Malecela angeukwaa urais ingekuwaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malecela angeukwaa urais ingekuwaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Calnde, Nov 23, 2008.

 1. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni John Malecela, mumewe Anne Kilango,

  Ameona matatizo ya mgomo wa vyuo vikuu, akatafakari kwa makini, akaona kwake yeye suluhisho ni kuwafukuza wote walioogoma na kuwapa udahili wale ambao waliomba nafasi wakakosa. Kwamba hakuna haja ya serikali kuhangaika na watu wasiojua umuhimu na maana ya elimu!

  Amenipa nafasi nitafakari,

  Je,kama serikali ikifanya hivyo,na hao watakaodahiliwa mara ya pili wakagoma watachukuliwa akina nani?

  Na je, katika sakata la walimu na makundi mengine wanaogoma kudai haki zao kwa mtazamo wake nini kifanyike?

  Hapo akanipa zaidi nafasi ya kujiuliza, Kama angeupata uraisi mwaka 2005 kama alivyokuwa akitamani, hali ingekuwaje? Angetatua vipi matatizo ya wananchi?
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Inaelekea yeye ndio atakayeyaweza kuyashughukilia matatizo yanaiyoikumba nchi ikiwemo ufisadi?

  Je ni wakati wa CCM kumfikiria kama mgombea urais kwa tiketi ya chama chao 2010.
   
 3. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #3
  Nov 23, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280
  urais si lelemama ..rais akiwa laini laini kama huyu ..ndio nchi hutawaliwa na migomo hata isiyokuwa na sababu...migomo mingine ingewezwa kuzuiwa kwa kuchukua hatua mapema za kusawazisha mambo au kutoa misimamo wakati muafaka...kwani watanzani ni waelewa....tatizo rais kauli zake haziheshimiki tena ...na that will cost us one day..........ukweli ni kuwa serikali haiwezi kulipia asilimia 100% za udahili kwa sasa ..hilo ni wazi ...kwani watoto wanaotaka elimu ni wengi....wenye uwezo lazima walipe.....msimamo huo ungewekwa wazi kwa watoto tangu awali tena kwa waziri husika kwenda pale nkrumah hall na kuwaambia watoto usoni....kwa ufasaha ..na kujibu hoja zao...nadhani wangeelewa..tatizo kuanzia rais hadi watendaji wake siku hizi wanaogopa kukutana na wanafunzi ana kwa ana ...hata rais alipokutana nao alikimbilia kuwabeba kwa mabasi hadi karimjee...so kwa namna hii hawa watoto watawasumbua tu,wanafunzi wa university wanapenda mtu aliye tayari kuwa face....kuna kipindi walitaka kugoma ..mkono alienda pale akawahubiria ....wakamuelewa..sasa kuwaagopa haisaidii..

  enzi za mwalimu alikuwa akienda mara kwa mara lushiriki kwenye midahalo yao..na hata akipata mgeni alienda naye pale kwa ajili ya lectures....kikwete anashindwa nini...na yeye alikuwa pale????...maghembe anashindwa nini na alikuwa lecturer SUA .....

  kimsingi MALECELA is strong na huiwezi kumlinganisha na kikwete ambaye hata tunajiuliza kama kweli alikuwa afisa wa jeshi......rais huwezi kumfurahisha kila mtu.....kuna mambo mengine lazima uwe na MSIMAMO USIOYUMBA....na hata watu wakuelewe hivyo ........
   
 4. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #4
  Nov 23, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Tungekuwa bora mara 101 kuliko tulivyo leo na huyu ndugu yetu!
   
 5. M

  Mama JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  okay okay Phil, kwa hiyo Malecela agombee urais 2010 kwa tiket ya CCM. What are his strengths and weaknesses?
   
 6. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Umri je? Au ndo utu uzima dawa!!?
   
 7. M

  Mama JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Iwapo anaweza kutoa busara za wanafunzi wote kufukuzwa na kudahiliwa upya? Hiyo yatosha.
   
 8. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mbona basi hamshauri mkuu, au hashauriki?
   
 9. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kama JK alikuwa jeshini na Makamba then unategemewa awe strong kivipi!!?
   
 10. M

  Mama JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  CCM ina credibility ya kuongoza ikiwa na viongozi wanaopepesuka kama huyu. Wakisapotiwa na upinzani.

  Mwenyewe Kitila wa Chadema keshamkubali, mambo mswano duh, Malecela for president 2010.
   
 11. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Mbona sioni busara hapa,or I have to read between lines?
   
 12. M

  Mama JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Wewe unaonaje, Malecela akiwa rais, Anne first lady, Tanzania without mafisadi is possible.
   
 13. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Dah, ushaanza kampeni! Haya Bwana. Nafikiri apumnzike au ataongoza kwa sapoti ya mkewe?
   
 14. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  labda mkewe amsaidie,Naye mbona yupo kimya siku hizi au anamalizia mambo vikaoni? Unajua wanawezekana kuonekana safi lakini wakishaingia kwenye system.....matatizo yanaanza
   
 15. M

  Mama JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  huyu mama ndio shujaa wa nchi hii, labda yeye agombee urais halafu mumewe awe first gentleman.
   
 16. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hakuna anayetufaa kati ya walo katika system kamwe. Kama wameshindwa kuwa viongozi bora why give them promo for presidency. Tanzania sio kama studio za bongo flava ati!!
   
 17. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #17
  Nov 23, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  uuhgh!! Hapo nimekuelewa. Lakini si waungwana wanamwundia Zengwe maana alikisema chama vibaya? Wanataka hata ubunge asiupate yule mama.Halafu watu wenye taaluma ya ualimu ni wazuri eenh! Baba wa Taifa alikuwa mwalimu,Aloyce Kimaro (Mb) Vunjo pia ni mwalimu,afi Kilango nae mwalimu! Sijui Anna Abdala ye nana maana....!
   
 18. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #18
  Nov 23, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  I believe kuna wachache wakisimama binafsi wanaweza! Tatizo ni system. Na ndo maana CCM wanaogopa wagombea binafsi maana ndani yao watameguka na ndo CCM itajizika yenyewe!
   
 19. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Malecela amekuwa kiongozi kwa muda mrefu sana lakini amefanya nini cha maana kwa Taifa letu?.
  Ukubwa wa pua si wingi wa makamasi, mzee huyu anakosa maadili.

  Na kuna tetesi kwamba Malecela na kingunge ni moja kati ya waasisi wa wizi wa EPA kwa lengo la kupata pesa za kampeni kwa ajili ya ushindi wa CCM. Kama ni kweli je anafaa kuwa raisi wetu?. Balali aliitwa na wazee hawa kule Dodoma na kuchimbwa mkwara ili awape hayo mapesa kwa ajili ya kampeni kuanzia za ubunge hadi Uraisi.

  Kwa maoni yangu hatuwezi kupata kitu kipya toka CCM, kwani si rahisi kumpa jina jipya mbwa mzee, tunahitaji mabadiliko kwa kuwa na chama pinzani ndani ya utawala. CCM imekuwa madarakani kwa miaka nenda rudi lakini ni uwozo mtupu kwa kifupi ni bora tulivyokuwa chini ya Mkoloni, hivyo ni muda sasa tukajaribu vyama vingine tuone tutafika wapi?. CCM wamelewa madaraka inatosha waondoke.
   
 20. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Malecela is so old school, nisingeshangaa kama angewashikia fimbo hawa vijana kama Nyerere.

  Malecela has been in the system since the sixties, and has a bigger sense of entitlement than Kikwete, potentially compounding his entlitlement borne issue to be bigger than Kikwete's.

  Malecela si ndiye huyu aliyewaaambia watanzania "they can go to hell"?

  Malecela mtu aliyekataliwa na wananchi wa jimbo lake katika ubunge ndiyo aende kuwa rais?

  Malecela ambaye Nyerere alimuita "muhuni"?

  Au Malecela gani?

  Kama ni huyu utakuwa assured nchi kuendeshwa na draconian grip kuliko ya Kikwete.Mseme Kikwete unavyotaka, na mimi namsema, the reason we fault him on fredom of press is because we demand impeccably high standards, lakini mpaka kufikia kufungiwa gazeti bongo lazima umekandamiza kiaina, tena ile si ki professional. Malecela angeendesha nchi kichama chama tungeona CCM inashika hatamu tena.Ingawa kwa watu wa CCM hii ndiyo wangetaka, kwa wapenda demokrasia hili lingekuwa pigo.

  Tunataka mtu ambaye eithert hakuwa kwenye top leadership kabisa au kaingia karibuni.Huyu Malecela kina Kikwete wamemkuta kashakaa serikalini miaka kibao.Vyeo alivyopitia Malecela in the 60s huko katika ngazi za mkoa kina Kikwete wamezipitia miaka ya 80, sasa kumtoa Kikwete na kumuweka Malecela kutakuwa progress kweli?
   
Loading...