Malecela: CCM isihusishwe na ufisadi

Malecela: CCM isihusishwe na ufisadi

Huyu mzee bana. Anadhani bado ni tinga tinga, wakati sisi tunajua limekwisha hilo...

Hana jipya huyu...
 
duh... mzee yuko shallow sana aise... kama viongozi wenzake wa juu wa ccm!!! sintashangaa kauli hii akiitoa pia KJ, Kingunge, Msekwa, Makamba, Chiligati, etc. maana wanafanania na hii kauli ya tingatinga [aka kibajaji]

sijui huwa wanakula nini hawa jamaa wakishapata uongozi ndani ya ccm???

Mkuu mbona walishasema tayari!!! Rushwa iliyokuwa kwenye kura za maoni walisema ipo kila sehemu na wote walitoa rushwa isipokuwa walizidiana dau! Shame on them!
 
Ehh bwana weee, ina maana yeye na huyo mama anayegombea ubunge? Kwani yule mama kaolewa?

Wee Mume wa mama Mbega sijui, angalia maneno haya chini na CUHUNGE MZIGO WAKO.......

Mama Anna na wewe chunga mzigo wako usije ukaachia ngazi na wewe......

Tatizo la UFISADI kwa CCM ni kuwa MSINGI wa serikali ya awamu ya nne, umejengwa kwenye UFISADI. Wakiubomoa basi na nyumba itaanguka. Ndiyo maana walikata LIVE show ya TBC1 pale wajenzi wa huo msingi wa Ufisadi walipotajwa.

Tukitaka kuumaliza ufisadi ni kuwataja WAASISI wa Ufisadi kama alivyosema Marando. Kuumauma maneno na kuzunguka kwa ohh, serikali ya Kikwete, ohh CCM, ni kupoteza muda. Watajwe wenyewe moja kwa moja. Mkapa, Rostam Azziz, Lowassa, nk nk na siyo unatutajia akina Kagoda, Mhindi gani sijui, mhhhhhh....................
Huyu aende akamfanyie kampeini Livingstone Lusinde kule Mtera. Iringa kafuata nini kama siyo kutaka kuvunja nyumba ya mtu.
 
Mkuu mbona walishasema tayari!!! Rushwa iliyokuwa kwenye kura za maoni walisema ipo kila sehemu na wote walitoa rushwa isipokuwa walizidiana dau! Shame on them!
cha kusikitisha kabisa ni kwamba rais ameshindwa kukemea kauli zinazohalalisha rushwa kwani yeye ni mmoja wao

too bad!!!

Hivi Z'bar nako kuna rushwa?
 
Mkuu mbona walishasema tayari!!! Rushwa iliyokuwa kwenye kura za maoni walisema ipo kila sehemu na wote walitoa rushwa isipokuwa walizidiana dau! Shame on them!

Makamba amekiri hili la rushwa, na kusema "kama ni rushwa wote wametoa" huyu ndo GS wa CCM!!!
Mzee kafulia hana uwezo wa kufikiri tena! Kawa kama Makamba tu... lol
 
hii message ya baba wa taifa imetulia, ndio maana CCM hawataki kutoka madarakani, Chadema tengenezi poster mnacapitalize hapahapa " Kila nilipokuwa nikitaka kung'atuka, walikuwa wakiniambia Mwalimu andelea tu, hii nchi bado ni changa na umeitoa mbali, nchi haitaendelea bila wewe. Nami niliendelea, hadi pale nilipokuja kugundua kumbe nchi changa wanayoiongelea ni FAMILIA ZAO, na hazitaendelea bila mimi kuwepo madarakani, maana walikuwa hawana uhakika kama RAIS ajae atawaacha katika nafasi walizokuwa nazo" Julius Nyerere
Haya ndio maneno wasemayo viongozi wetu wa sasa, wanasema BILA CCM nchi haitaendelea, lakini ukweli ni kuwa BILA CCM ufisadi wao hautaendelea, maana hawan uhakika kama CHAMA kingine kikichukua nchi watabaki salama!
 
cha kusikitisha kabisa ni kwamba rais ameshindwa kukemea kauli zinazohalalisha rushwa kwani yeye ni mmoja wao

too bad!!!

Hivi Z'bar nako kuna rushwa?

Acid! JK hawezi na wala hao thubutu kukemea rushwa, yaani ni sawa na mtu kukata tawi la mtu ulilokalia, Rushwa ndio imembeba JK hadi kufikia hapo alipo, akiikemea tu basi ndio anguko lake! yaani dawa hapa ni sisi wananchi kuukata mti ulio na tawi alilokalia JK ifikapo October 31, this year! maana UWEZO TUNAO! NIA TUNAYO NA SABABU TUNAYO!
 
Pumzika kwa amani mzee wetu, hakuna anayekusikiliza tena. Hao thithiem hawakutaki!! Kama wangekutaka alama za nyakati ungeshaziona. Kula pensheni kaka. Umeshakuwa mfupa aliouhsinda fisi!! Tehe tehe!!
 
hii message ya baba wa taifa imetulia, ndio maana CCM hawataki kutoka madarakani, Chadema tengenezi poster mnacapitalize hapahapa " Kila nilipokuwa nikitaka kung'atuka, walikuwa wakiniambia Mwalimu andelea tu, hii nchi bado ni changa na umeitoa mbali, nchi haitaendelea bila wewe. Nami niliendelea, hadi pale nilipokuja kugundua kumbe nchi changa wanayoiongelea ni FAMILIA ZAO, na hazitaendelea bila mimi kuwepo madarakani, maana walikuwa hawana uhakika kama RAIS ajae atawaacha katika nafasi walizokuwa nazo" Julius Nyerere
Haya ndio maneno wasemayo viongozi wetu wa sasa, wanasema BILA CCM nchi haitaendelea, lakini ukweli ni kuwa BILA CCM ufisadi wao hautaendelea, maana hawan uhakika kama CHAMA kingine kikichukua nchi watabaki salama!

Asante. Ila kila kitu kina mwisho wake. Vyama mbadala visichoke kupambana, na kwa sasa hebu jaribuni kuungana mpisheni Dr. Slaa ambaye anarusha karata kwa mara ya kwanza maana nyie wengine mlishashindwa huko nyuma tena na umaarufu umeshapotea. Sasa kwa nini msiungane kwa urais mkampa Dr. Slaa na ubunge mkapigania tu seat!! fungukeni macho ndugu zanguni.

Ila nina hofu kuwa Marando ametumwa kuja kuwachafulia. Kuweni makini sana, yeye na wengineo ni mapandikizi tangu enzi hizo??? Msimshirikishe sana mipango yenu.

Lakini naskia Mzee Malecela ana sauti kubwa sana ndani ya CCM na wanamwogopa kweli.
 
Ukiona wazee kama hawa wanaongea hivyo ni dhahiri kuwa CCM ni mafisadi, Mzee Samweli na Kingunge ni mafisadi wakuu na wanajijua ndio maana full kurudishwa bungeni kawa fadhila za JK.
 
Aliyewahi kuwa waziri mkuu na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Mh John Malecela, ameshangaza umati aliyokuwa akihutubia Iringa kwa kuweka bayana kuwa ufisadi umehalalishwa na serikali ya CCM. Alienda mbali zaidi na kusema nchi zote duniani kuna ufisadi kwa maana hiyo haoni sababu kwanini wapinzani wanahoji ushiriki wa CCM kwenye ufisadi uliokithiri.

Nanukuu maneno yake!

Nipashe:

Huyu Mzee haeleweki sijui hata anatetea kitu gani!

Msekwa alishasema exactly the same thing. Sasa hiki kusemwa na kiongozi wa ngazi ya juu mmoja wa CCM watu wangeweza ku dismiss kwamba ni maoni potofu ya mtu mmoja, lakini tunaona mtu zaidi ya mmoja anatuambia hii habari.

Ina maana ni kitu cha kweli, CCM inakumbatia ufisadi, haioni ufisadi kama kero, haioni ufisadi kama jambo la aibu. Zaidi ya hapo inataka kuuhalalisha ufisadi kama kitu cha kawaida. Well kuanzia Colombia mpaka Mexico na sehemu nyingi tu duniani watu kibao wanauana kila siku, je CCM watakumbatia uuaji nao na kusema "uuaji ni kitu cha kawaida, upo duniani kote"?

Ufisadi ni kitu cha kawaida ? Kwa hiyo hata wale wanaotaka kuanzisha vita dhidi ya ufisadi waache siyo?

Ufisadi ni kitu cha kawaida? Ndiyo maana na wewe unahusika katika ufisadi siyo? Ndiyo maana mwaka 2005 katika kinyang'anyiro cha urais majambazi waliposimamisha gari la mke wako na kumsachi wakamkuta ana mamia ya mamilioni ya shilingi ? Zile hela ulikuwa unataka kufanyia ufisadi wa kununua kura siyo ? Ufisadi si ni kitu cha kawaida na upo dunia nzima tushangae nini sasa ?
 
Ukiona wazee kama hawa wanaongea hivyo ni dhahiri kuwa CCM ni mafisadi, Mzee Samweli na Kingunge ni mafisadi wakuu na wanajijua ndio maana full kurudishwa bungeni kawa fadhila za JK.

Sema mkubwa, huyo highlighted hapo juu ndiye kiongozi wa mafisadi. Ana tenda tata nyingi sana, kwa kumega tu tuanzie kile stand ya mabasi ya mikoani ubungo, Pinda alitaka kupachafua naona amenyamaza kama vile mdomo umejaa mabonge ya barafu!! Temeke ana tenda ya usafi na kampuni yake imejenga yard ya kuhifadhia magari ya taka na akamega sehemu ya barabara na kuziba mtaro. Viongozi hata kama ni wajasiriamali wanatakiwa watuonyeshe mfano bora wa utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali.

Mtaji wa CCM ni umaskini wa wawaDanganyika. Ni pale wenye nchi yao watakapo komboka kiuchumi ndipo CCM watakapo-ondoka madarakani. CCM wanalifahamu hili na ndio maana hawanadhamira ya dhati kuwakomboa wananchi kiuchumi. Pili ni kukosa elimu, wanatumia kuwahofisha wenye nchi yao vijijini kuwa wakija vyama vingine nchi itaharibika na vita n.k. Kwa mtaji huu ndio maana wameanzisha shule za voda fasta ilhali watotowao wako majuu kupata elimu inayofaa ili watakapo zeeka waendelee watoto kutawala hivyo kujihakikishia mwisho mwema. Mfano hai ni wakina Februari Katani, Dhoruba Kiwawa nk, nk
 
cha kusikitisha kabisa ni kwamba rais ameshindwa kukemea kauli zinazohalalisha rushwa kwani yeye ni mmoja wao

too bad!!!

Hivi Z'bar nako kuna rushwa?
Amkemee nani wakati ndiyo walio muweka Ikulu na Hiyo pesa ya Kifisadi....
 
inaonekana huyu mzee hakuwa amejiandaa kustaafu, amestaafishwa kwa manufaa ya watu wa mtera
 
Back
Top Bottom