Egongos, japo sijui kuhusu Iringa, ila kwa taarifa too, mali zote za serikali ya Uingereza duniani kote, kisheria zinamilikiwa na Malkia, na zimeorodheshwa kama HM properties, hivyo nyumba zote za wanabalozi wa Uingereza ni mali ya Malkia.
Kwa Tanzania, wanamiliki nyumba nyingi, prime properties maeneo ya O-bay na Sea View ambayo walijimilikisha tangu wakati wa kutupa uhuru. Pia walimiliki baadhi ya majengo ya kihistoria ya Zanzibar likiwemo jumba maarufu la Hammerton House next to nyumba ya Salmin.
Ardhi zote hizi, zina kinga ya kibalozi (diplomatic immunity), hivyo mtu akikimbilia humu na kufanikiwa kuingia ndani ya uzio, polisi wetu hawa ruhusa ya kukukamata, maana hata kutia mguu ni kosa kisheria.
Pia Malkia anamiliki baadhi ya maeneo ya public, yakiwemo makaburi ya vita kuu ya kwanza na ya pili ya dunia ambayo yametapakaa mahali kwingi hapa nchini ikiwemo Iringa. Kwa Dar es Salaam, makaburi ya vita kuu ya kwanza yako pale mjini next to Hellenic club opposite Red Cross. Na ya vita kuu ya pili yako Kijitonyama nyuma ya Millenium Park.
Ni serikali ya Uingereza inagharimia kila kitu mpaka utunzaji wa maeneo hayo, hivyo sio vibaya mkitembelea mkajionea jinsi wenzetu wanavyotunza makaburi ya mashujaa wa vita vyao ambao miongoni mwao wapon Watanzania wengi tuu, halafu na tutembelee kule Mutukula mkaone jinsi serikali yetu inavyotunza makaburi ya mashujaa wa vita vya Kagera.