Ifike mahala Watu waelewe kuwa Jukumu la Malezi sio la Serikali

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
IFIKE MAHALI WATU WAELEWA KUWA JUKUMU LA MALEZI SIO LA SERIKALI

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Ukishaishi kwenye taifa ambalo halina Dini ila Watu wake wanadini, hiyo itoshe kukueleza kuwa jukumu la Malezi ni jukumu la wananchi wenyewe na sio jukumu la serikali.

Ni kosa la kiufundi kufikiri kuwa Malezi ya watoto wako ati yasimamiwe na serikali. Kosa kubwa.

Serikali kazi yake ni kutawala. Na unapozungumzia kutawala unazungumzia kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa(maslahi) ya Watawala na kidogo maslahi ya wanaotawaliwa.

Mtoto wako kuwa Mwizi au mhuni serikali haipati hasara popote pale. Zaidi itatumia uhuni wake kujinufaisha kwa namna moja ama nyingine.

Kupitia uhuni wa mtoto wako serikali italipa Mahakimu, majaji, polisi, na askari magereza na huko ndiko kujinufaisha.

Serikali inajua kabisa duniani sio mbinguni. Inajua kabisa! Inajua haiwezi kustawi kwa uadilifu pekee bali hata uhuni na watu wasio na maadili ni muhimu kwa serikali.

Ni jukumu lako kuhakikisha unawalea watoto wako katika maadili mema. Na sio jukumu la mtu mwingine kama serikali.

Kitendo cha kumpa mtu mwingine hasa serikali jukumu la kukulelea mtoto wako hapo tayari lazima ulipie. Lazima serikali inufaike. Tena ikiwezekana kwa maumivu makali na Presha na mateso.

Yaani uzae watoto wako alafu unataka mwingine akulelee. Uliona wapi hiyo.

Usipolea watoto wako kuna waja watawatumikisha kiharamu. Watageuzwa punda wabebe Madawa ya kulevya wawazalishie wengine faida alafu mwisho wa siku wakikamatwa bado watazalisha faida kwa serikali huko magereza kwa sababu serikali itakuwa imejipatia Cheap Labour.

Usipolea watoto wako vizuri watageuzwa mashoga na kupumuliwa. Na hakuna yeyote atakayepata hasara zaidi yako. Achana na zile kauli za kisiasa kuwa sijui taifa limepata hasara, hizo ni porojo. Taifa halipatagi hasara kwa mambo ya uhalifu bali linanufaika zaidi na kirahisi.

Umeshindwa kumlea mtoto wako, amekimbia shule kizembe. Kinachofuata sio hasara ya taifa bali faida kubwa kwa kumtumia mtoto wako kama kibarua kwa kazi ngumu na kubwa kwa malipo kidunchu. Hiyo inaitwa nguvu kazi. Ukosefu wa maadili kwa upande mwingine unazalisha nguvu kazi ambayo ni gharama nafuu kabisa.

Hiyo nguvu kazi ndio hiyohiyo itatumika kwenye maandamano ya Wanasiasa kwa maslahi ya Watawala. Hiyo nguvu kazi ndio itatumika kwa Manabii na masheikhe wa mchongo.

Haitakuja kutokea Watawala wakapambana kwa dhati yote kutetea maadili ya mtoto wako wakati wanajua kushindwa kwa malezi yako kwa watoto kwao ni faida kubwa kuliko kufanikiwa.

Serikali itakachoingilia kati ni kuzidi kwa matukio ya kihalifu yaani yasipitilize lakini kuyatokomeza kabisa ni kuangusha taifa.

Nawatakia jumapili njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Wadangaji, mabameidi na mahausi gelo ni zao la malezi mabaya ambavyo hubatuzwa jina la umasikini.

Wadangaji waliolelewa vizuri huwezi kumwagia ndani bila mamilioni au umuhonge cheo au mjengo.

Hawa wa 10,000 kulala wengi wameanza umalaya wakiwa std V
 
Screenshot_20231117-053116.png
 
Mtibeli siyo kuwa serikali ikiwa na sheria makini ndiyo na watoto wanakuwa na malezi mazuri? Tabia ya mtoto inaanzia tangu anspozaliwa na inategemea sana vilevile na ndoa ya wazazi. Single mothers/fathers, sheria za ndoa. Unategemeaje ndoa za wake wengi kuwa na watoto wenye malezi mema?

Halafu haki ya mtoto, sioni kama kuna sheria ambayo inamlinda mtoto kwenye elimu na maamuzi ya maisha yake.

Halafu vipato. Unemployment kwa Tanzania ni zaidi ya 60%, society kama hiyo unategemea itazalisha watu wa aina gani? Kama hakuna kipato hapo ndiyo watu huanza tabia za ajabu. Kwa sababu lazima waishi

Mila na desturi, - kuna watu wavivu, kuna makabila vitu ambavyo ni taboo wengine ni hobby. Kuna watu sex ni hobby. Kuibia serikali ni ushujaa, kuwa na watoto wengi au wake wengi ni sifa.

Serikali inahusika moja kwa moja na kufuatilia na watu wake sheria ziimalishwe + motivation.

Mzazi ana share yake 30%
 
Back
Top Bottom