Malecela: Magufuli hatarini

Malecela: Magufuli hatarini

siasa buana, mzee anaiomba serikali imuongezee ulinzi, kwani hiyo serikali inaongozwa na nani?
 
Labda anamwombea kazi ya ubaunsa Le Mutuz.....you never know



Le Mutuz hajitambui japo he's almost 60 years old. Yeye aje apewe ubaunsa kwa Magufuli badala ya kumlinda Mh. rais yeye atakuwa bize kujipiga "Selfie Ekoti Te," na wasichana uchwara anaowapigia promo hapa mjini kwa mshahara wa hugs.
 
Magufuli aongezewe ulinzi wa nini wakati ni kipenzi cha watz,wamuue waone mimi nitaanzisha kundi la ISIS kwaajili ya kuwaua mafisadi wote hata kama haujashiliki kuua,na nitaanza na mkuu wao yule mwenye nywele nyeupe alafu namaliza na madereva wa magari yanayobeba makontena
 
Na ole wao wathubutu kumdhuru raisi wetu Magufuli japo kwa lolote tu,
Nadhani ndio watajua kwamba Watanzania walikua wanampenda na kumhitaji au lah.

Yani patachimbikaje hapa? hakiyanani!!!!! watatubeba eti wamguse huyu kipenzi chetu weweeeeee..... tutadedishana aiseeee!!!! Yani hata mbu au nzi hatitakitaki amguse. God bless our president JPM
 

Attachments

  • 1449676996052.jpg
    1449676996052.jpg
    27.6 KB · Views: 377
Waziri mkuu mstaafu, bwana John Malecela, amesema ana hofu ya Raisi Magufuli kuhujumiwa na ameitaka serikali imuongezee ulinzi na kwamba isidharau.Mzee Malecela pia amekwenda mbali zaidi kwa kukumbuka jinsi Mwalimu Nyerere alivyotaka kupinduliwa.

Chanzo:JamboLeo

Bora na wakubwa nao sasa waseme,wengine tumebaki tu yetu macho na masikio.

Huo ni uoga husio na msingi kwani ulinzi wa rais ni imara na murua au ndiyo aliyosema pinda kuwa mafisadi wakiguswa nchi itayumba?
 
Kweli kabisa.
Tukumbuke na yaliyotokea "ajali" ya Sokoine.
Wanaotikiswa safari hii wamo kambini mwa watawala.

Unataka kutwambia kuwa sokoine alifanyiwa kitu mbaya? Una ushahidi wa kujitosheleza?
 
ni vema wazee wetu wajifunze kukaa kimya badala ya kupayuka
Raisi wetu hahitaji kuambiwa hilo kwa sababu analijua vizuri sana kuliko hata wao
Nchi yetu kwa kasi hii ya mpendwa raisi wetu ni miaka miwili tu itakuwa kwenye nchi zenye uchumi wa kati ambao kasi yake ya upaaji itakuwa ni zaidi ya asilimia 20
Katika mazingira kama haya hata idara zetu za usalama zinajua umuhimu wa hili jambo lakini paia kikubwa ni kujua kwamba kila mwenye kutenda jema yupo poja na Mwenyezi Mungu
 
Kwa uzalendo wa Magufuli, analindwa na karibu nchi nzima sasa. Atakayemgusa amegusa hell fire
 
Anajipa tu ujiko.Hakumbuki yeye si rais tena. Na wala hatakaa awe tena milele. Hata akina Geo Davy na Gwajima wana walinzi.

Kwani urais ni nini? Akiamua anakuwa rais wa wacheza disco au wacheza bao
 
Hahahahaha CCM wameipenda wenyewe, ngoja waisome namba! Aie wengine yetu macho tu
 
Mambo haya yasizungumzwe kwa mzaha na kejeli ni mambo mhimu kwa taifa letu kutokana najuhudi zinazoganywa na rais wetu.
Matajili wengi wanaguswa sana na hizi juhudi za kubana matumizi unagusa mashirika ya ndege kampuni za uwakala makampuni ya kuuza magari hivyo si jambo la masikhara
Lakini unapozungumzia madawa ya kulevya unaigusa dunia maana mtandao wa madawa ya kulevya umeenea dunia nzima na wafanya biashara hii wa utajiri wa kupindukia huku wakimiliki vikosi vyao vya ulinzi katika baadhi ya nchi.
Tumuombee katika ibada zetu kama alivyosema yeye mwenyewe katika hotuba zake

Vipi cc ya ccm jana iligusia meli ya kigogo iliyokamatwa ughaibuni na meno ya tembo?
 
Back
Top Bottom