Mama Hamisa asema anataka mwanae aolewe na Mzungu, Waafrika hawafai

View attachment 747024

Mama wa mwanamitindo, Hamisa Mobeto, Shufaa Rutiginga amesema katika maisha yake alikuwa anamuombea mtoto wake huyo aolewe na mzungu.

Akizungumza na MCL Digital, Shufaa amesema sababu ya kutaka aolewe na mtu wa aina hiyo ni kutokana na wanaume wa kiafrika kutokuwa na mapenzi ya kweli.

“Unajua mtoto wangu ni mzuri, mrefu ana shingo nzuri nataka mwanaume atakayemuoa amuangalie kama malaika, kama malkia kwa kuwa ni mwanamke mwenye misimamo yake na ametulia sio muhuni kama watu wanavyomfikia.

“Wazungu hawana ‘stress’ wanajua namna ya kujali mwanamke, hawanaga mambo ya longolongo linapokuja suala zima la mapenzi tofauti na wanaume wetu wa kiafrika,”amesema.

Kuhusu suala la kuzaa na wanaume tofauti, mama Hamisa amesema hilo kwake halimpi shida na angependa amletee wajukuu wengi zaidi kwa kuwa yeye alijaliwa kumzaa peke yake na kudai kwamba hao ndio ndugu zake.

Ni kutokana na hilo, amesema anatamani amzalie watoto sita, kwa kuwa sasa hivi ana nguvu za kulea wajukuu zake na siku hayupo duniani hao ndio watakuwa ndugu zake na kuweza kumsaidia.

Mpaka sasa Hamisa ana watoto wawili.


Chanzo: Mwananchi
Ukoloni hautokaa uishe.. Lakini pia this is another bullshit thinking from African women... Kumbe huyu mama ana mawazo kimo cha mbilikimo kiasi hiki... Anasifia uzuri wa mwanae hajui hujafa hujaumbika!?
Na angemjua mzungu ni nani katika uhalisia wake asingehara kiasi hiki
 
Yaani Tz, mtoto akipata umaarufu kidogo tu; mama zao nao wanafuata!

Karibia naye mtasikia ana kiben 10, si bure.

Mawazo takataka kabisa.
Naona huyo mama hana mume mwafrika.
Hamisa, baba yake ni mzungu bila shaka.
Basi tu nimekuwa mtu mzima sasa... Ningemtokea huyo nimpe habari yake kwa vitendo
 
Anamuona mtoto wake ameishakuwa kipolo anaanza kujifanya anataka wazungu yeye asubirie tu na mjukuu wa 3 huku mwanae bado akiwa nyumbani
 
Back
Top Bottom