Malecela: CCM isihusishwe na ufisadi

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Malecela-CCM isihusishwe na ufisadi

Na Waandishi wetu
30th August 2010


Malecela%2811%29.jpg

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), John Samwel Malecela


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), John Samwel Malecela, amesema kamwe CCM kisihusishwe na ufisadi kwa kuwa kimeonyesha jitihada kubwa za kulishughulikia tatizo hilo.

Malecela alitoa kauli hiyo juzi katika viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa, wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu Mkoa wa Iringa. Malecela alilazimika kuyasema hayo katika uwanja huo wakati akijibu hoja za wapinzani ambao alidai kuwa ajenda yao kubwa katika kampeni ni madai ya kuwepo kwa ufisadi ndani ya CCM.

“Wapinzani wetu watakuja hapa na nataka niwaambie wananchi wa Iringa kwamba, hoja yao kubwa watakayokuja nayo ni kwamba CCM ni mafisadi, lakini watambue kuwa ufisadi upo duniani kote na si Tanzania tu,” alisema.

Malecela alisema ufisadi ni jambo ambalo linaitesa kila nchi duniani ikiwemo Tanzania, lakini jambo la muhimu ni jinsi ambavyo serikali inayoongozwa na CCM.

“Mafisadi ni sawa na majambazi hivyo wasihusishwe na CCM. Serikali yake na hata shughuli zingine zozote zinazofanywa kwa niaba ya CCM, jamani si sahihi kusema kwamba CCM ni mafisadi,” alionya.

Alisema kwa kutambua hilo, Serikali ya CCM imeimarisha mahakama na kwamba watuhumiwa wa ufisadi wamepelekwa huko ili kujibu mashitaka yanayowakabili.
“Serikali ya CCM ni ya utawala bora na wa haki inayofuata utawala wa sheria, sasa wanaotaka kila anayetajwa kuwa ni fisadi tumshughukie kama wanavyotaka wao, itakuwa siyo kutenda haki, tumewaachia mahakama,” alisema.

Hata hivyo, alikiri kwamba CCM haijamaliza matatizo yote ya wananchi, lakini akadai kwamba ndicho chama ambacho kina mwelekeo mzuri na mikakati inayotekelezeka kuendelea kushughulikia kero za wananchi.

Pia, alikiri kwamba rasilimali za nchi hususani madini kutomnufaisha mwananchi wa kawaida awali, lakini Serikali iligundua na kuunda kamati ambayo ilitoa mapendekezo mazuri yaliyopelekea kutungwa kwa sheria nzuri ya usimamizi wa madini ambayo itawafanya wananchi wanufaike nayo.

Malecela pia alitumia muda huo kuzungumzia mgogoro ndani ya CCM Wilaya ya Iringa mjini ulioibuka baada ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kuondoa jina la Mgombea aliyeongoza kwenye kura za maoni, Frederick Mwakalebela.
Imeandikwa na Mawazo Malembeka na Godfrey Mushi, Iringa.


CHANZO: NIPASHE

Serikali ya Tanzania ni ya chama kimoja, na watendaji wake ni wanachama wakuu. Ni vipi unaweza lutenganisha hivi viwili? Hata ushahidi unaonekana kuwa wahusika wakubwa katika ufisadi ni hao hao viongozi waliopo ccm. Haihitaji akili nyingi kujua kuwa uongozi wa ccm ni chanzo cha ufisadi na kinaendeleza na kukumbatia ufisadi. ccm=UFISADI.
 
Atakuwa hakumsikia Marando huyu.....Tido unaona madahara yako ya kuzima TBC1?.......sasa Mzee wako is out of touch....nafikiri yuko Iringa bila Mama pia ndio maana anaongea hivi.....so sad....inanikumbusha Tyson na Matumla walipokuwa wanadundwadundwa na watoto katika ngumi zao za mwishomwisho.....baada ya mapambano hata post-macth interview ni maneno ya ajabuajabu tu...Mzee please try to stay at home and do some hobbying like gardening, reading, and stop this swiming in mud...
 
Huyu aende akamfanyie kampeini Livingstone Lusinde kule Mtera. Iringa kafuata nini kama siyo kutaka kuvunja nyumba ya mtu.
 
Kaa Kimya Malecela muda wako kisiasa umekwisha!

Huyu jamaa naona busara zinampotea kama si kutokomea kabisa. Kwanza ilani ya CCM inasema rushwa ni adui wa haki halafu yeye anakiri ufisadi upo kila mahali ikisha anatuambia CCM isihusishwe na ufisadi. Kwa mtu mwenye akili ataona kama anakiri ni kweli wao mafisadi lakini duniani kote kuna mafisadi hivyo si cha ajabu. Naweza tukana bure kwa hasira!!!!!!
 
Huyu keshakataliwa na wanaCCM wenzake tena wa nyumbani kwake sasa tutamwelewaje, charity starts at home mbona hapigi kampeni Mtera?
 
Aliyewahi kuwa waziri mkuu na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Mh John Malecela, ameshangaza umati aliyokuwa akihutubia Iringa kwa kuweka bayana kuwa ufisadi umehalalishwa na serikali ya CCM. Alienda mbali zaidi na kusema nchi zote duniani kuna ufisadi kwa maana hiyo haoni sababu kwanini wapinzani wanahoji ushiriki wa CCM kwenye ufisadi uliokithiri.

Nanukuu maneno yake!

“Wapinzani wetu watakuja hapa na nataka niwaambie wananchi wa Iringa kwamba, hoja yao kubwa watakayokuja nayo ni kwamba CCM ni mafisadi, lakini watambue kuwa ufisadi upo duniani kote na si Tanzania tu,” alisema Malecela.
Nipashe:

Huyu Mzee haeleweki sijui hata anatetea kitu gani!
 
Huyu anasubili fadhira ubunge wa uhuruma.
Lakini kesha jichokea aendelee kulima mizabibu na kutunza wajukuu tu.
 
Wamezoea, Mzee Malecela anajiamini sana, tena siku hizi ni nadra sana akasikika anajenga hoja, anajisemea tu maana anaamini neno lake litapokelewa bila kuguswa. Tumsamehe tu!!!

Ila kuna kitu ambacho sijakielewa bado; hawa wananchi ndugu zetu huko vijijini, ni nini kinawatuma kwenda kuwasikiliza hawa watu miaka nenda rudi, hadithi ni zile zile, maisha ni yale yale, watu ni wale wale, lakini bado tu wanajitokeza kuwasikiliza. Ni mahali gani tunakosea! Kwa nini wakiambiwa mapya wanasita!

Tunahitaji programu za radio zaidi, magazeti hayawezi kwani ni lazima wayanunue na hawana hela, ni lazima wayasome na wengi wao hawajui tena kusoma (elimu ya ngumbaru ilikufa na Nyerere), wengine wanajua kusoma lakini wana shida ya macho na huko vijijini hakuna kliniki za macho, na Aga Khani hawajaweza kutembelea kote.

Mungu wabariki wanakijiji wetu wote!
 
Malechela bana. Nyerere alimpiga rungu la nguvu bado akasavaivu, ccm wameendelea kumtwanga marungu bado kinganganizi. Kweli hili ni Tinga.
 
Aliyewahi kuwa waziri mkuu na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Mh John Malecela, ameshangaza umati aliyokuwa akihutubia Iringa kwa kuweka bayana kuwa ufisadi umehalalishwa na serikali ya CCM. Alienda mbali zaidi na kusema nchi zote duniani kuna ufisadi kwa maana hiyo haoni sababu kwanini wapinzani wanahoji ushiriki wa CCM kwenye ufisadi uliokithiri.

Nanukuu maneno yake!

Nipashe:

Huyu Mzee haeleweki sijui hata anatetea kitu gani!
duh... mzee yuko shallow sana aise... kama viongozi wenzake wa juu wa ccm!!! sintashangaa kauli hii akiitoa pia KJ, Kingunge, Msekwa, Makamba, Chiligati, etc. maana wanafanania na hii kauli ya tingatinga [aka kibajaji]

sijui huwa wanakula nini hawa jamaa wakishapata uongozi ndani ya ccm???
 
Ni wakati wa Mzee Malecela kupumzika,kadili unavyojaribu kujipambanua katika viwanja vya siasa ndivyo unazidi kukipunguzia chama chako kura za kishindo .Wakati umefika ukatulia na pension yako.Uzee ni ugonjwa ndio maanake kuna umri wa kustaafu.Wakati ni ukuta.
 
Huyu mzee vipi kuanza kulalama? Walikuwa wote na marehemu kolimba katika jitihada za kuisafisha ccm, akamsaliti na kumtosa kwa hakuwa na immunity kama zake hivyo akolimbwe. Lakini tunamkumbuka kolimba siku zote kwa kuwa altuiachia usia na alikufa akiutetea ndani ya kamati kuu ya ccm huko dodoma baada ya kudaiwa kuwekewa kitu katika maji aliyopatiwa kilichopandisha msukumo wa damu na kupelekea kifo chake. Marehemu kolimba alidai kuwa"ccm haina dira wala muelekeo".

Ufisadi ni sifa kama zilivyo sifa zingine zote walizo nazo ccm kama vilekuleta ukombozi kusini mwa afrika, kujenga amani na utulivu tanzania n.k. Kama ilivyo ada kujenga taswira fulani ni rahisi sana, lakini kulilinda taswira hiyo ndio kazi ilipo. Hivyo viongozi wa ccm baada ya nyerer wamepwaya katika viatu vyake kwa kushindwa kulinda sifa alizozijenga na udhaifu huo ukajitokeza kwa kujenga sifa mpya kutokana na matendo ya viongozi wake ambao ni ufisadi.

Kama ufisadi ni wa mtu au watu, watu wenye tuhuma kubwa kubwa za ufisadi ndio hao wanaokaa mzea kuu katika mikutano ya kamati kuu ya ccm na halamashauri kuu? Mtu kama chenge mwenye kutuhumiwa na kuchunguzwa na taasisi za kimataifa kwa makosa ya kiahalifu na kutuhumiwa mpaka kugushi bima ya gari mabona bado ni mwenyekiti wa kamati ya maadili ya kamati ya ccm?

Mbaona wabunge walioko mahakamani kwa tuhuma mbali mbali k.m mramba n.k wamepitishwa na vikao vya kifisadi vya ccm kuendelea kugombea kuongoza taifa hili?

Inamaan hakuna wanaqccma wengine wasiokuwa na tuhuma kuongoza?

Kwa hali hiyo haiwezekanai kutenganisha ufisadi na ccm hata siku moja hadoi siku ya kuingia kaburini.
 
Back
Top Bottom