Mama Anne Killango Malecela ndani ya TBC

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Wakuu;

Kuna kipindi kinaendelea sasa hivi TBC. Suzan Mungy anamhoji TBC.

Du! Mama kaongea mambo mengi sana ya siasa, maisha mpaka yale ambayo ni very personal ya past life yake na hata ya kwake na Mzee Malecela.

Hongera sana Mama kwa kuweka mambo yote bayana.

Bahati mbaya nilikuta kipindi kimeshaanza. Waliotangulia mnaweza kutujuza zaidi.
 
Wakuu;

Kuna kipindi kinaendelea sasa hivi TBC. Suzan Mungy anamhoji TBC.

Du! Mama kaongea mambo mengi sana ya siasa, maisha mpaka yale ambayo ni very personal ya past life yake na hata ya kwake na Mzee Malecela.

Hongera sana Mama kwa kuweka mambo yote bayana.

Bahati mbaya nilikuta kipindi kimeshaanza. Waliotangulia mnaweza kutujuza zaidi.


Niliangalia kipindi chote. Nimefurahishwa na ujasiri wake aliouonesha wakati anaamua kuachana na mume wake wa zamani. Alikuwa na miaka 30 na watoto 4 lakini alimudu kusonga mbele. Ni mfano mzuri wa kuigwa na wanawake wa TZ. Hili suala la wanawake kuonekana wanaogopa maisha pale wanapofikiria kuachana na waume zao linawasababishia waonekane wadhaifu sana. Ila breakfast ilikuwa na mushkeli kidogo, mayai na mikate viliungua. Lakini ni kipindi kizuri sana. Natumai kitarudiwa ili na wengine waone.
 
mimi nilikiona chote siku ya jmosi jana yalikuwa marudio. yule mama mjasilia mali kweli ana maduka ya maana, ni muwazi sana yaani katoa data zote jinsi alivyomnasa mzee malecela. anajua kupika japo moto ulizid sana ndio maana akaunguza.

sio akina dada wa leo ndio umemuoa hana hata wiki moja ndani anakwambia ''dear naomba tutafute bint wa kazi''!! ndani ya mwezi mzee unakuwa unaonja radha ya h.girl na si ya waifu.na wengine hawajui kupika hasa hawa wanaotoka chuo.jifunzen kwa mama kilango
 
yes this mama is very serious with issues.................let her contiue to prosper..
 
Huyu ni mama na mpiganaji. Ni transparent in any way!! Haogopi! Huyu ex hubby Nyange, pole sana. Pengine alikuwa goigoi maana kwa kawaida wachapakazi wowote wale wawe wanaume au wanawake hawataki magoigoi. Keep it up mama. I wish wanao wanne hata mmoja ataiga mfano wako, being a strong woman/man.
 
Ni Biashara gani hiyo........ukifuatilia sana wanawake wengi waliotoka.. walijiusisha sana na Biashara za Unga hapo miaka ya 80'--90'

Baadaye wakajifanya wanadini...... Mzee J'ne naye yumo ktk list hiyo... fuatilia nyendo za uchaguzi ule pale chimwaga.....
 
Seriously???
What's wrong with some women?
Of course,she had to be jasiri....she had it coming,up,down and sideways!!!


Mkuu kwani kipi cha ajabu? Usichanganye kizazi hiki cha dot com na wao. Alikuwa anaongelea miaka ya mwishoni mwa 1970; kwa hiyo siyo mambo ya leo. Alisema alikuwa na watoto 4, mkubwa akiwa na miaka 6.5 na mdogo akiwa chini ya mwaka mmoja. Kwa enzi hizo, hicho kilikuwa kitu cha kawaida sana. Na kwa ushauri wa kitaalamu ni vizuri mwanamke akazaa watoto akiwa chini ya miaka 35 kupunguza matatizo kibao yanayowapata dada zetu siku hizi.
 
Ni Biashara gani hiyo........ukifuatilia sana wanawake wengi waliotoka.. walijiusisha sana na Biashara za Unga hapo miaka ya 80'--90'

Baadaye wakajifanya wanadini...... Mzee J'ne naye yumo ktk list hiyo... fuatilia nyendo za uchaguzi ule pale chimwaga.....


Hii ni tuhuma nzito. Naomba umtendee mhusika haki na wate walio nasaba naye kwa kuweka mambo wazi. Naamini wapo watu walio na pesa safi kabisa ingawa ni wachache. Kwa hiyo Anne anaweza kuwa mmoja wao.

Na pia utatusaidia sana ukitujuvya kama mzee J'ne (naamini una maana ya Mzee J S Malecela) ana pesa nyingi sana. Mimi namwona kama mtu wa kawaida tu, anayeishi kwa pensheni na mshahara wa ubunge!
 
mie niliangalia kipindi chote.mama kilango amekuwa muwazi kabisa,kwa kila kitu- alinifurahisha sana aliposema mazoezi wanafanya hapo hapo nyumbani kuzunguka nyumba,na hii inatokana na kuona kama usumbufu kwa walinzi.
Pia jinsi alivyoendeshana na Keenja kwenye kura ya ya maoni,hapo ndipo nilipomfahamu mama huyu ni jasiri sio -mchezo.msemo wake hapa patakuwa hapatoshi nao ni motto nzuri.Hongera mama Killango tunataka muwe wengi kama wewe.
 
Mimi nilipenda alivyokuwa transparency, yani yupo openly, hajaonyesha madoido wala majigambo! Yupo sure na anachoongea,very confidently and very charming mpaka hata Suzan alikuwa anamuadmire,, by looking into her face kama ungeona ungeelewa!!
 
Keep it up again mama Anne Kilango-Malecela. Huyo member aliyesema kuwa wanawake waliibuka enzi zile pengine ni biashara ya unga inabidi apige magoti aiombe hii forum na mama na familia yake msamaha. Huyu mama kumbuka alikuwa ameajiriwa Air Tanzania (na kwingineko) na aliamua kuacha kazi akawa anafanya biashara. Biashara zake za awali zilikuwa kupika (catering), tailoring mart na alikuwa na Botique Nina Fashion pale Kinondoni TX. Enzi hizo aliweza kusafiri nje kununua nguo (marekani na uingereza) na alikuwa anauza nguo nzuri sana zikiwemo za harusi (pamoja na kukodisha). Ni kati ya wajasiriamali wa kwanza wa maduka ya nguo. Tailroring mart yake alikuwa amejenga pale nyumbani kwake Kinondoni maeneoo ya Biafra, it was excellently managed na duka la nguo na viatu lilikuwapo hapo nyumbani pia. Enzi zile ukitaka kumfurahisha mamsapu basi unamtoa suprise hadi Nina Fashion unampiga gauni la nguvu na kiatu. Vilikua ni vitu vya maana si vya China vya kileo. Mama ni mhangaikaji hadi leo duka lake lipo dodoma kwa sasa na Saloon kubwa sana. Acheni mambo yenu wale ambao mnafikiri utajiri wa njia za panya!! alipita njia ndefu sana mama. Ni baker mzuri sana wa keki!!!! Sijui kama siku hizi anafanya tena biashara ya keki (all occassions).

Keep it up mama Namfua!!!!
 
Nami pia niliangalia kipindi chote. Jana ilikuwa ni marudio, kilisharushwa kabla. Hata hivyo si vibaya kikirudiwa tena na tena maana kina mengi ya kujifunza. Hongera sana Mama Anne.
Nimejifunza mengi km:
-Kutokata tamaa. Meli ya ndoa inapoyumba, usikae chini na kulia. Simama imara, weka mwelekeo, chukua hatua, songa mbele .....mwisho wake ni mafanikio!
-It's never too late to learn.
-One can get a life partner at any age.
-Kutimiza wajibu hakuhitaji mshirika, just play your part.
-Ni muhimu kwa wanandoa kuwa marafiki.
-It's better to be alone than in ill-company.

Hayo ni machache kati ya yale niliyojifunza. Pengine tunayajua lakini tunahitaji kukumbushwa kama vile alivyotukumbusha Mama Anne, Asante sana.
 
mi nilivutiwa na mambo ya cookery ingawa pancake iliungua kidogo lakin si neno, maswali ya suzzy yalizid akaunguza....kweli wadada mjitaid kunogesha ndoano zenu kwa mapishi otherwise ma full back wataendeleza... big up graft fighter
 
Back
Top Bottom