de Gunner
JF-Expert Member
- Nov 2, 2021
- 10,911
- 21,638
Kuna kitu nime witness Leo kwenye daladala, Kuna mama sjui bibi! Alikua na mtoto mdogo, very innocent.. inaonekana kabisa hakua mama yake, yule mtoto hakua comfortable, alikua anaumwa jino (nilikuja kugundua baadae!)
So kwanza dogo, dogo kawekwa pembeni, siti ya kukaa watu wawili yule mama kambanisha dogo kwenye dirisha! Sio case kwangu maana wote waliweza kucompesate siti Yao!!
Ila angeweza kumbeba Bado ni mdogo. kingine nilichoanza kunotice ni kama yule mlezi(bibi yake) hakua na connection yoyote na mtoto, dogo kakaa kinyonge, kaegemea dirisha..
Kuna scenario ikatokea kwenye gari, mtu kaibiwa simu, kumbe inaonekana, yule mdada(abiria mwingine aliesimama) alichomolewa kwenye mkoba wake katika purukishani za kuwahi siti (si unajua joini hapa dar purukishani kama zote) plus foleni so usipopata siti utasota..
Kwanza nilidhani yule, mama(bibi ake mtoto Kwa kudadisi) hakua mwongeaji, ila baada ya tukio, nikajua kabisa ni mtu flani mwongeaji na anapenda mabishano which clearly shows on how anavyo mtreat mtoto, kimabavu.
Tumekaa watu wameongea, majibizano ya hapa na pale, nimechill na observe kama tu, Mimi siomuongeaji sana... Na sometimes hata presence yangu unaweza isiwe noticeable, sometimes, Baada ya majibizano mjadala ukaisha alieibiwa akakubaliana na hali kuwa kazidiwa ujanja. Ukimya ukatwala tena.
Tumetulia kwenye foleni, mara dogo akamgeukia akiwa na nyuso ya huzuni yule, mama akamjunjia sura, "Nini tena, embu tulia" dogo Kwa unyonge akarudi kuegemea dirisha.
Ila inaonekana alikuwa na maumivu ya jino maana mkono wake wa kushoto ulikua una papasa shavu upande wa magego, hakuwa comfortable kabisa dogo,
Baada ya muda nikaskia dogo anamwambia yule mama Aunty… jino langu linauma,” alisema kwa sauti ndogo, lakini yenye ujasiri wa kujieleza.
Yule mwanamke hakumtazama hata. Alijibu kwa ukali, “Acha kusema hivyo. Unataka nifanye nini? Kuongea hakusaidii kitu.”
Kisha kulikuwa na ukimya.
Lakini si ule ukimya wa kawaida… ulikuwa mzito. Ulikuwa na maana.
Na mimi nikabaki hapo, nikitazama. Nikihisi kuna kitu hakiko sawa ndani yangu. Lakini sikusema chochote.
Hapo ndo ikaja coleration ya kile nilicho jifunza ukubwani kuwa maumivu na stress za ukubwani huanza kama utani vile, mtoto anakuwa unsafe Kwa kitu kidogo kama hicho, then kina kuwa strong baadae, anaanza kuona watu wote ni kama yule mlezi, she couldn't notice the difference, hajui kama yule mama nae anarespond hivyo kutokana na maumivu alopitia udogoni au magumu anayopitia so it becomes an endless cycle.
Alijifunza kuwa maumivu yake hayana umuhimu.
Alijifunza kuwa kusema kunaleta kukataliwa.
Alijifunza kuwa ni bora anyamaze.
Na hapo ndipo mambo huanza kubadilika.
Mara nyingine, hatasema tena. Ataumia kimya kimya. Ataanza kujiuliza kama kweli anachohisi ni halali. Ila nani alaumiwe?
Naamini hakuna mtu yuko perfect, Kila mtu anpitia anachopitia kwasababu. Kuna vitu watu tunajifunza tukiwa wazee, ila maumivu sio mpk tuyapeleke Kwa viumbe wasio na hatia, ambao wanna maono makubwa maishani ila wanalelewa katika misingi ya kujiona hawawezi kitu.
Ile scenario imeniuma sana, huenda ningemtetea dogo, ningeonekana nafuatilia mambo ya watu, na kingezua mjadala, yule dogo nilimpa elf 5 nikaona katabasamu, na hio ndo ilikua furaha yangu. Huenda atapitia magumu mengi mbeleni which is horrible, ila hiki kitu kidogo tu kimeniuma sana..
Kuna vitu nimepitia hii scenario ndogo tu ila ikumbusha, ila Kuna vitu wazazi wanafanya bila kujua vina affect watoto, wazazi wanaweza wakawa na Kila kitu, ila tu kutowajali wana Kuna haribu future nzima, wana kuja kuwa watu wazima wanaviptisha Kwa watoto wao pia.
Sio hasira, ni maumivu. Nimeishi kichukia watu, hasa wa karibu na imesababisha mengi hasa kwangu sio kwao, nikataka kujua Nini chanzo, chanzo kikarudi kwenye malezi, utotoni, so sijui kama hata Kuna mtu kanielewa?, ni ngumu imenichukua muda sana, naanza kuona mwanga ila Bado na Mimi na madhaifu yangu pia.
Huenda yule mtoto alitibiwa sawa, ila tayari Kuna unyonge flani kashajifunza kuhusu self expression(kujieleza).
Akiendelea kupata treatment ya namna hii, itamharibu sana, atakuja kuwa either mtu mkorofi au mpole kupindukia na kuacha wengine wamkanyage. Ndo maana narudi kwenye malezi, hii scenario ni ya kawaida sana kiafrika, ila ndo mwanzo na chimbuko la matatizo mwengine.