Malawi wamfikisha mahakamani mwandishi aliyedanganya kufukuzwa kwa balozi wa Tanzania

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Mwandishi wa habari wa Malawi Justice Mponda amefikishwa mahakamani kwa kufungua "kiwanda cha kutunga uongo" kuwa Serikali ya Malawi imemwamuru Balozi wa Tanzania nchini Malawi kuondoka nchini humo ndani ya masaa 48.

Inasemekana mwandishi huyo alikamatwa nyumbani kwake na polisi wenyewe silaha mida saa kumi leo alfajiri na kupelekwa kwenye kituo cha polisi cha Blantyre kwa mahojiano kabla ya kufikishwa mahakamani.


Dogo mwenyewe huyo hapo chini. Ana miaka 27.

Screen-Shot-2012-10-15-at-07.14.42.png
 
Naona kuna wenye hekima wamewatonya kuwa usicheze na Tz watawafix mtaja juta kuitwa Malawi
 
Naona kuna wenye hekima wamewatonya kuwa usicheze na Tz watawafix mtaja juta kuitwa Malawi

Lakini wanasema amekamatwa pia kwa sababu baadhi ya habari ambazo amekuwa akiandika zinatishia usalama wa taifa la Malawi. Mojawapo ni ile aliyoandika kuhusu kujiuzulu kwa Rais wa Malawi.
 
Mpuuzi sana huyu dogo. Analeta habari za uongo uongo kwenye suala sensitive kama hili. Anastahili kuchukuliwa hatua kali na ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo kutaka kuwapotosha watu na kuchonganisha nchi.
 
Asante kwa taarifa.

Huyu Mponda jina lake si geni sana kwa makabila ya Tanzania, kama sijakosea jina kama hilo huenda ni kutokea ukanda wa ziwa Nyasa, au kusini nyanda za juu, la sivyo mikoa ya kati ya Tanzania.

Ukiwa nchi za wenyewe jitahidi kuandika habari kwa uadilifu na ukweli, maana uandishi huu tuliouzoea Tanzania wenzetu wanatushangaa sana.
 
Mponda ni kama majina ya ndugu zangu wangoni au wale wa mwambao wa mbambabay litui manda!
 
Dogo anatolewa kafara tu, viongozi wa Malawi walikurupuka kusema maneno yale aliyonukuu dogo.

Lakini kama wamejirudi ni jambo jema. Tusonge mbele kutafuta muafaka.
 
......Angalau wenzetu wanachukua hatua za uwazi kwa wale wenye ushabiki uliowaziba macho kiasi kwamba hutumia kalamu zao kulenga malengo yao bila kujali madhara ya jamii ......
 
Alec CheMponda wa kule Mlimani usimsahau katika kumbukumbu hizo.

Asante kwa taarifa.

Huyu Mponda jina lake si geni sana kwa makabila ya Tanzania, kama sijakosea jina kama hilo huenda ni kutokea ukanda wa ziwa Nyasa, au kusini nyanda za juu, la sivyo mikoa ya kati ya Tanzania.

Ukiwa nchi za wenyewe jitahidi kuandika habari kwa uadilifu na ukweli, maana uandishi huu tuliouzoea Tanzania wenzetu wanatushangaa sana.
 
Hana gazeti la kufungiwa?

Sidhani kama wataweza kulifungia kwa sababu ni online newspaper. Wenye hiyo site wanalalamika kuwa they have "been receiving constant from government agencies in attempt to close it down."
 
Mwanza cha mtoto maana ilikua kuviziana night kwa night, maneno Nyololo bhana, ndio wajue kuwa askari wetu wanapiga mpaka kamanda wao wenyewe!!! Yaani ni wakali kama mbwa mwitu, maana naskia mbwa mwitu wakiwinda wakila nyama wakimaliza, yule ambaye hatajifuta vizuri anageuzwa kitoweo
Mpwa sio Mwanza?
 
Ktk habari kwenye blog yake alisema pia Balozi wa Tz nchini Malawi Tsere kapewa masaa 48 arudi TZ. Kitu ambacho si kweli maana Serikali ya Malawi imekanusha haijasema suala hilo. Alichohojiwa Tsere na vyombo vya habari mwandishi akakigeuza maana BALOZI TSERE kasema wazi kama MTANZANIA kasoma shule akifundishwa kuwa mpaka ni katikati ya ziwa. Kasema kama malawi wanasoma mpaka ni ufukweni mwa TZ ndiyo maana wanafanya majadiliano kupata muafaka bila kuleta matatizo yoyote.
 
Malawi journalist Justice Mponda has been charged in court for publishing false reports.


Mr Mponda was arrested Monday morning, for among others, reporting that Tanzanian High Commissioner to Malawi Patrick Tsere had been declared persona non grata and ordered to leave Malawi within 48 hours.


He was picked up in the wee hours by heavily armed police officers in an armoured vehicle at his Chiwembe residence in Blantyre. He was taken to Blantyre police station for questioning before being charged in court.

Mr Mponda's articles, according to the Malawi online news website Nyasa Times, stemmed from a fake Facebook account of the President, which he is linked to have been using. One of them, Nyasa Times reported, ''alleged that the Tanzanian diplomat was declared persona non grata and has been required to leave the country following an interview on a local radio, Zodiak''.


Government refuted the story.

By AFRICAREVIEW.COM | Monday, October 15 2012
 
Malawi journalist Justice Mponda has been charged in court for publishing false reports.
Mr Mponda was arrested Monday morning, for among others, reporting that Tanzanian High Commissioner to Malawi Patrick Tsere had been declared persona non grata and ordered to leave Malawi within 48 hours.
He was picked up in the wee hours by heavily armed police officers in an armoured vehicle at his Chiwembe residence in Blantyre.
He was taken to Blantyre police station for questioning before being charged in court.
Mr Mponda's articles, according to the Malawi online news website Nyasa Times, stemmed from a fake Facebook account of the President, which he is linked to have been using.
One of them, Nyasa Times reported, ''alleged that the Tanzanian diplomat was declared persona non grata and has been required to leave the country following an interview on a local radio, Zodiak''.
End
 
Liwe fundisho kwa wanahabari wetu hapa nchini ambao pia wakati fulanifulani hujisahau na 'kuongeza chumvi' kwenye habari zao.
 
Back
Top Bottom