Malecela: Magufuli hatarini

Malecela: Magufuli hatarini

Mungu wa israel atamlinda maana anayoyafanya yanawasaidia sana watu wake
 
Hawezi kuwa mshauri wa kitaifa tena baada ya Mtera kumuona hana la maana bora kibajaji. Atuambie hiyo hatari no ipi kwanza na nani anamshuku kufanya hayo. Sio wamelala na mkewe aliyepigwa chini ubunge kama yeye wakiamka ndoto zao wanazitoa hadharani zijadiliwe.

Ndio nini hiki MKUU?
 
Kwa lipi alilofanya hadi atake kuuwa wa kufuguza wafanyakazi 70 mbwembwe za kumkuza wakati hajadeliver
 
Hata mataifa makubwa yaliyotufanya shamba la bibi pia sasa ni adui
 
Hii nchi bana kila mtu anatafuta KIKI,,, amiri jeshi mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama hawezi kushindwa kujua mahitaji yake kiulinzi na usalama, unless kama watu wanamuona -----. Magufuli anajua nini anafanya
Kwani yule jamaa wa nchi jirani Lawrence Kabila hakuwa Amiri jeshi mkuu wa Taifa lake la Congo?
Mbona aliuawa kirahisi mno na walinzi wake mwenyewe?
Cha muhimu cha kuzingatia ni kuwa hii vita aliyoianzisha hapa nchini, ingawa inaungwa mkono na Umma wa watanzania, lakini kikundi kidogo cha watu ambacho kina nguvu kubwa sana kiuchumi kutokana na mapesa mengi sana waliyoyavuna katika dili zao za kiufisadi, ndiyo watakaokuwa wanakerwa mno na vita ya kupambana na ufisadi aliyoianzisha Magufuli.
Kwa hiyo siyo jambo la kupuuza pale yanapotolewa maoni ya kumwongezea ulinzi Rais Magufuli.
Lakini lililo la muhimu zaidi ni watanzania wote kwa ujumla wetu, kumwombea kwa Mungu ili amkinge na njama zozote za kumhujumu katika hii vita kubwa anayoitekeleza ya kupambana na mafisadi papa.
 
Hawezi kuwa mshauri wa kitaifa tena baada ya Mtera kumuona hana la maana bora kibajaji. Atuambie hiyo hatari no ipi kwanza na nani anamshuku kufanya hayo. Sio wamelala na mkewe aliyepigwa chini ubunge kama yeye wakiamka ndoto zao wanazitoa hadharani zijadiliwe.

Hahaha huyo mzee siku hizi amekua mkulima wa zabibu, kwenye siku ya wakulima nilimuona analalamika hawapati pembejeo kwa wakati muafaka
 
Namuunga mkomno Mzee Malechela kwani Mh. Rais ana maadui japo wachache lakini wenye jeuri ya pesa!!! Aongezewe ulinzi.

Ukona mzee anachangia kitu positively ujue kuna chambichambi kashaona. Ni bora wahusika waslidharau hili. Amina
 
Mambo haya yasizungumzwe kwa mzaha na kejeli ni mambo mhimu kwa taifa letu kutokana najuhudi zinazoganywa na rais wetu.
Matajili wengi wanaguswa sana na hizi juhudi za kubana matumizi unagusa mashirika ya ndege kampuni za uwakala makampuni ya kuuza magari hivyo si jambo la masikhara
Lakini unapozungumzia madawa ya kulevya unaigusa dunia maana mtandao wa madawa ya kulevya umeenea dunia nzima na wafanya biashara hii wa utajiri wa kupindukia huku wakimiliki vikosi vyao vya ulinzi katika baadhi ya nchi.
Tumuombee katika ibada zetu kama alivyosema yeye mwenyewe katika hotuba zake
 
Back
Top Bottom