Malezi: Salamu kwa Serikali na Mashirika Binafsi

Hemedy Jr Junior

JF-Expert Member
Feb 17, 2023
908
1,064
Mambo yanabadilika kila kukicha kuhusu malezi, mpaka malezi kubadilika kuna sababu. Kipindi cha nyuma malezi yalikuwa bora tena sana japo watoto watukutu hawakukosekana, lakini ukichunguza vizuri hao watoto watukutu walitokea familia za aina gani?

Utagundua familia hizo ni za walevi au baba alikimbia familia akabaki mama au mama alikimbia akabaki baba, na baba nae akawa mlevi, watoto wakakua kwa style hiyo ya kujilea. Katika maisha ya kujilea kuna mambo mengi sana hasa pale unapokumbana na changamoto.

Mtoto kuvumilia changamoto inakuwa ngumu tofauti na mtu mzima, pia mwanamke nae sio kiumbe cha kuvumilia changamoto ndio maana familia nyingi za zamani kidogo kama mwanaume alikimbia familia utakuta mwanamke ni danga la kijiji kama wa mjini danga la mjini. Sasa hapo unategemea mtoto atakuwa wa aina gani kama mama yake ni mdangaji?

Hizi familia zilizalisha watoto wengi wahuni, majambazi, waliojaliwa na kubarikiwa na kuyavumilia kwasasa wanapambana sana maana walikopitia hawatamani watoto wao au kizazi chao kije kurudi kule. Watoto ni watoto tu hakuna mtoto anayeshindikana kwa mzazi.

Utasikia hili toto ni jeuri, mtoto anakuwa jeuri kwasababu we ndo ulimwandaa kuwa jeuri kwa kipindi fulani. Mtoto anatukana wakubwa au watoto wenzie umkanyi unajichekesha we unafikiria nini au unatengeneza motto wa aina gani?

Mimi sishangai hata kwa viongozi tulionao kwasasa maana wote wametoka kwenye jamii, ona wanapopata madaraka wanajipa ukuu, wanasahau aliyetuumba, wanajisahau. Malezi ni kitu muhimu sana kwa watoto wetu.

Sisi tulipigwa, kwanini watoto wetu tusiwapige? Mwanao huwezi kumuadhibu kama mnyama, watu ambao huwa wanatoa vipigo vya ajabu ni kutokana na watu wenye (hasira kali kama asili ya familia au ulevi).

HITIMISHO

Mabadiliko yanayoonekana kwenye malezi ni kutokana na jamii nyingi kujikita kwenye utafutaji wa pesa/maisha na kusahau kuwa kuna viumbe vinahitaji kupata elimu ya maisha.

Kingine, wanawake wengi nao wako bize kutafuta pesa, hiki kitu kimekuja kubadili mfumo mzima wa malezi kwasababu gani? Mwanamke (mama) ndio mtu wa karibu na mtoto, ila kwasasa hivi mtu wa karibu na mtoto ni dada wa kazi (nyumbani).

Mwanamke kufanya kazi masaa sawa na mwanaume hili nalo ni tatizo, tushakuwa na kizazi ambacho mama na mtoto wanapashana habari za mabwana wapya.

PENDEKEZO KWA WAAJIRI/SERIKALINI AU WATU BINAFSI

Mwanamke kama kaolewa asifanye kazi muda sawa na mwanaume, ili apate muda wa kuongea na mtoto na kumfunza kitu. Ila baba anarudi saa moja jioni mama saa moja jioni. dooh, Taifa linaenda hatarini.

Malezi ni fursa jwa sasa Tanzania, chochote unaweza changia.
By @Hemedyjrjunior
 
Back
Top Bottom