Malipo ya Wabunge ni kufuru

Malipo ya Wabunge ni kufuru

Hawa wabunge wanaweza kuwa wanapata hii pesa yote ila kwa hesabu zangu ni pesa ndogo sana ukilinganisha na natumizi yao.

1. Matumizi makubwa yapo kwenye campain. Budget huongezeka kutokana na nguvu ya upinzani jimboni.

2. Gharama zake za kimaisha kama mbunge.
Kumbuka mbuge hawezi ingia hotel za chakula cha elf 2000 kama sisi makapuku. Hawezi vaa nguo za mitumba.
Kwa ufupi kunacost za kimaisha ambazo hukutana nazo kumaintain status yake kama mbunge.

3. Mbunge anacost nyingine za ulinzi, usafiri etc.

Kwa ujumla hii ni pesa ndogo ni sawa na mshagara wa mwalimu kule USA.
 
Sina uhakika kama Mbunge lets wa nchi zilizoendelea kama Marekani ama Uingeleza analipwa Pound 57,000 ama $74,000 kwa mwaka, hakuna. Tujitafakari sana hapa kwani nchi yetu bado ni fukara tena mbaya zaidi wa kifra zinazopelekea umaskini mkubwa - juzi tu tulikuwa tunachangishana madawati wakati wenzetu suala la madawati waliachana nalo karne ya 17 afu tunamlipa mtunga sheria wetu 170m.

OK chukulia hawa wabunge tunao 380 x 170m = 6,460,000,000,000. Hii ni kwa mwaka mmoja, sasa hebu piga hesabu kwa miaka 5 inakuwa 32 Trilion.
 
Kwa mwaka mmoja mbunge hulipwa takribani million 170, pesa hizo hulipwa kutokana na mshahara ambao ni zaidi ya milioni 11 ambayo ukizidisha mara miezi 12 unapata milioni 132.

Vilevile mbunge hulipwa posho za vikao (sitting allowance) Tsh 220,000/= na posho ya kujikimu (perdiem) Tsh 80,000/=, posho hizi hulipwa kwa kipindi ambacho mbunge anakuwa bungeni ambazo ni zaidi ya siku 130 ikiwemo zile za kamati, kwa vikao tu mbunge hukunja takribani million 39 ikiwa ni nje ya mshahara, lakini pia mbunge ni diwani pia hulipwa posho mbali mbali anapokuwa kwenye vikao vya halmashauri.

Na baada ya miaka mitano hulipwa kiinua mgongo cha zaidi ya milioni 250.
Wacha walipwe umewahi sikia MTU anazikwa na pesa au thamani alizo pata duniani wacha wale maisha hakuna kipya hapo.
 
Ndio gharama anazoingia mbunge kwa process yote?😳

Nilimsoma Hayati Mkapa kwenye kitabu chake akisikitishwa na gharama za uchaguzi wanazoingia wanaosaka madaraka, nikahisi kuna tatizo ila sio kwa gharama hizi!
ZINAFIKA MKUU TENA NA KUZIDI
 
ZINAFIKA MKUU TENA NA KUZIDI
Anagharamia nini labda? Maana napiga picha uwekezaji wa milioni 300+ kwenye biashara, hata kama ni kwa awamu, unapata biashara ya/za maana kabisa.
 
Mkuu biashara ipi ya maana? muulize aliyejenga Gurdoto Hotel
 
Hahahaa..ile ni mismanagement tu

Kuna wanaofanya biashara ya kusafirisha nyama kwenda Uarabuni, kwa mfano. Ukiwa na mtaji wa milioni hamsini na ukiweza kutengeneza network nzuri, yaani unatengeneza hela vizuri tu ndani ya muda mfupi. Ila nakuelewa mkuu, "biashara ya Ubunge" naona ina risk ndogo zaidi.

Kinachonishangaza hizo hela anazitumia wapi na kivipi? Kwa mfano, ni kulipia matangazo, "kulipia" kura ya wajumbe, kulipa wasaidizi, nk. inafika milioni 100 hata? Au gharama kubwa anaingia wapi?
 
Hakuna watu waliombeba jpm mwaka huu Kama walimu, mbaya zaidi madaraja wengi wanalia, mishahara hawajaongezewa.Nimeamini baniani kiatu chake dawa
Walimu wamembebaje Magu wakati kwenye kampeni walikuwa wanalazimishwa kwenda na kusign mahudhulio
 
Vikao tu kwa wiki si chini ya milioni 400 kwa Kazi gani wafanyazo Hawa Hali majimboni urudi kuomba kura tu.
 
Kama tumeamua kubana matumizi kwa kutowaongeza watumishi mishahara why tupoteze nyingi kuwalipa wabunge.
Ubunge iwe ni Kazi ya wito Ili tuweze pata wabunge makini
 
Wawekee na matumizi - ukiwa mbunge ghfla unakuwa benk - mwenye shida ya ada jimboni unamsaidia, mwenye shida ya matibabu unaangaliwa, viongozi wa chama wakiwa na safari unapigiwa simu, nk
 
Hebu nenda straight kwenye maana yako. Ukimaanisha kuwa???
 
Kwa mwaka mmoja mbunge hulipwa takribani million 170, pesa hizo hulipwa kutokana na mshahara ambao ni zaidi ya milioni 11 ambayo ukizidisha mara miezi 12 unapata milioni 132.

Vilevile mbunge hulipwa posho za vikao (sitting allowance) Tsh 220,000/= na posho ya kujikimu (perdiem) Tsh 80,000/=, posho hizi hulipwa kwa kipindi ambacho mbunge anakuwa bungeni ambazo ni zaidi ya siku 130 ikiwemo zile za kamati, kwa vikao tu mbunge hukunja takribani million 39 ikiwa ni nje ya mshahara, lakini pia mbunge ni diwani pia hulipwa posho mbali mbali anapokuwa kwenye vikao vya halmashauri.

Na baada ya miaka mitano hulipwa kiinua mgongo cha zaidi ya milioni 250.

Kuna umuhimu wa kutafiti, maisha wabunge kama wanaishi dunia ya kwanza au wanaishi dunia ambayo waTanzania wengine wanaishi. Kwa maana kuna tofauti kubwa sana ya kipato kati ya mTanzania mbunge na asiye mbunge.

Nini msingi (base) wa kuwapa kipato cha hali ya juu kiasi hiki?
 
Kwa mwaka mmoja mbunge hulipwa takribani million 170, pesa hizo hulipwa kutokana na mshahara ambao ni zaidi ya milioni 11 ambayo ukizidisha mara miezi 12 unapata milioni 132.

Vilevile mbunge hulipwa posho za vikao (sitting allowance) Tsh 220,000/= na posho ya kujikimu (perdiem) Tsh 80,000/=, posho hizi hulipwa kwa kipindi ambacho mbunge anakuwa bungeni ambazo ni zaidi ya siku 130 ikiwemo zile za kamati, kwa vikao tu mbunge hukunja takribani million 39 ikiwa ni nje ya mshahara, lakini pia mbunge ni diwani pia hulipwa posho mbali mbali anapokuwa kwenye vikao vya halmashauri.

Na baada ya miaka mitano hulipwa kiinua mgongo cha zaidi ya milioni 250.
Mkuu hayo malipo ni kodi zetu kwaiyo useseme hulipwa sema tunawalipa
 
Hawa wabunge wanaweza kuwa wanapata hii pesa yote ila kwa hesabu zangu ni pesa ndogo sana ukilinganisha na natumizi yao.

1. Matumizi makubwa yapo kwenye campain. Budget huongezeka kutokana na nguvu ya upinzani jimboni.

2. Gharama zake za kimaisha kama mbunge.
Kumbuka mbuge hawezi ingia hotel za chakula cha elf 2000 kama sisi makapuku. Hawezi vaa nguo za mitumba.
Kwa ufupi kunacost za kimaisha ambazo hukutana nazo kumaintain status yake kama mbunge.

3. Mbunge anacost nyingine za ulinzi, usafiri etc.

Kwa ujumla hii ni pesa ndogo ni sawa na mshagara wa mwalimu kule USA.
Upo sahihi kabisa mkuu hapo bado hujapigiwa simu na wapiga kura wako uwatatulie kero ndogo ndogo za dharura ambazo lazima muda mwingine utoe pesa yako ya mfukoni.

Hayo malipo ni sahihi kabisa wao kulipwa.
 
Back
Top Bottom