Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,653
- 25,661
Huko Botswana kwa mdada wa kibongo kucheat si rahisi, wale ni watu wazima, hawapitii jando.
Mkuu, umeniacha hapo au labda nimeleewa vingine, (maambukizi)
Huko Botswana kwa mdada wa kibongo kucheat si rahisi, wale ni watu wazima, hawapitii jando.
Afadhali umetuburudisha na hadithi hii tamu na kusisimua tumechoka na siasa. Ni hivi vipi huyo mchumba aliyeko Botswana akaja kusema amepata mchumba huko aliko!Samson hakusoma alama za nyakati hahahhaah akikuambia mama mzazi ukamsalimie jua amewathibitishia Nina mchumba xyziiii.Alipomuona Samson alishajijengea picha kuwa yeye ndiye mke, alishaiaminisha akili yake hivyo.
Si aliyajaza kwenye kapu mwenyewe lazima tu alionjaaSamson hakula tunda???

Thats the beaty of the 21st century. MemesThese memes
HoooHii ni hadithi au true story?
Mwanaume kamili wa kiafrika akae miezi sita bila sex then
papucci ijipendekeze halafu aitolee nje
Kama ni kweli basi aliyekuhadithia kuna episodes nyingi sana ameziruka
Habari za leo wapendwa,
Hii story nimepewa na swahiba wangu ambae anafanya kazi na kuishi Dar, nitampa jina la Samson katika story hii.
Haha umenikumbusha Sunday school jamaninywele, nywele zake zilikuwa ndefu. alikuwa bado kunyolewa...........
Hahaha wanawake wabovu wanasoko gumu sanaHabari za leo wapendwa,
Hii story nimepewa na swahiba wangu ambae anafanya kazi na kuishi Dar, nitampa jina la Samson katika story hii. Samson ana umri wa miaka 35+ hajaoa, ni mfanya kazi katika taasisi moja ya serikali. Samson alikutana na mchumba wake UDSM miaka mingi iliyopita, katika kuhangaika na maisha mchumba alipata kazi Botswana. Kwa kila vigezo Samson anajua huyu ndiye mke mtarajiwa, na mahari imeshalipwa, kinachotatiza ni kuwa wote wana career na mchumba kwakweli anapenda maisha ya Botswana na anamshawishi sana Samson kuhamia kule. Samson pamoja na ajira ana miradi ya hapa na pale mjini na anafahamu kuwa akienda Botswana mwisho wa siku yeye ni mtanzania na kuna umuhimu wa kuwekeza nyumbani. Uhusiano wao ni kuwa kila mwaka Samson anakwenda likizo Botswana na mchumba anakuja likizo Dar, inaweza kuchukua miezi sita wawili hawa hawaja onana.
Miezi michache iliyopita ofisni kwa kina Samson aliajiriwa mdada, yuko kwenye late 20's au early 30's hivi, kwa hapa nitamrefer kama dada A. Dada A dada alipomuona Samson moyo wake ulitokea kumpenda, alijitahidi sana kuwa karibu nae, alianza kumkaribisha kanisani kwao, Samson alikumbuka kuwa ni muda mrefu hajakwenda kanisani, labda huyu ametumwa na Mola kuja kunikumbusha jukumu hili, basi walikwenda kanisani J2 ya kwanza, A alianza kumweleza Samsoni kwamba yeye ni mgeni kabisa Dar, ingawa alikuwa anakuja likizo kwa mama mdogo akiwa mwanafunzi, na baada ya kupata kazi mama mdogo amempokea na kwasasa ndiko anakoishi.
Pamoja na kuwa Samson hajaoa lakini anamheshimu sana mchumba wake, na ni utaratibu aliojiwekea kuwa hakaribishi mwanamke yeyote nyumbani kwake. A alisubiri kukaribishwa kwa Samson, aliona hilo halitokei, alipanga kichwani kwake kuwa labda akiwa na kwake Samson atakuwa anakuja kumtembelea. Alianza kumwambia Samson anataka kuhama kwa mama mdogo aanze kujitegemea, ingawa Samson alipinga sana wazo lile, kama mdogo wake, alimshauri aweke pesa zake ili afanye makubwa baadae kama anapo mahali pa kukaa.
Kero zilipokuwa nyingi, Samson alimsaidia A kutafuta nyumba katika moja ya nyumba za marafiki zake, alipata guest wing ndogo inayojitosheleza. A alihamia, baada ya kama wiki mbili baada ya kuhamia nyumba mpya, A alimwambia Samson mama yake amefika kutoka mkoani, hivyo J2 watakwenda wote kanisani na mama, Samson alishtuka kuwa, hii sasa inakuwa familiar zaidi ya uparokia, alimwambia A, kwamba J2 ile hataweza kwenda kanisani. A alisisitiza sana aende basi jioni kumwona mama, na pia kumkaribisha nyumbani kwake rasmi.
Samson alipitia sokoni alinunua matunda mengi tu kwenye kikapu, aliona si uungwana kwenda mikono mitupu ulipokaribishwa. Nyumbani alimkuta A, mama yake na mama mdogo wakimsubiri kwa hamu, baada ya salamu na vinywaji kutengwa, A alianza, mama na mama mdogo huyu ndiye Samson labda kwenu atawaeleza zaidi mipango yake kwangu.
Samson ilibaki kidogo tu kinywaji alichokuwa anakunywa kuingia kwenye njia ya hewa, alipata mshtuko wa ghafla. Akiwa kama mwanaume, ilibidi awaeleze wakina mama habari za mchumba wake alieyoko Botswana. A alibaki na hali ambayo imechanganyika aibu na mshangao.