China yaunga mkono mchakato wa maendeleo ya viwanda barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG41N1327603766.jpg

Tarehe 20 Novemba ni Siku ya Maendeleo ya Viwanda Barani Afrika. Ikiwa ni sehemu muhimu ya ushirikiano wa kirafiki kati yake na Afrika, China imewajibika kuzisaidia nchi za Afrika kuendeleza viwanda, na kuchukua hatua nyingi zinazolingana na hali halisi ya nchi hizo.

Baada ya kuingia katika karne ya 21, Afrika imepanga upya mkakati wake wa kuendeleza viwanda, na kuanzisha Ushirikiano Mpya wa Maendeleo ya Afrika (NEPAD), Mpango wa Kuharakisha Maendeleo ya Viwanda Barani Afrika, na Agenda ya Mwaka 2063. Hata hivyo, nchi za Afrika bado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kuendeleza viwanda, ikiwemo miundombinu duni, mnyororo usiokamilika wa viwanda, na ukosefu wa uwiano wa uzalishaji na mahitaji.

Wakati ikizisaidia nchi za Afrika kuendeleza viwanda, tofauti na nchi za Magharibi ambazo zinaweka masharti ya kisiasa na kiuchumi yanayolingana na vipimo vyao vya ndani, China imechukua hatua mbalimbali kufuatia hali halisi ya nchi za Afrika.

Hatua ya kwanza ni kujenga maeneo maalumu ya kiviwanda ili kuzisaidia nchi za Afrika kujenga mnyororo wa viwanda. Hadi sasa China imejenga maeneo makubwa 25 za kiviwanda barani Afrika. Maeneo hayo yanasaidia kuanzisha ushirikiano wa moja kwa moja kati ya makampuni husika, na yanatoa huduma za kimsingi kwa uzalishaji wa viwanda. Kwa mfano, China imejenga Eneo la Ushirikiano wa Kiuchumi na Biashara kati ya China na Zambia la Chambishi, ili kuchakata kwa kina madini yanayochimbwa nchini humo.

Hatua ya pili ni kuunganisha ujenzi wa miundombinu na uwekezaji wa viwanda. Kwa mfano wa reli inayounganisha mji wa Addis Ababa na Djibouti, ambapo China ilihimiza makampuni yake kuunganisha ujenzi wa reli na ujenzi wa eneo la kiviwanda, na kupanga viwanda kando ya reli hiyo ili kuitumia kikamilifu. China pia ilishiriki kwenye ujenzi wa bandari mpya nchini Djibouti, ili kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa bandari kufuatia ongezeko la kasi la uwezo wa kusafirisha mizigo wa reli hiyo mpya.

Tatu, uwekezaji wa viwanda wa China barani Afrika unalenga kuzalisha bidhaa zinazofaa kwa soko la kienyeji. Kwa kuwa soko la Afrika si kubwa na liko mbali, linapuuzwa na makampuni ya nchi zilizoendelea. Licha ya kuwa na bei ghali, bidhaa nyingi zinazouzwa kwa Afrika hazilingani na mahitaji maalum ya Waafrika. Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na uhusiano wa karibu wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika, makampuni mengi ya China yameanzisha shughuli zao za uzalishaji barani Afrika, na kuzingatia soko la ndani la nchi za Kiafrika. Bidhaa zinazozalishwa na makampuni hayo barani Afrika si kama tu zimepunguza gharama za usafirishaji, bali pia zinalingana zaidi na mahitaji ya wateja wa Afrika.
 
Back
Top Bottom