Malipo ya Wabunge ni kufuru

Malipo ya Wabunge ni kufuru

Halafu utasikia,Mara ho wafanyakazi wasiongezewe mshahara,tuna watu waajabu Sana tz , ubifsi,wizi ambao wengi utawakuta wakidajali kwamba ni fulsa na ukiwagusa wanachachamaa Kama kunguni.

Tanzania ina shida Sana kila mmoja huku chini hutafuta fulsa za wizi, na dhulma.
 
Halafu ndiyo tunasema Tanzania kuna usawa?

Hakuna!

Nenda kwa watumishi wa kawaida ambaye ana - toil mchana na usiku ili hawa wanasiasa wawatumie kama ngazi za kujisifia na kujiinua uone wanalipwa kiasi gani kwa mwezi.

Mwalimu mwenye cheti cha daraja la IIIA mshahara wake anapoanza kazi ni Tshs 400,000 na senti kidogo kabla ya makato (Gross Salary).

Mwalimu mwenye Stashahada (Diploma) akianza kazi Leo, mshahara wake kwa mwezi ni Tshs 516,000 kabla ya makato (yaani Gross Salary).

Mwalimu mwenye Shahada (First degree) akianza kazi leo, mshahara wake kwa mwezi kabla ya makato (Gross Net pay) ni Tshs. 716,000.

HALAFU:
Eti Tanzania hii hii kuna watu waitwao wabunge wanalipwa mshahara wa Tshs. 11,000,000 kwa mwezi; Posho ya kukaa (sitting allowance Tshs. 70,000 kila siku; posho ya mafuta, mkopo usio na riba wa karibu Tshs. 100,000,000 eti anunue gari ya kutembelea nk nk...

Katika mazungira haya utasemaje kuna usawa katika nchi hii?

No way. Lazima tulikatae hili na kulipinga kabisa. Lazima tugawane keki ya taifa kwa usawa. Haiwezekani wengine tuwe watwana, watumwa na manamba ndani ya nchi yetu menyewe.

Are these the fruits of Uhuru we got on 9th December, 1961?
 
Kuna hela ya maendeleo ya Jimbo, inayopatikana katika mfuko wa jimbo, pale ndio hutoa pesa za kufanya hayo...ilimradi tu madiwani wameshirikishwa wakatia saini.

Ulichoongea hapa inaonekana hujui hata taratibu za kutoa fedha za mfuko wa jimbo ukoje. Naona unadhani hizo pesa zinaingia kwenye account ya mbunge na yeye ndio anazitoa anavyotaka.
 
Siasa ni eneo ambalo watu wanavuna mamilioni bila jasho, huko hakuna kukaguliwa ni kuvuta marupurupu tu.Katika eneo ambalo watu huibia nchi kisheria ni siasa.Fikiria mtu baada ya miaka 5 analipwa milioni 200+ Kama kiunua mgongo.Je kazi gani ya umma utalipwa pesa hyo kwa utumishi wa miaka mitano?
 
Kwa mwaka mmoja mbunge hulipwa takribani million 170, pesa hizo hulipwa kutokana na mshahara ambao ni zaidi ya milioni 11 ambayo ukizidisha mara miezi 12 unapata milioni 132.

Vilevile mbunge hulipwa posho za vikao(sitting allowance) Tsh 220,000/=na posho ya kujikimu (perdiem) Tsh 80,000/=, posho hizi hulipwa kwa kipindi ambacho mbunge anakuwa bungeni ambazo ni zaidi ya siku 130 ikiwemo zile za kamati, kwa vikao tu mbunge hukunja takribani million 39 ikiwa ni nje ya mshahara, lakini pia mbunge ni diwani pia hulipwa posho mbali mbali anapokuwa kwenye vikao vya halmashauri.
Na baada ya miaka mitano hulipwa kiinua mgongo cha zaidi ya milioni 250.
Kati ya malipo ya hovyo kufanywa kwa wabunge ni hiyo sitting allowance. Kazi mojawapo ya ubunge ni kuhudhuria vikao vya bunge na kuchangia mada kwenye vikao hivyo, sasa iwapo kukamilisha kazi yake analipwa ziada ni upuuzi sana; ni sawa na kumlipa mwalimu teaching allowance kila anapoingia darasani kufundisha, au kumlipa dereva driving allowance kila anaponedesha gari, malipo hayo yakiwa nje ya mshahara wake..
 
Back
Top Bottom