Malecela and Dr. Salim - Into Oblivion?

JokaKuu,
Kuhusu wanajeshi wetu na mafao yao, kuna wakati wanajeshi waliokuwa Msumbiji walirudi na wakapelekwa kambi ya Tabora. Pale walipiga makelele kudai mafao yao Mwinyi akiwa kimya. Hatimaye wakamtishia. Na yeye akataka kupeleka kikosi cha FFU kupambana nao. Wataalamu wakamshauri hilo lingekuwa kosa kubwa sana. Hatimaye ilibidi Mzee Kambarage aingilie kati kusuluhisha mambo.
 
Mzee Jasusi & Joka Kuu,

Mwalimu alipokuwa akimshambulia rais wetu wa wakati ule Mwinyi kuwa hafai, Mwinyi akiwa izarani Msumbiji, aliwahi kumjibu Mwalimu kwa kusema kuwa

alifanya anayoweza kutokana na hali nchi yetu alivyoikuta, yaani kwenye giza na kuisogeza kwenye mwanga, lakini ktaika miaka yake kumi ya urais hakuwahi kutaka kupinduliwa na wanajeshi wetu hata mara moja, ukilinganisha na utawala wa Mwalimu. Mwinyi alidai kuwa hicho ndicho kinapswa kuwa kipimo muhimu kwa anyetaka kulinganisha utawala wa awamu ya kwanza na wa pili,

Ninaomba kusikia maoni yenu kwenye hayo maneno ya Mwinyi kufuatia hoja zenu za jeshi na Mwinyi!
 
Kaka bora umesema wewe maana kuna stori za kupikwa na zilizojaa nusu ukweli nusu uzushi kuhusu Mzee Mwinyi na majeshi. Lakini yote haya ni kwa ajili ya kukosekana documentation ya ukweli wa historia yetu.

Kaka Jasusi check data zako kabla ya kuconclude. Ama unapima ujuvi wa watu humu?

Tanzanianjema
 
Wanasiasa waliotajwa hapa JamboForums.com kwamba walikuwa in marafiki au wafwasi wa Oscar Kmbona - Fundikira, Malecela, Lusinde, Kamaliza, Mkapa na wengineo - hakuna ushahidi wowote unao onyesha kwamba walihusika na kesi ya uhaini, jaribio la mapinduzi October 1969, pamoja na Kambona?

Swali langu la pili ni hili: Kambona alipata msaada kutoka nchi za nje kujaribu kumpindua Nyerere? Nimesoma kitabu kimoja, "Nyerere and Africa: End of an Era," kilichoandkiwa na mzalendo mmoja, Godfrey Mwakikagile, na sijaona chochote katika kitabu hicho kinacho onyesha kwamba Kambona alisaidiwa na nchi za nje katika jaribio hilo.

Swali la tatu: Kambona na wafwasi wake - Bibi Titi Mohammed, Kamaliza, Colonel Chacha, Chipaka na mdogo wake - waliamini kweli kwamba wangefanikiwa kumpindua Nyerere, Watanzania wengi wangefurahi?

Nilipomaliza kusoma, "Nyerere and Africa: End of An Era," sikuwa na mashaka hata kidogo kwamba Nyerere alikuwa ni kiongozi halali na makini aliyekuwa mtetezi wa wanyonge. Na hakuwa na upendeleo wa aina yoyote - hata kidogo! Kuna watu wanaosema Mwakikagile aliandika kitabu hicho, kumsifu Mwalimu, kwa sababu yeye ni rafiki na watoto wa Nyerere na alifahamiana na Mwalimu. Lakini sijaona ushahidi wowote kuhusu "ukweli" huo, ingawa yeye mwenyewe katika kitabu hicho amesema kwamba alisoma shule pamoja na Andrew Nyerere pale Tambaza High School, na pia kwamba Benjamin Mkapa alikuwa mhariri wake gazetini "Daily News" na alimsaidia kwenda kusoma shule Merikani.

Na yuko wapi mzalendo huyo Mwakikagile? Anafundisha nchi za nje au amestaafu? Nimesoma bio yake online, "Godfrey Mwakikagile: Tanzanian Writer," na kuna nyingine katika wikipedia, "Godfrey Mwakikagile - wikipedia," lakini zote mbili hazisemi yuko wapi. Sijazungumza na Watanzania wowote wanaosema yuko nyumbani nchini Tanzania.

Pia nimesikia kwamba kuna viongozi fulani wa Kiafrika, miongoni mwao wa Kitanzania (wengi au wachache, sijui), ambao hawakufurahi alipoandika kitabu kimoja, "Africa is in A Mess."

Simlaumu. We are in a mess, big mess!
 
Kwa nini swali lisiwe,

Je ni kweli kulikuwa na mpango wa mapinduzi ama mwalimu aliingia mkenge wa maadui wa ukombozi Afrika waliokuwa na nia ya kumdistabilize?

Tanzanianjema
 
Joka Kuu & Jasusi,

The fact kwamba Mwalimu alitaka kupinduliwa na wanajeshi mwaka 1964, mnaionaje kulinganisha na matatizo ya jeshi under Mwinyi?
 
Joka Kuu & Jasusi,

The fact kwamba Mwalimu alitaka kupinduliwa na wanajeshi mwaka 1964, mnaionaje kulinganisha na matatizo ya jeshi under Mwinyi?

Mwaka 1964 halikuwa jaribio la mapinduzi. Wanajeshi wale walikuwa wanataka kitu kilichokuwa kinajulika wakati huo kama "Africanization." Baada ya uhuru, sehemu zote za serikali zilikuwa zinedeshwa na waafrika lakini makamanda wa jeshi walikuwa bado ni wazungu; kwa hiyo walikuwa wanataka wazungu waondolewe jeshioni kusudi makamanda wote wawe ni waafrika.
 
Mwinyi walimtishia akamua kuwanunulia magari maofisa wote!!!
 
Mzee ES,
Amini usiamini, isingekuwa mwingilio wa Mwalimu Mwinyi angepinduliwa na jeshi.
 
Kichuguu,
Lakini ukisoma kitabu cha Judith Listowell utaona kuna wajanja wachache waliojaribu kutumia uasi huo kuipindua serikali. Nina hakika kama Kawawa asingemficha Mwalimu kungekuwepo uongozi mpya 1964.
 
Ni nani waliojaribu kupindua serikali mwaka ule 1964? Victor Mkello na Christopher Kasanga Tumbo, also cited in "Nyerere and Africa: End of an Era."
 
Bianafsi nafahamu kuwa maasi ya 1964 hayakusukumwa na nia ya kuiondoa serikali madarakani kwani kama hiyo ndiyo ingekuwa nia, Nyerere asingetoka mafichoni akawa salama. Miaka hiyo tulikuwa na maofisa wachache sana watanzania, na ninaowakumbuka ni Sarakikya na Nyirenda. Askari wetu hawakuridhika na treatment waliyokuwa wanapata wakijilinganisha na askari wazungu waliokuwepo kama expatriates, na mkuu wa majeshi pia alikuwa mzungu. Hata baadaye Kambona alipoweza kuwatuliza na kuongea nao, moja ya sharti lao lilikuwa kuwa na mkuu wa majeshi mtanzania na hapo ndipo ilibidi kuchagua kati ya Sarakikya na Nyirenda. Binafsi naiona kama njia ya kudai haki yao sawa na wanafunzi wanaogoma vyuoni kwani njia yao hii ilifanya matakwa yao yakasikilizwa.
 
So kati ya Sarakikya na Nyirenda nani alipewa cheo??? Hivi Sarakikya bado ni barozi tuu au ameshastaafu!!
 
Gagnija,
Hakuna aliyesema uasi ule ulikuwa na lengo la kupindua serikali. Nilichosema ni kwamba "wajanja" wachache walijaribu kuutumia uasi huo kubadilisha serikali.
 
Jasusi,
Kitabu cha Maasi ya 1964 kinaeleza kwamba aliyewezesha kutoroka kwa Nyerere na Kawawa ni Mkuu wa Usalama wa Taifa wakati huo akiitwa Emelius Mzena. Inasikitisha kwamba Mzee Mzena amefariki na hakuna anayefahamu aliwaficha wapi Kawawa na Nyerere.

Wakati Mwalimu anajiuzulu Mzee Mzena alipewa nishani ya Utumishi uliotukuka. Pamoja naye alikuwepo Lt.Gen.Abdalah Twalipo na Lt.Gen.David Musuguru.

Pamoja na Nishani, Nyerere aliwapinda vyeo Abdallah Twalipo na David Musuguri kuwa Majenerali[4-Star]. Tukio hilo lilimfanya Twalipo kuwa Jenerali[4-Star] wa kwanza ktk JWTZ.

MAASI YA 1964 HAYAKUWA NA NIA YA KUPINDUA SERIKALI. WANGEKUWA NA NIA HIYO, WAASI WANGEMTANGAZA AMIRI JESHI MKUU WAO. HAWAKUFANYA HIVYO!!

WALICHOFANYA WAASI NI "KUMTEUA" MTANZANIA LT.KAVANA KUWA CDF. WAASI WALIMPA LT.KAVANA CHEO CHA BRIGADIER. KAVANA ALIKUWA ASKARI MSOMI MWENYE SHAHADA YA SAYANSI TOKA MAKERERE UNIVERSITY!!
 
Mzee ES,
majibu yako kwa maswali yangu hayajaniridhisha, lakini bado nayatafakari. umejibu kwa mafumbo, kwa kunirushia maswali.

Hivi Mama Julie Manning yuko wapi? Huyu Mama aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Sheria. Alikuwa mwanamke wa kwanza Mtanzania kupata shahada ya Sheria.

Mama Manning either alibwaga manyanga au alilazimishwa kujiuzulu. Sidhani kama aliondoka kwa wema.

Mzee ES, naomba taarifa za Mama Manning kama unazo.
 
jokaKuu,
Nilimfahamu marehemu mzee Mzena. Basi kama ni yeye aliyemficha Mwalimu na Kawawa basi alijua what was going on. Hivi hujawahi kujiuliza ni kwa nini kati ya mawaziri wote only Kambona was "friendly" to the mutinious soldiers? Wengine nasikia walipigwa bakora.
 
Inasemekana walifichwa katika kibanda cha nyasi Kigamboni. Katika kitabu cha "Nyerere and Africa: End of an Era," kuna chapter - Chapter 13 - "Coup Attempts Against Nyerere" kuhusu mambo hayo lakini hakuna details ni wapi wlifichwa.

Ni vizuri kuna Watanzania wanaondika vitabu kuhusu mambo ya siasa nchini Tanzania kama hicho, "Nyerere and Africa: End of an Era."

Wenzetu pia, hasa wa Afrika ya Magharibi, wamefanya hivyo; kwa mfano, Ghanaian Professor George Ayittey's "Africa Betrayed" and "Africa in Chaos"; Chinua Achebe, "The Problem with Nigeria"; Soyinka, "Open Sore of A Continent: A Personal Narrative of the Nigerian Crisis" and "The Blood-Soaked Quilt of Africa," na wengineo. Kwetu Afrika ya Mashariki kuna Ngugi wa Thiong'o aliyeandika vitabu vya aina hiyo na wengineo pamoja na Watanzania kama Godfrey Mwakikagile, "Africa is in A Mess."

And I know something about Mwakikagile - and the people who KNOW him. Contrary to what someone said in one of the posts here, Mwakikagile NEVER worked at "Uhuru" and "Mzalendo" - or at "The Nationalist" -newspapers where people like Costa Kumalija ("Uhuru" editor), Stanley Kamana, Joe Masanilo, Marcellion Komba and others worked.

You can verify that with people like Kassim Mpenda, director of Information Services at the Ministry of Information and Boradcasting; Jenerali Ulimwengu, Joseph Mapunda, Charles Kizigha, Makwaia wa Kuhenga and others. They all worked with Mwakikagile at the "Daily News," except Makwaia who was still at the Ministry of Information then and where Mwakikagile also once worked (at Maelezo). I also know all those people personally, including those whos died. Also Costa Kumalija and Stanely Kamana worked with Mwakikagile at the "Daily News." So did Philip Ochieng', the Kenyan journalist and political commentator. But he NEVER worked at "Uhuru" or "Mzalendo" or at "The Nationalist."

And Godfrey Mwakikagile did NOT go to the United States in 1977. I KNOW that for a fact. He was already there by then. He left Tanzania in 1972 and by 1977 he had already graduated from college in the United States. In fact his departure from Tanzania was published in the "Daily News" in November 1972 when he left in the first week of that month.

Also the first edition of his book, "Nyerere and Africa: End of an Era," was published in 2002, and the second edition - which I have - in 2005. And he knew Nyerere died in October 1999. In fact, I know that he knew within days after Nyerere died. He was also in toucn with Andrew Nyerere when he was writing this book. His other books contain details about elections in Tanzania since the introduction of multiparty democracy and knew about Mkapa all the way - more than you think he does! One thing about the Internet is that when you post messages, you DON'T KNOW who will be reading them, or exactly whom you are responding to!

I'm also interested in Mwakikagile's works as an author, not in his personal life. Those are private matters. And I'm not really sure if he - or anybody else for that matter - would like to have his contact phone number blasted all over the Internet! That's not what I asked for.

I also know he has a blood cousin (very close relative of his) in New York who is married to the son of a prominent Tanzanian politician but I won't go into that.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…