Ndugu wana JF
Kuna taarifa ambazo sijazithibitisha kwamba, Malkia wa Uingereza anamiliki Eneo Kubwa sana Ndani ya Nchi yetu, ambapo Hata Serikali yetu haina Mamlaka ya Kuingia.
Eneo linasemekana liko Mkoa wa Iringa
Naomba mwenye taarifa kamili anijuze
Nasikia Malkia Wa Uingereza ndiye mkuu wa nchi za Canada, Jamaica , New Zealand, Barbados, Papua New Guinea n.k
Hebu click hapa
Commonwealth realm - Wikipedia, the free encyclopedia
Ndugu wana JF
Kuna taarifa ambazo sijazithibitisha kwamba, Malkia wa Uingereza anamiliki Eneo Kubwa sana Ndani ya Nchi yetu, ambapo Hata Serikali yetu haina Mamlaka ya Kuingia.
Eneo linasemekana liko Mkoa wa Iringa
Naomba mwenye taarifa kamili anijuze
Amekuwa Mmiliki wa ENEO hilo tangu enzi na enzi - hata wakati "Saint-to-Be" anataifisha mashamba kule Arusha ilo shamba/eneo halikuguswa.. Lipo Wilaya/MKOA? ya/wa? NJOMBE.
Sikumbuki kama huyo Malkia alishafika Iringa.
Ndugu wana JF
Kuna taarifa ambazo sijazithibitisha kwamba, Malkia wa Uingereza anamiliki Eneo Kubwa sana Ndani ya Nchi yetu, ambapo Hata Serikali yetu haina Mamlaka ya Kuingia.
Eneo linasemekana liko Mkoa wa Iringa
Naomba mwenye taarifa kamili anijuze
Kwanza kumbuka, Serikali haina mamlaka ya kuingia hata nyumbani kwako bila kufata kanuni na sheria.
Malkia ana ubalozi hapa Tanzania, hizo ardhi ni mali ya himaya yake na ndio maana anaweza kutundika bendera yake pale na hata Serikali ya Tanzania haina mamlaka ya kuingilia. Kwa hayo, utaona si Uingereza tu bali ni mataifa yote yenye ubalozi Tanzania yanahodhi ardhi yao na halikadhalika kwa Tanzania katika nchi zingine.
Kwa namna ninavyofahamu, hiyo ardhi unayoizungumzia ni kampuni ya miwati(Tanganyika Wattle Company) iliyopo Kibena Njombe.
Awali inavyosemekana ilikuwa ni mali ya Royal family ya Uingereza na ambapo CDC(Commonwealth Development Co-operation) walikuwa na hisa na TDFL pia nao walikuwa na hisa(sifahamu % ya hisa ilivyokuwa). Baadae(mwishoni mwa miaka ya 80 kama sijakosea), Royal family waliachia hisa zao zote kwa CDC n kufanya CDC kumiliki 85% ya hisa na TDFL Kuwa na 15% ya hisa.
Baada ya hapo sijui kilichotokea, lakini 2005, ikaonekana kama CDC ilikuwa inamiliki 100% ya hisa na hivyo ikauza hisa zake zote kwa Kampuni ya Kenya ijulikanayo kama KALDORA International, inayomilikiwa na masingasinga ambao asili yao ni Iringa na ndiyo wanamiliki Mufindi Paper Mills(zamani SPM Mgololo)
Katika kipindi chote cha mabadiliko TANWAT ilijipanua hadi Kilombero na kujishughulisha na upandaji wa Mi Tiki wakiwa na kampuni ya KVTC, so KVTC ikatenganishwa na TANWAT na ika fall kwa African Forestry ambayo ina misitu Uganda, Gabon na pia South Sudan.
Kwa hiyo nadhani Malkia alishaiacha hiyo ardhi ya Njombe na kama ana ardhi anayomiliki kwa sasa labda itakuwa hiyo ya Kilombero.
Ni mashamba ya miwati na chai huko Lupembe na Njombe kama sikosei inaendeshwa chini ya kampuni iitwayo Crown(sorry nimesahau jina)Haitakuwa ajabu hata wafalme wa Saudia na UAE wanamiliki maeneo makubwa tu hapa tz.
Hii kampuni ya wakenya walionunua Sao Hill Paper Mill ndio wamenunua pia misitu yote kule Njombe iliyokuwa mali ya CDC; maana yake ni kwamba sehemu kubwa ya mkoa wa Njome inamilikiwa na waKenya akiwamo Rais wao mstaafu Moi ambae ana hisa kwenye hiyo kampunu ya masinga singa!! Halafu wabongo mnalalamika kuwa ardhi yenu itapokwa na wageni wakati wenzenu wamekwisha wahi!!
Ndugu wana JF
Kuna taarifa ambazo sijazithibitisha kwamba, Malkia wa Uingereza anamiliki Eneo Kubwa sana Ndani ya Nchi yetu, ambapo Hata Serikali yetu haina Mamlaka ya Kuingia.
Eneo linasemekana liko Mkoa wa Iringa
Naomba mwenye taarifa kamili anijuze