Malecela: CCM isihusishwe na ufisadi

Malecela: CCM isihusishwe na ufisadi

Nilitegemea aseme hivyo kabisa kwani CCM haiwezi kuung'ata mkono wa mafisadi unaowalisha
 
Mnataka huyu mzee akale polisi?!! Akienda huko kwenye kampeni ndio nae anapata posho na honoraria..
 
Uhai wa CCM ni ufisadi na ndio maana ukiupiga vita ufisadi unakuwa adui mkubwa wa CCM na serikali yake. Ufisadi ndio mashine ya hewa ya oxygen wanayopumulia CCM ikilindwa na dola, ukitaka kuuondoa ujue umeamua kupambana na dola na hiyo ndiyo hali tunayoishuhudia hivi sasa. Wanaoitetea CCM wananufaika na ufisadi na ndio maana watu kama Cigwiyemisi John Samwel Malecela hawatoki humo, hawana ubavu huo kwani wameishaathirika vya kutosha na kuishiwa nguvu.
 
Uzuri wa siasa hasa wakati wa Uchaguzi ni kwamba mpinzani ana ruksa ya kutumia makosa ya utawala kiutendaji na kuwa sababu kubwa ya kuwaondoa madarakani. Na CCM wali underestmate uwezo wa Chadema ifikapo uchaguzi mkuu huu. Wao walijua haya mambo yatakwisha na kusahaulika mapema kabla hata ya uchaguzi wa mwaka huu. Lakini imepita miaka minnne bado wananchi wanakumbuka kama ilitokea jana tu.

Sasa maadam wameacha wao nafasi ya kushambuliwa, wakidai kwamba CCM yote sio ya Mafisadi ila baadhi ya viongozi WAO na kwa kusema hivyo, CCM imewaacha hao viongozi ndani ya chama tena wengine kugombea Ubunge hali bado ni watuhumiwa makubwa. IMEWAPONZA!...

Haya ni makosa makubwa sana na Chadema wametumia mwanya huu kutonesha donda la wananchi.
Mimi nilidhani JK sio mjinga kiasi hicho kuwacha hili swala la mafisadi wazi kiasi hicho. Nilitegemea kufikia mwezi wa huu wa nane angewaangusha watu wenmgi sana ikiwa ni pamoja na Lowassa, Rostam, na kundi lote la watuhumiwa ambao sidhani kama wangekosa lolote kwani tayari walikwisha chuma Utajiri. Kwa kufanya hivyo JK angejipatia sifa zaidi kwamba kaweza kuwashughulikia mafisadi baada ya uchunguzi kukamilika.

Lakini maadam JK kachagua kufa na tai shingoni akijua wazi kwamba tawala nyingi sana duniani zimeangushwa kwa SHUTUMA za Ufisadi pasipo hata kesi zao kufikishwa mahakamani, bila shaka Kachemsha vibaya sana...hizi zilikuwa hesabu mbovu sana kwake na chama kizima.

CCM wasiwalaumu Chadema kwa kutumia Ufisadi na hata kuwataja watuhumiwa ambao kesi zao zipo mahakamani. Ni mbinu inayokubalika kisiasa na siku zote maadam mtuhumiwa ni mwanachama na mgombea na yupo under investigation as a SUSPECT, hapa principal of conscious creation to manifest the circumstances inakuwa applied..In this case UFISADI (the law of attraction) ambayo ndiyo wameshtakiwa (tuhumiwa) inaweza kabisa kutumika til proven otherwise.

Kwa hiyo CCM ku deny all what happened kwa kujaribu kufagia chini ya uvungu ni makosa yao wenyewe hali wakijua fika kwamba hawa watu walitumia vibaya madaraka yao na kujineemesha kwa mabillioni ya fedha ambazo zimefanyiwa hata uchunguzi na vyombo vya nje na kuonekana ZIMEIBIWA - Bado sijui walikuwa wakifikiri kitu gani hata kuwaruhusu hawa kina Lowassa na Rostam kubakia ktk uchaguzi huu..

Ninaamini kabisa kama JK angeweza kuwaondoa Lowassa, Rostam na badhi ya viongozi ambao wanafikiri wana UBIA naye (untouchables) hata kuweza kujinufaisha wao kwa mali ya serikali basi bila shaka ingekuwa kazi kubwa sana kwa Chadema ya chama chochote kutumia Ufisadi kama ni udhaifu wa utawala wake. Na hakika ni vichekesho kumsikia Malecela akizungumza Ufisadi kwa ufinyu kiasi hicho.

Hata sisi tulipokuwa tukipigania Uhuru wetu tulijua fika kwamba sio Wazungu woote walikuwa watawala wetu au sio wazungu woote walikuwa wabaguzi isipokuwa ni kutokana na serikali yao kutoona ubaya wakutawaliwa, kuweka tabaka baina ya watawala na watawaliwa ndipo cheche za chuki zilivyoweza kushamiri hadi wananchi wakaweza kudai Uhuru wao. Na hakika mkoloni hakuweza kuelewa kabisa kwanini wananchi walitaka Uhuru hali walikuwa wakipewa almost kila kitu kwa ubora, uchumi bora na pengine hata kuletewa vitu vya Ulaya ambavyo wasingeweza kuvipata.

Kile kidogo walichosahau ndicho kilikuwa chanzo cha kuondoka kwao, nacho ni - IGNORANCE.
 
Wamezoea, Mzee Malecela anajiamini sana, tena siku hizi ni nadra sana akasikika anajenga hoja, anajisemea tu maana anaamini neno lake litapokelewa bila kuguswa. Tumsamehe tu!!!

Ila kuna kitu ambacho sijakielewa bado; hawa wananchi ndugu zetu huko vijijini, ni nini kinawatuma kwenda kuwasikiliza hawa watu miaka nenda rudi, hadithi ni zile zile, maisha ni yale yale, watu ni wale wale, lakini bado tu wanajitokeza kuwasikiliza. Ni mahali gani tunakosea! Kwa nini wakiambiwa mapya wanasita!

Tunahitaji programu za radio zaidi, magazeti hayawezi kwani ni lazima wayanunue na hawana hela, ni lazima wayasome na wengi wao hawajui tena kusoma (elimu ya ngumbaru ilikufa na Nyerere), wengine wanajua kusoma lakini wana shida ya macho na huko vijijini hakuna kliniki za macho, na Aga Khani hawajaweza kutembelea kote.

Mungu wabariki wanakijiji wetu wote!

Njilembera, inaelekea muda mrefu hujaenda vijijini. Kule tamko la kiongozi wa chama tawala ni sawa na agizo la serikali. Vijijini hawaalikwi kuhudhuria vikao - wanaambiwa waende! Usiposhiriki unatengwa, upinzani ni sawa na adui - wanaishi kwa woga wa kuiudhi serikali iliyopo madarakani. Wazee wanataka amani, kwani watoto wanakimbilia mijini na kuwapelekea wajukuu na visenti kidogo kidogo, hivyo kuwalazimu wazee waone aliyepo madarakani ndiye mlezi halisi na si wale wanafamilia walioko mijini ambao huja katika jeneza tu
 
Mzee wa Kigogo yuko desperate...katika kuogopa kummwagwa na Anne Kilango (maake yule mama ni sha*****ngi anayependa umaarufu) anaitafuta ile portfolio aliyokuwa nayo Kingunge ya kuteuliwa na JK endapo atashinda urais.
Lakini atashangaa... kwani JK uchaguzi huu hali ni tete!
 
Kweli wananchi wa Mtera hawakukosea kwenye kura za maoni, huyu Mzee nadhani anawalakini kidogo kichwani, kwani hata kama angekuwa anawahutubia wagonjwa wa akili Mirembwe, alipaswa kuchagua cha kusema, ama ndio tuseme Iringa ni wagonjwa wa akili kuliko walopo Mirembwe? Kweli CCM kimekuwa ni chombo cha dharau lakini hii imezidi !!!
 
Anajikaanga mwenyewe hata sijui nilini huyu babu atasema nimepumzika siasa nibora atulie siasa!!
 
Mzee ana mtindio wa ubongo kutokana na umri mkubwa. Halafu tukumbuke kuwa aliambulia Tsh. 200,000,000 toka kwa Jeethu Patel kwenye arusi yake na mama Anne Kilango, na hii ni kwa mujibu wa SS, Waziri wa Utawala bora.
 
Malecela Ni Mzee,

Huyu ninavyomjua mimi ni mtu mbinafsi, ni mroho wa madaraka, alitaka kupaka madarak, Nyerere akataa.

Huyu bwana ni Fisadi wa akili, amewalaghai sana watu kwenye kampeni nyingi. Nadhani kwa ushauri, apumzike kabisa na asijaribu

kujihusihsa na kampeni za mwaka huu mpaka afe.

Hebu tumuulize ingekuwa serikali ya Nyerere kweli Lowasa angekuwa wapi leo?, AU Dk Slaa angekuwa ndiye rais tayari EPA pepole

wangekuwa wapileo.

Malecela yuko kwenye machela kwa sasa, anhitaji matibabu ili uzee wake usimtese lakini si kufanya kampeni za ulaghai.

Anajua fika kuwa CCM haina tena uthubutu wa kuiongoza Nchi ila anahofia asipoipigia kampeni akifa hatapewa heshima, namshauri

ni bora asema ukweli jinsi chama kilivyoasi na skifa atakuwa kafia ujasiri kuliko kufia mawazo mfu.
 
Huyu jamaa naona busara zinampotea kama si kutokomea kabisa. Kwanza ilani ya CCM inasema rushwa ni adui wa haki halafu yeye anakiri ufisadi upo kila mahali ikisha anatuambia CCM isihusishwe na ufisadi. Kwa mtu mwenye akili ataona kama anakiri ni kweli wao mafisadi lakini duniani kote kuna mafisadi hivyo si cha ajabu. Naweza tukana bure kwa hasira!!!!!!

He's on drug!!
 
Some of these used politicians should retire from retirement. Mwalimu alisema CCM inanuka rushwa. Hukumsikia?

Dili zote kubwa za wizi wa mali ya umma na rushwa zinahusisha viongozi wa ngazi za juu za CCM. Sasa iweje CCM isihusishwe na UFISADI?

Mimi nilisoma Mkwawa. Kuna ulanzi mzuri sana sehemu zile. Labda wamemkirimia Mzee vizuri mno?
 
MTU B nimekukukubali sana!!!!!!!!!!!! hoja yako ni ya msingi sana! imefika wakati hapa forum hata kujadili hoja za msingi imekua vigumu! watu wenye mlengwa wa chadema hata tu kujadili mambo kwa uhalisia hawawezi wamezidisha mahaba sana! jamani hapa tunafurahisha genge tu ccm lazimaitashinda wamejipanga kuanzia ngazi ya kaya hadi kitaifa! chadema haijasimamisha wagombea ubunge zaidi ya majimbo 150 sasa wanashinda kwa nguvu za giza au kwa mazingayombe! jamani mipangaoooooooooooo inatakiwa tutashabikia lakini wote tunajua oktoba 31 nini kitatokea!!!!!
 
MGOMBEA urais wa Chadema, Dk.Willibrod Slaa na mkewe mpya, Josephine Mushumbusi, watafunguliwa kesi wakidaiwa fidia ya Sh bilioni moja na mume wa ndoa wa Josephine, Aminiel Mahimbo.

Kesi hiyo itakayofunguliwa leo katika Mahakama Kuu inawataka Slaa na Josephine kulipa fidia hiyo kutokana na mgombea huyo kudaiwa kumnyang'anya mke Mahimbo na Josephine kuvunja mkataba wa ndoa ya mke na mume mmoja.

Mwanasheria wa Mahimbo, Abduel Kitururu, aliwaambia waandishi wa habari jana Dar es Salaam, kuwa kesi hiyo imeshaandaliwa ikiwa ni pamoja na vielelezo vyote; vyeti vya ndoa, vya kuzaliwa watoto wawili na picha za ndoa.

Alisema, mteja wake anadai fidia ya Sh milioni 200 za usumbufu aliopata baada ya Slaa kumtangaza mkewe wa ndoa kuwa mchumba wake, huku akijua ni kinyume cha sheria.

Alisema Sh milioni 800 ni hasara za jumla ambazo wanaamini madhara aliyopata yanalingana na gharama hizo na anastahili kulipwa kabla hajafungua kesi nyingine kwa mujibu wa sheria ya ndoa, itakayoshughulika na masuala ya talaka na malezi ya watoto.

"Kwa sasa tunafungua kesi ya madai ya fidia kutokana na Dk. Slaa kumnyang'anya mteja wangu mkewe wa ndoa na kumtangaza kwenye majukwaa kuwa ni mkewe na pia Josephine kuvunja mkataba wa ndoa uliosainiwa kanisani na si suala la sheria ya ndoa," alisema Kitururu huku akionesha nakala ya cheti cha ndoa ya Mahimbo na Josephine.

Alisisitiza kuwa kesi hiyo haitahusu sheria ya ndoa wala malezi ya watoto, kwani kwa mujibu wa sheria, aliyeoa au kuolewa kidini kwa ndoa ya mke na mume mmoja, haruhusiwi kuoa wala kuolewa wakati mwenziwe yuko hai, labda ndoa hiyo ikibatilishwa na kuwa ya wake wengi.

"Ndoa ni mkataba na mmoja anapouvunja anapaswa kumlipa fidia mwenzake … mteja wangu anapaswa kulipwa fidia kwa Josephine kuvunja mkataba na suala hili halina uhusiano wowote wa kisiasa, bali imetokea kama ajali tu wakati huu siasa zikipamba moto," alisema kuondoa hisia kuwa suala hilo lina uhusiano na kampeni za kisiasa zinazoendelea.

Alisema mteja wake alifika katika ofisi yake kuitaka kufungua kesi hiyo ya madai dhidi ya Slaa na Josephine, kutokana na kunyang'anywa mke wa ndoa waliyofunga katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama na kufungishwa na Mchungaji Lewis Hiza wa kanisa hilo.

Alisema wakati huo, Mahimbo alikuwa na miaka 30, Josephine akiwa na miaka 26 na mashahidi wao wa ndoa walikuwa ni Sam Paul na Roselyn Paul na baada ya ndoa hiyo, walipata watoto wawili Upendo mwaka 2003 na Precious mwaka 2007.

Alidai katika ndoa yao waliishi Kimara Baruti na mwanzoni mwa mwaka huu, Josephine alianza safari za mara kwa mara na mumewe kuamini ni za kikazi lakini Aprili mwaka huu, aliondoka nyumbani kwao na watoto.

Kitururu alidai kwamba Mahimbo alifanya uchunguzi na kubaini kuwa wawili hao wanaishi hotelini na kwenda kuona watoto wake, na akaelezwa na mmoja wa wafanyakazi hotelini hapo kuwa mkewe anaishi na Slaa mbali ya hivyo Slaa amekuwa akimtangaza katika mikutano ya kampeni kuwa Josephine ni mkewe, wakati bado hajaachana na mumewe.

Akizungumzia suala hilo, Slaa alisema hana wasiwasi na kufunguliwa kesi na kutaka Mahimbo aulizwe wakati anaporwa mkewe yeye alikuwa wapi.

Alidai kuwa hizo ni kampeni chafu za kutaka kumharibia katika kipindi hiki na kwamba zinafanywa na CCM na kudai kuwa chama hicho kimemnunulia gari Mahimbo ili amchafue.
 
Bad campaign by the opposition parties. Instead of stressing about your future policies and strategies, you start whining about corruption. That's why the majority of the Tanzanians still overwhelmingly approve the job that has been done by CCM since independence because its leadership is lase-focused on how they can improve the economy and the lives of the citizens. There's no corruption in this country. If so, then why Chadema and CUF are not winning elections? Stop making false allegations about JK/CCM.
Vote CCM
 
Back
Top Bottom