Mimi nimetembea mikoa ming ya tz na nimeongea na wazee wakongwe wa baadhi ya vijiji na kugundua siri nyingi sana kuhusu alama mbalimbali kwenye baadhi ya milima na mawe ktk maeneo mbali mbali. Kuna watu wanasafiri mara kwa mara hiv mmewahi kujiuliza nani anachora alama fulan fulan kwenye baadh ya milima au mawe kule porini na hasa alama ya mistar kama ya pundamilia ya rangi nyeupe au alama za fuvu na mifupa miwili(Danger mark)? Mi najua hakuna aliyewahi kujiuliza au kufuatilia juu ya alama hizo.
Na kwa wale wana jf ambao hawana tabia ya kufanya utafiti halafu wanakurupuka kupinga kitu pasipo kuwa na uhakika waache. Watz wengi hatupati maendeleo makubwa kwa kujifanya wajuaji wa kila kitu kumbe hamna kitu. Kwa taarifa tu ni kwamba wapo matajiri wengi wanaotajirika kupitia mali hizo ila hawasemi na hawawezi kuwaambia watz hata siku moja maana wakiwaamsha hawataendelea kunufaika kama sasa.
Serikali inajua kuwa mali zipo isipokuwa haiwezi kuzitoa yenyewe kwa sababu ya mali hizo kutopatikana ktk eneo moja tu.
Ni hii mambo zipo, nimefanya kautafiti kangu nikiwa mwanza, nilifuata alama kwa maelekezo nilopewa nikafika mahali kuna handaki, kiukweli niliogopa kuingia, kwanza nlikua pekeangu, so safar iliishia hapo, nia yangu ilikua kuthibitisha story nilizopewa, hivyo nina hakika kama nitapata muda nitaendelea na utafiti wangu, na ni kweli mashart yake wala si umwagaj damu, ni marahisi tu, sema inatakiwa kuwa na ujasir, kuna mitego, na ni sehemu hatar sana.
Hiyo ni picha kati ya maeneo nilopita.
Hiyo chokaa ni moja kati ya alama zinazowekwa, zipo alama tofauti tofauti kulingana na aina ya mzigo ulotunzwa, alama nyingine ni direction ya sehem maalumu ulipo mzigo, au alama za njia.
Kuna alama za miti fulani ivi ambayo inaishi muda mrefu na katika maeneo ya mawe mawe, pia kuna alama ya mchanga, yani kuna mchanga umemwagwa uko tofauti na mchanga halisi wa eneo hilo, na unaukuta mwanzo wa mawe, ama ukiona alama fulan ukaifata ktk pango unakuta umemwagwa juu.