Mama Hamisa asema anataka mwanae aolewe na Mzungu, Waafrika hawafai

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
pic+mama+mabeto.jpg

Mama wa mwanamitindo, Hamisa Mobeto, Shufaa Rutiginga amesema katika maisha yake alikuwa anamuombea mtoto wake huyo aolewe na mzungu.

Akizungumza na MCL Digital, Shufaa amesema sababu ya kutaka aolewe na mtu wa aina hiyo ni kutokana na wanaume wa kiafrika kutokuwa na mapenzi ya kweli.

“Unajua mtoto wangu ni mzuri, mrefu ana shingo nzuri nataka mwanaume atakayemuoa amuangalie kama malaika, kama malkia kwa kuwa ni mwanamke mwenye misimamo yake na ametulia sio muhuni kama watu wanavyomfikia.

“Wazungu hawana ‘stress’ wanajua namna ya kujali mwanamke, hawanaga mambo ya longolongo linapokuja suala zima la mapenzi tofauti na wanaume wetu wa kiafrika,”amesema.

Kuhusu suala la kuzaa na wanaume tofauti, mama Hamisa amesema hilo kwake halimpi shida na angependa amletee wajukuu wengi zaidi kwa kuwa yeye alijaliwa kumzaa peke yake na kudai kwamba hao ndio ndugu zake.

Ni kutokana na hilo, amesema anatamani amzalie watoto sita, kwa kuwa sasa hivi ana nguvu za kulea wajukuu zake na siku hayupo duniani hao ndio watakuwa ndugu zake na kuweza kumsaidia.

Mpaka sasa Hamisa ana watoto wawili.

Chanzo: Mwananchi
 
Hivyo ndivyo wanavyodanganyana watu wa huko daslam! Yaani wanataka wajifanye kuwa sisi wanaume wa kiafrika hatuna jipya na huko anakokimbilia nako hawamtaki! Yaani tabu tupu.
 
View attachment 747024

Mama wa mwanamitindo, Hamisa Mobeto, Shufaa Rutiginga amesema katika maisha yake alikuwa anamuombea mtoto wake huyo aolewe na mzungu.

Akizungumza na MCL Digital, Shufaa amesema sababu ya kutaka aolewe na mtu wa aina hiyo ni kutokana na wanaume wa kiafrika kutokuwa na mapenzi ya kweli.

“Unajua mtoto wangu ni mzuri, mrefu ana shingo nzuri nataka mwanaume atakayemuoa amuangalie kama malaika, kama malkia kwa kuwa ni mwanamke mwenye misimamo yake na ametulia sio muhuni kama watu wanavyomfikia.

“Wazungu hawana ‘stress’ wanajua namna ya kujali mwanamke, hawanaga mambo ya longolongo linapokuja suala zima la mapenzi tofauti na wanaume wetu wa kiafrika,”amesema.

Kuhusu suala la kuzaa na wanaume tofauti, mama Hamisa amesema hilo kwake halimpi shida na angependa amletee wajukuu wengi zaidi kwa kuwa yeye alijaliwa kumzaa peke yake na kudai kwamba hao ndio ndugu zake.

Ni kutokana na hilo, amesema anatamani amzalie watoto sita, kwa kuwa sasa hivi ana nguvu za kulea wajukuu zake na siku hayupo duniani hao ndio watakuwa ndugu zake na kuweza kumsaidia.

Mpaka sasa Hamisa ana watoto wawili.

Chanzo: Mwananchi

Ukiichukua IQ ya huyo Mama na ya Mwanae ( Binti yake ) ukaichanganya unaweza usipate kabisa Tiba ya Kuondoa ' Upumbavu ' uliokithiri ndani ya ' Ubongo ' wa Mwanadamu Mwafrika.
 
Urefu na ana shingo nzuri ndo sababu anazoona mwanae ni mzuri

huyu maza anazeeka vibaya kumbe

Mwambieni aje na njia hii ya kuja Rwanda aje aone shingo za ukweli lkn bado hawaolewi
Nimeingia kusoma post yako tu
 
Back
Top Bottom