Malengo Yako Ya 2026 ni yapi?

Funga ndoa kwanza, ndipo uzae
 
Mtoto uzoefu utaupata kwa kumlea, kaa na wazazi waliowahi kulea wanaooenda malezi bora watakusaidia. Jiunge vikundi vya wazazi wapya wenye changamoto sawa.

Kimataifa zaidi tafuta kitabu kinaitwa "What To Expect When You Are Expecting" kinaongelea mambo mengi kuhusu mama watarajiwa.

Kupush utapush tu hakuna jinsi, ukishindwa watakuchana Caesarean lakini hiyo mpaka ushindwe kwanza.

Ukipata mtoto ushakubali kumfanya mtoto ndiyo anakuwa kipaumbele utulivu wako unategemea bosi (mtoto) anatakaje. Akilia inabidi na wewe uwe kama mtoto uanze kuongea lugha yake unamchekesha "achigichigichigichiii... achigichigichigichiii.." mpaka anaacha kulia anacheka, mpaka ananyonya, mpaka analala.

Mimi mwaka uliopita nimewashika mkono vijana watano walio katika hatua ya masomo ya chuo, changamoto ni nyingi sana lakini tunakabiliana nazo mpaka wamalize.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…