!

Huko nyuma amewahi kutoa kauli kuwa kama watu wa mikoa ya kusini wangeanzisha sintofahamu juu ya suala la Korosho, basi ambacho angeanza nacho ni kupiga shangazi zao ( yaani wanawake)

Wakati huohuo, mpinzani mkubwa wa Magufuli katika uchaguzi mkuu huu ndugu Tundu Lissu, ameendelea kuhoji kauli hizi za Magufuli, Lissu anahoji kauli ya Magufuli siku chache kabla ya kampeni pale Magufuli alipopewa jogoo akiwa njiani kutokea Lupaso, na kwa mizaha akamwambia yule mzee aliyempa jogoo kuwa laiti angekuwa nyumbani kwao huko Chato angemuozesha mama yake. Kauli hii imeleta mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wengi wameonyesha kutoifurahia kauli hiyo. Iweje mtoto awe mshenga au kuwadi wa mama yake?

MY TAKE:
Rais Magufuli aache kutoa kauli za mizaha na utaniutani juu ya wanawake. Hawa ni mama zetu, ni dada zetu, ni bibi zetu, ni wake zetu, ni dada zetu), wanastahili kuheshimiwa. Si sahihi kila wakati akishika mike basi anaanza kutoa kauli tata kuhusu mwanamke.

Kuwa kwake msukuma, au kutokea kwenye background ya jamii ya mfumo dume hakumpi uhalali kumgeuza mwanamke kama mwanasesere wa kufanyia mizahamizaha.

Yeye ni mtu mkubwa sana katika nchi, na ofisi yake ni kubwa sana. Kauli zake si tu zinaweza kuathiri wanawake humu nchini, bali zinaweza kuathiri mtu mweusi yeyote duniani kwa kuendelea kubaguliwa sababu ya rangi ya ngozi yake.

Pia kuwa raisi haimaanishi anamiliki kila mtu na kwamba anaweza kusema lolote na chochote mahali popote na eti ikawa chereko tu, hapana tunataka mtu anayekalia kiti cha rais apime kauli zake, aangalie athari yake kwa jamii kuanzia watoto wadogo hadi wazima, atazame muktadha mzima wa mahusiano ya kijamii nchini na hadi kimataifa ndo aamue kuzungumza au kuacha!. Siyo kila kitu chafaa kwa utani!

Tumewahi kuwa na maraisi wanne kabla yake, na walikuwa wakifanya utani wa hapa na pale katika mazingira muafaka, lakini hawakwenda mbali huko anakokwenda Magufuli kwenye utani juu ya utu wa mtu na rangi za ngozi.

Magufuli anaonyesha "obsession" iliyopitiliza kwenye issue za wanawake, na hili kusema kweli halifai kwa mtu mwenye hadhi ya nafasi ya ofisi aliyoikalia!.

Hapa chini ni kauli za mama Kijo Bisimba:

 
Ukimsikiliza Jiwe sana

1. Haheshimu wanawake kabisa anawaona ni watu duni kwake

2. Likely yuko very obsessed sana na mambo yale

3. Hajali kuumiza hisia za mkewe hadharani

4. Anadhani kwa kuwa ni mtu mkubwa basi anaweza kuzungumza chochote with impunity

Msikilize JPM hapa akitoa kauli za ajabuajabu juu ya mwanamke:


 
Kikao cha wamanzego wasio na uhakika wa kupiga kura. Wakuu msiishie kumwaga povu hapa mkapige kura pia
 
Inaonekana Jiwe hana mapenzi ya dhati kwa mkewe.

Huwezi kuwa na mke mweusi halafu kwenye hadhara zako mbalimbali unaonyesha kutovutiwa na wanawake wa aina hiyo!
 
Huyu mtu naamini hata mkewe pamoja na ndugu, marafiki na jamaa zake wengine wa jinsia ya kike hawatampa kura kabisa. Wanaishi naye tu kinafiki kwa ajili ya maslahi yao binafsi, ila mioyoni mwao wanafadhahishwa mno na kauli na matendo yake, wana jambo lao ifikapo siku ya Jumatano ya tarehe 28-10-2030.
 
Back
Top Bottom