Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 11,902
- 27,646
Nimesikiliza hotuba ya raisi akifungua rasmi bunge la 13 na nimeona ni kama ameanza kuinama na kujisitiri kutokana na yale yaliyotokea.
Binafsi kwa niliyoyasikia nimeona ni inawezekana watawala wameona mabavu siyo suluhisho litakalotufikisha mahali pazuri kama taifa. Nafikiri haya mambo 5 yameashiria kwamba sauti za watanzania zina nguvu:
Mambo mengine niliyoyasikia ni blah blah za kila mwanasiasa - Mikopo, uboreshaji miundombinu , kilimo, utalii, uwezeshaji madini, kuinua uchumi, tehama, mwendokasi, reli, madaraja mapya etc.
Kilichonishangaza: ni wabunge kupiga makofi mengi pale raisi aliposema anywe maji kidogo 😂😂
- Je, ili achutame kabisa kiungwana na kuepuka fedheha inabidi afanye nini?
- Kwa wenzangu mliosikiliza hotuba: je imewatia moyo au ndiyo imewaongeza hasira?
- Gen Z na wote wanaosapoti D9: kuna hoja hata moja imeongelewa ambayo inagusa malalamiko ya maandamano yaliyopita au yale yajayo?
Binafsi kwa niliyoyasikia nimeona ni inawezekana watawala wameona mabavu siyo suluhisho litakalotufikisha mahali pazuri kama taifa. Nafikiri haya mambo 5 yameashiria kwamba sauti za watanzania zina nguvu:
- Kukiri kuhusu mauaji ya siku za uchaguzi na kutoa pole
- Mchakato wa katiba mpya kurejea ndani ya siku 100 za kwanza
- Kufuta kesi za uhaini kwa vijana
- Tume ya kuchunguza mauaji ya Oktoba 29 na maridhiano (japo bado kuna maswali: watu gani wapo kwenye hiyo tume na wamepatikanaje)
- Kuanzisha wizara maalum ya vijana na ajira mpya sekta za elimu na afya