Mama Anne Killango Malecela ndani ya TBC

Du hata mimi nimebahatika kukiona mwishoni ,kwa kweli Mama Kilango katoa somo zuri la maisha na mambo yote kaweka hadharani,pia nimefurahi kumuona shemeji yetu Mzee Malecela akiwa amerelax hongera wote,Mzee pamoja na kuwa sasa umeenda Same usisahau kukaja Mbeya shemeji zako bado wapo pale Mwanjelwa mheshimiwa!
 
Charles Nyange ndio nani tena acha kuchafua hali ya hewa bana hah hah waswahili bana hakuna dogo mnapekua mpaka chini ya mvungu sasa akina mama lion watashindwa kutupa butamu ba maisha yao jameni
 
Huyu ni mama na mpiganaji. Ni transparent in any way!! Haogopi! Huyu ex hubby Nyange, pole sana. Pengine alikuwa goigoi maana kwa kawaida wachapakazi wowote wale wawe wanaume au wanawake hawataki magoigoi. Keep it up mama. I wish wanao wanne hata mmoja ataiga mfano wako, being a strong woman/man.

Wanaume wanyanyasaji wajifunze!
Hakuwa goi goi bali mnyanyasaji wa hali ya juu na sasa kafulia big time!
 
Charles Nyange ndio nani tena acha kuchafua hali ya hewa bana hah hah waswahili bana hakuna dogo mnapekua mpaka chini ya mvungu sasa akina mama lion watashindwa kutupa butamu ba maisha yao jameni

#20
post_old.gif
Yesterday, 08:35 PM
mfianchi
user_offline.gif

mfianchi has no status.
Senior Member
red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png
green.png
green_right.png
Join Date: Wed Jul 2009
Posts: 199
Thanks: 4
Thanked 28 Times in 25 Posts
Rep Power: 21
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif

icon1.gif
Re: Mume wa bi sofia simba
Yanatuhusu mtu akiwa kiongozi lazima tuingie mpaka mvunguni kumjua bana kwani anatakiwa kuwa mfano kwa jinsi anavyoishi yeye mwenyewe,je kiongozi akiwa na sifa mbaya kwa mfano za kuwa na nyumba ndogo mtu kama huyo lazima akiwa kiongozi atakuwa na tabia chafu so ni muhimu kujua viongozi wako the way wanavyoishi,pole mzee KK si ajabu saa hizi ni historia baada ya mamsap kuula kutesa kwa zamu bana nani angemkataa KK enzi hizo akiwa pale Karimjee thubutu
 
Mama anajua kupangilia hoja na anajua kuweka hisia ktk hoja ili msikilizaji asikie ladha ya uchungu au utamu wa hoja zake.

Ila kitu kimoja. anafaa sana akiwa pembeni maana akiingia ktk kilinge cha kabinet ataboronga kwani she dont speak their language and she might be forced to bend down low... hapo ndipo laana zetu zitamwendea.

Ada ya mtakatifu ni kudumu ktk sala na kutenda mema ili awashawishi wengine kuwa watakatifu.
 
Hata mm sijakiona ila nimesimuliwa, nasikia kilikuwa kipindi kizuri sana....Big up kwa mtayarishaji Suzana Mungy, tuletee na wengine tena hata kama si wanasiasa tuwafahamu..Mama Lowasa, Mama Mengi, Mama Zakhia Meghji, Mama Anna Abddalla n.k
 
Mama mengi yupo kweli nasikia waliachana na mzee siku nyingi
 
Du! Mama kaongea mambo mengi sana ya siasa, maisha mpaka yale ambayo ni very personal ya past life yake na hata ya kwake na Mzee Malecela.
Afadhali sijasikiliza coz very unfortunately sipendi kusikia personal ishuz za watu wengine. Hapo kwenye s.i.a.s.a labda but not that much pia. hii kitu bongo hakuna ndio tunafanya rehersal
 
mume wa kwanza wa anna kilango anaitwa charles nyange. huyu bwana alikuwa finance controler wa tanzania breweries tbl miaka ya 80, na anna kilango alikuwa mwalimu wa commerce na bookkeeping kisutu sekondari. charles na anna wamezaliwa kijiji kimoja wilayani same. charles nyange ni mdogo wake elizabeth nyange yona, ambaye ni mke wa daniel yona ndhira. anna kilango anafanya makosa makubwa kuizungumzia ndoa yake iliyovunjika kwenye vyombo vya habari. ex wake akiamua kuzungumza hali ya hewa inaweza kuchafuka na kurudia yale magomvi yao ya miaka ya 80 ambayo kila mzee wa kipare hapa mjini alishindwa kuyasuluhisha. ngoja niachie hapa maana hili ni bomu lisijenilipukia mwenzenu.
 
- Hatred na huyu mama, mkuu alikukosa nini hasa ambacho akitajwa tu ni lazima uje na hatred mara za kuuza unga, mara bomu acha hizo mkuu, jaribu kuelewa historia ya mama shujaa ambayo inapaswa kuwa an inspiration kwa kina mama wote wasiojiamini mbele ya wanaume wajinga wajinga kama mume wake wa kwanza,

- Ambaye alikuwa na kimada wa muda mrefu sana kwa siri, aliposhikwa na kuwa-confronted bado alikuwa na nerves za kuchukua pasi ya moto na kumchomeka nayo mama mwilini kwa hasira na kumuachia kovu zito sana mwilini, ingekua majuu au kwenye nchi zinazofuata sheria huyu Nyange alitakiwa kufa jela, lakini mama kwa ushujaa akamfukuza kwenye nyumba na kubaki na watoto wadogo wanne, ambao through hard working peke yake ameweza kuwasomesha mpaka sasa mmoja ni Director wa Stanbic bank, mwingine ni mwanasheria maarufu wa kujitegemea hapa mjini aliyemaliza MBA UK, mwingine anamaliza MBA ya uchumi kule Minneapolis, na mdogo kuliko wote sasa hivi anamalizia BA ya sheria kule Bangalore, India.

- Hivi ni kina mama wangapi bongo wameweza kufikia hatua kubwa namna hii baada ya kukataa kufanywa wajinga na kina baba wasio ana akili kama huyu Nyange! I mean mkuu acha hizi hatred against huyu mama, she is a fighter na sisi wengine wote ma-fighter wa maisha kama yeye tunamuheshimu sana tutamtetea to the end kila unapojaribu kumshambulia bila sababu as you always do, Mungu ampe nguvu na ampe busara za kuweza kuyaweka maisha yake kwenye vitabu ili viweze kuwasaidia wanyonge wengine hasa hawa mama zetu, ili waelewe kwamba sio lazima kukubali abuse za kina baba, na pia iwe inspiration za kuanzishwa kwa sheria za kuwalinda kina mama na abusive husbands na hasa domestic violence!

Respect.

Field Marshall Es!
 
Field Marshal ES,
wakale walisema, "ukiishi kwenye nyumba ya vioo kamwe usitupe mawe." masuala ya charles nyange na anna kilango ni bomu linaloweza kukulipukia watu wakapatwa na aibu kubwa mbele ya jamii. kwamba charles alimchoma anna na pasi ya moto ni habari ya kutunga. kwamba anna alimfukuza charles toka nyumba walimokuwa wakiishi ni uongo mwingine. shauri la ndoa ya charles na anna lilifika mpaka mahakamani na kama kungekuwa na masuala ya kuchomana kwa pasi basi mahakama ingeweza kumhukumu charles kwa shambulizi hilo. tatizo lako unafikiri huyu mama ni malaika hivyo kila anayemgusa hata kwa mbali lazima umshambulie kwa matusi. halafu unajidai kutuletea habari za watoto wake kututisha kwamba unamjua vizuri. wengine tuna data zao toka kwenye sherehe ya harusi yao pale ukumbi wa ifm, kabla na baada ya hapo.
 
- Yale yale tu mkuu huna jipya, mama sio malaika wala hakuna bina-adam ambaye ni malaika duniani ila huwezi kumchafua bila facts, aliyekwenda mahakamani ni yeye mama kudai talaka na nyumba ili alelele watoto, na alama nzito sana iliyoachwa na ya pasi ya moto anayo mwilini mkuu, nafikiri kwenye hili sina mengi ya kusema maana facts zinajisema wazi na uongo unajiweka wazi, ya watoto wake useme kama ni uongo au?

- Punguza jazba na chuki na mama mkuu!
ninasema hivi mama aandike kitabu cha maisha yake kuwasaidia kina mama wanyonge na kusaidia kutungwa kwa sheria za domstic violence kwa taifa letu maana wapo kina mama wengi wanaoteswa na wajinga wajinga wasioelewa ubin-adam, mama anastahili heshima nzito on her personal life maana she is a real fighter!

es!
 
Field Marshal ES,
wenye busara zao hawawezi kuzungumza masuala ya ndoa ya kwanza ya anna kilango kwenye ukumbi kama jamii forums. anna naye anakosa busara kama mwanasiasa kumzungumzia mtalaka wake kwenye vyombo vya habari. kama wewe na anna kilango mnaona ni ujanja endeleeni.
kuhusu facts wewe ndiye uliyeleta uongo kwamba anna kilango alimfukuza mumewe toka kwenye nyumba. nikakueleza kwamba suala hilo lilienda mahakamani, sasa umerudi na kurekebisha post yako. kama mama alichomwa kwa pasi mahakama ilikuwa na uwezo wa kushughulikia suala hilo kama jinai. hapo inaonyesha kwamba unasema uongo.
mwisho, hii damage contol unayofanya hapa inatokana na mama kilango kukosa umakini na kuanza kuzungumzia masuala yake ya zamani. mshauri ajikite zaidi kwenye present, maisha yake kama mbunge, mke wa mh.john malecela, na bibi kwasababu sasa ana wajukuu, na uchaguzi wa 2010.
 
- Ngoja nijaribu kukuelewa, eti wenye busara zao hawawezi kuzungumzia ndoa zao hapa JF, lakini na wewe mwenyewe uko mstari wa mbele kuzungumzia ndoa ya mama huyo huyo vipi mkuu are you okay au?

kuhusu facts wewe ndiye uliyeleta uongo kwamba anna kilango alimfukuza mumewe toka kwenye nyumba. nikakueleza kwamba suala hilo lilienda mahakamani, sasa umerudi na kurekebisha post yako. kama mama alichomwa kwa pasi mahakama ilikuwa na uwezo wa kushughulikia suala hilo kama jinai. hapo inaonyesha kwamba unasema uongo.

- Toka umeanza unarudia yale yale niliyoyasema mimi hujasema anything new kwa mtu mwenye dataz zake kama ulivyodai mwanzoni, acha majungu mkuu Mama yuko mbali sana na hizo filimbi zako, mama alimpeleka Nyange kwenye sheria kudai talaka na kudai nyumba ili alelee watoto wanne, na mpaka leo anayo hiyo nyumba pale Kinondoni, karibu na Open University.

- Ya kuchomwa na pasi yaliishia kumalizwa nje ya sheria, lakini hilo wala sina sababu ya kushindana na wewe kwa sababu sio siri kwamba huna lolote ila ni mimi sasa ndiye ninayekupa info, acha hizo mkuu it is about time sasa ukaongelea na ya kwako mbona unayo mengi sana ya ajabu na wanaokuhusu pia, acha majungu wewe ni mtumzima sasa!

mwisho, hii damage contol unayofanya hapa inatokana na mama kilango kukosa umakini na kuanza kuzungumzia masuala yake ya zamani. mshauri ajikite zaidi kwenye present, maisha yake kama mbunge, mke wa mh.john malecela, na bibi kwasababu sasa ana wajukuu, na uchaguzi wa 2010.

- Mbona unaweweseka sana, Mama Kilango anamfanyia nani damage control? Wewe? kukosa umakini ni pale kila jina la mama likitajwa unakosa usingizi na kulala hapa kumtukana bila sababu, wakati wewe mwenyewe yamekufika shingoni, hakuna cha damage control wala anything kiongozi yoyote wa taifa ana haki ya kuzungumzia maisha yake, tumesoma maisha ya Nyerere sasa unasema na yeye alikuwa anatafuta damage control kwa kuyasema maisha yake jinsi alivyokulia kijijini na kusoma kwa shida!

- Huu unaoutoa ni ushauri wa siasa za wapi hizo mkuu? Background ya mama inatakiwa iwekwe kwenye vitabu ili kusaidia kina mama wanyonge ambao wanaonewa kila siku na wajinga wanaodhani mwanamke ni object ya kuchezea kama mpira, huu ushauri wako baki nao mwenyewe mkuu Mama kilango hahuitaji hata kidogo, ni mwanasiasa gani anayeficha background yake?

- Eti ajikite kwenye present are you serious? hivi kuna present bila ya kujua the past ilikuwaje? Mkuu acha hizi, Mama Kilango ni mbunge wa kuchaguliwa na wanachi, wamemchagua kwa kumuondoa the sitting Waziri wa jamhuri tena a powerful and rich one kama Yona, na toka ashike ubunge amewafanyia mengi sana wananchi wa jimbo lake na bado yanazidi kumimnika na wala hana mpinzani kwenye huu uchaguzi labda uwe wewe!

es!
 
Back
Top Bottom