Malipo ya Wabunge ni kufuru

Malipo ya Wabunge ni kufuru

Kwa mwaka mmoja mbunge hulipwa takribani million 170, pesa hizo hulipwa kutokana na mshahara ambao ni zaidi ya milioni 11 ambayo ukizidisha mara miezi 12 unapata milioni 132.

Vilevile mbunge hulipwa posho za vikao(sitting allowance) Tsh 220,000/=na posho ya kujikimu (perdiem) Tsh 80,000/=, posho hizi hulipwa kwa kipindi ambacho mbunge anakuwa bungeni ambazo ni zaidi ya siku 130 ikiwemo zile za kamati, kwa vikao tu mbunge hukunja takribani million 39 ikiwa ni nje ya mshahara, lakini pia mbunge ni diwani pia hulipwa posho mbali mbali anapokuwa kwenye vikao vya halmashauri.
Na baada ya miaka mitano hulipwa kiinua mgongo cha zaidi ya milioni 250.
Kina Lema, Mbowe, Msigwa, Lissu, Mdee, Heche, n.k. wametumbua Sana hizi hela
 
Hao waache hata wafe hasa walimu yaani ni mazumbukuku kupitiliza wanaimba nyimbo za "kusifu na kuabudu"kwa watawala,natamani ikibidi wapunguziwe mshahara.
Hakuna watu waliombeba jpm mwaka huu Kama walimu, mbaya zaidi madaraja wengi wanalia, mishahara hawajaongezewa.Nimeamini baniani kiatu chake dawa
 
Ulichoongea hapa inaonekana hujui hata taratibu za kutoa fedha za mfuko wa jimbo ukoje. Naona unadhani hizo pesa zinaingia kwenye account ya mbunge na yeye ndio anazitoa anavyotaka.
Hujaelewa ulichosoma. Nimesema kuwa inaingia kwny A/C yake?

Haiingii kwny A/C yake na pia hatumii atakavyo ndio maana kiutaratibu ikiwa anataka kutumia, kwa mfn labda kujenga darasa la shule wilayani kwake ni sharti aiombe hiyo pesa kutoka kwny mfuko wa jimbo (source ni serikalini) na ni lazima madiwani wa kata zote ktk jimbo waridhie na wasaini

Kisheria diwani hata mmoja asiposign inaweza kuzuia pesa kutoka na kutumika.

Huo ndio utaratibu, lakini mara nyingi wabunge wao huwa wanawaahidi wananchi tu...nitafanya hivi na hivi kana kwamba pesa inatoka mfukoni mwake.
 
Hujaelewa ulichosoma. Nimesema kuwa inaingia kwny A/C yake?

Haiingii kwny A/C yake na pia hatumii atakavyo ndio maana kiutaratibu ikiwa anataka kutumia, kwa mfn labda kujenga darasa la shule wilayani kwake ni sharti aiombe hiyo pesa kutoka kwny mfuko wa jimbo (source ni serikalini) na ni lazima madiwani wa kata zote ktk jimbo waridhie na wasaini

Kisheria diwani hata mmoja asiposign inaweza kuzuia pesa kutoka na kutumika.
Hili la madiwani wote lazima wasaini ili pesa itumike Sio kweli mkuu.fuatilia vizuri
 
Nakuambia hivii, kisheria inapaswa kuwa hivyo ila huwa hawazingatii

Mbunge hapaswi kutumia pesa za mfuko wa jimbo bila kushirikisha madiwani na ni lazima awaambie ni pesa za nini, diwani wa kata husika ahakikishe pesa inafanya kile kilichokusudiwa kutimiza ahadi
 
Sio kweli, Kuna kamati maalumu, hyo kamati huundwa na mbunge mwenyewe.Hiyo kamati inapaswa kujumuisha madiwani ila Sio wote...
 
Kuna hela ya maendeleo ya Jimbo, inayopatikana katika mfuko wa jimbo, pale ndio hutoa pesa za kufanya hayo...ilimradi tu madiwani wameshirikishwa wakatia saini.
Mbunge hana mamlaka ya kutoa pesa za mfuko wa jimbo ila ni mkurugenzi.

Hivyo hayo malipo wabunge wanastahili kabisa ili watatue kero ndogondogo za wapiga kura wao.
 
It depends, ziko professional zingine kwa mfano, Pilots wa Tz, hulipwa mara 1 na nusu hadi mbili ya mbunge wa Tz.. Na Pilots wa nje ya Tz hulipwa hata mara 8 hadi 10 ya mbunge wa Tz.. Mm nadhani kiwango hicho sio kikubwa.
 
Kwa mwaka mmoja mbunge hulipwa takribani million 170, pesa hizo hulipwa kutokana na mshahara ambao ni zaidi ya milioni 11 ambayo ukizidisha mara miezi 12 unapata milioni 132.

Vilevile mbunge hulipwa posho za vikao(sitting allowance) Tsh 220,000/=na posho ya kujikimu (perdiem) Tsh 80,000/=, posho hizi hulipwa kwa kipindi ambacho mbunge anakuwa bungeni ambazo ni zaidi ya siku 130 ikiwemo zile za kamati, kwa vikao tu mbunge hukunja takribani million 39 ikiwa ni nje ya mshahara, lakini pia mbunge ni diwani pia hulipwa posho mbali mbali anapokuwa kwenye vikao vya halmashauri.
Na baada ya miaka mitano hulipwa kiinua mgongo cha zaidi ya milioni 250.
Bunge ni mgodi kama ilivyo Tanzanite
 
It depends, ziko professional zingine kwa mfano, Pilots wa Tz, hulipwa mara 1 na nusu hadi mbili ya mbunge wa Tz.. Na Pilots wa nje ya Tz hulipwa hata mara 8 hadi 10 ya mbunge wa Tz.. Mm nadhani kiwango hicho sio kikubwa.
Ni kikubwa kupita kiasi
 
Sio kweli, Kuna kamati maalumu, hyo kamati huundwa na mbunge mwenyewe.Hiyo kamati inapaswa kujumuisha madiwani ila Sio wote...
Mbunge hateuwi kamati, kamati huteliwa na DED, Afisa mipango ni katibu wa kamati, madiwani wa 2 na watendaji 2
 
Kati ya malipo ya hovyo kufanywa kwa wabunge ni hiyo sitting allowance. Kazi mojawapo ya ubunge ni kuhudhuria vikao vya bunge na kuchangia mada kwenye vikao hivyo, sasa iwapo kukamilisha kazi yake analipwa ziada ni upuuzi sana; ni sawa na kumlipa mwalimu teaching allowance kila anapoingia darasani kufundisha, au kumlipa dereva driving allowance kila anaponedesha gari, malipo hayo yakiwa nje ya mshahara wake..
Hiyo ni gharama ya kulipia tako! Tanzania kuna malipo ya kipumbavu! Halafu tena eti kunakuwa na perdiem ya elfu 80. Kwa nini fedha yote hiyo isiunganishwe na kupewa jina moja tu? Halafu yalivyo na wivu sasa kwa wengine kupata hela za posho!
 
It depends, ziko professional zingine kwa mfano, Pilots wa Tz, hulipwa mara 1 na nusu hadi mbili ya mbunge wa Tz.. Na Pilots wa nje ya Tz hulipwa hata mara 8 hadi 10 ya mbunge wa Tz.. Mm nadhani kiwango hicho sio kikubwa.
Weka figure tuone
 
Back
Top Bottom