Malawi: Rais Chakwera akosolewa kwa kuteua ndugu kwenye Baraza la Mawaziri

Hii ndiyo Afrika......
Jamani sijui sisi waafrika tuna akili gani......yani umeingia kwa nguvu ya umma alafu unaanza kufanya upuuzi
Trump akimpa kazi Ivanka binti yake kuwa mshauri wake hakuna tatizo kwa vile si mwafrika?
maana huyo binti yumo kwenye watumishi wa Ikulu ya Marekani.

Magufuli akimpa kazi ndugu Dotto inakuwa Afrika ni tatizo ...!!!
 
Nimeshapita Mkuu. Niangalie kwenye post #14 huu upuuzi hata siku moja siwezi kuuafiki.
Naam mkuu yani watu wanaokurupuka kutoa maamuzi mazito sina imani nao. Alikuja kama kaagizwa na timu, kama kama kukomoa mtu au kulipa kisasi. Alifanya kitu kizuri lakini kwa haraka ya kutia shaka. Na hakuna watu sitaki kuwaamini kama hawa walala makanisani, kina Nkurunziza na Taylor wote walikuwa wasoma vifungu.
Mwafrika kuwa mpinzani haimaanishi ndiye mkombozi, muhimu ziwepo sheria na kanuni na zifuatwe. Sasa huyu kaapishwa leo, karekebisha kifungu cha sheria ili kimlinde yeye. Mpaka sasa bado sijui mamlaka ya kubadili vifungu anayo nani katika nchi hiyo, kwingine najua ni bunge au mahakama.
 
Mkuu ndiyo sababu ya umuhimu mkubwa wa kuwepo na uchaguzi huru na wa haki hivyo hata kama Wapinzani WATAVURUNDA basi na wao wawe voted out from power na siyo kung’ang’ania madarakani. Hiyo ndiyo democracy tunayoitaka ili katiba, Bunge na mahakama vyote vipewe HESHIMA inayostahili na siyo kudharauliwa na kuchezewa chezewa.

Naam mkuu yani watu wanaokurupuka kutoa maamuzi mazito sina imani nao. Alikuja kama kaagizwa na timu, kama kama kukomoa mtu au kulipa kisasi. Alifanya kitu kizuri lakini kwa haraka ya kutia shaka. Na hakuna watu sitaki kuwaamini kama hawa walala makanisani, kina Nkurunziza na Taylor wote walikuwa wasoma vifungu.
Mwafrika kuwa mpinzani haimaanishi ndiye mkombozi, muhimu ziwepo sheria na kanuni na zifuatwe. Sasa huyu kaapishwa leo, karekebisha kifungu cha sheria ili kimlinde yeye. Mpaka sasa bado sijui mamlaka ya kubadili vifungu anayo nani katika nchi hiyo, kwingine najua ni bunge au mahakama.
 
Wananchi wa Malawi wameanza vizuri sana kuonyesha ukomavu wa Kidemokrasia lakini wanaangushwa na wanasiasa.

Wanasiasa ni watu kama watu wengine lakini kuna wakati wanajisahau na kujiona kuwa wao ni watu muhimu sana kuliko binadam wengine.
Hii tabia anayo Mbowe; tabia ya kujiona kuwa yeye ndiye Chadema na Chadema ni Mbowe.
Mbowe hana Tofuti na huyo Rais wa Malawi.
Ni tabia za kijinga sana kujenga chama kwenye misingi ya kifamilia.
Hapa Kwetu Tanzania Chadema Chini ya Mbowe ni Chama chenye umri wa miaka 28 lakini Hakuna watu hata watano wanaoweza kushika nafasi ya Uenyekiti zaidi ya Mbowe. Huu ni ujuha. Chama kama hiki kikiingia madarakani hakina uwezo wa kupata Hata mawaziri achilia mbali Havana wa fedha na wakurigenzi wake. Chama kama hiki cha familia ya Mbowe, yaani Chadema hakiwezi kupata Mabalozi ,Wakuu wa mikoa , Mawaziri,Makatibu wa kuu n.k . Hii ni kwa sababu tu ya upuuzi wa mtu Mmoja Mbowe wa kujenga chama kionekane bila yeye kitauzwa na hakuna mtu wa kuaminika.

Yanayotokea nchi jirani yanafundisho kwetu hasa hawa akina Mbowe na wengine ndani ya CCM , wafia vyama badala ya Nchi na Taifa letu.

Afrika tuna matatizo makubwa sana kwenye katiba zetu. Katiba zinazowapa watawala nafasi ya kufanya mambo wanayotaka wao .
Katiba za nchi zetu ni za ajabu sana.
Lakini pia katiba za vyama nazo ni za ajabu sana mfano Katiba ya Chama isiyo na ukomo katika uongozi wa nafasi ya Uenyekiti wakati huo huo katibu wake anateuliwa tu na Mwenyekiti na kuondolewa hata kesho asubuhi bila kuulizwa na mtu.
Demokrasia za Afrika zimelenga kuwapa nguvu ,madaraka makubwa ,ufahari na Uhuru mkubwa sana wanasiasa tuu huku wananchi wakiishi kama watumwa wao.

Wapinzani wa Tanzania mjifunze na kujipanga huku mkiwa na uwezo wa kuwapinga wapotoshaji na walaghai ,wahuni na walevi kama Mbowe.

Mwongeze Mwenyekiti wa Chadema Konyagi!
 
Rais mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera amekosolewa kwa kuteua Baraza la Mawaziri linalojumuisha Mtu na Mke wake pamoja na watu wengine ambao ni ndugu

Sidik Mia, ambaye ni Mgombea mwenza wa Rais huyo katika Uchaguzi wa mwaka 2019 amechaguliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi huku mke wake, Abida Mia akiwa Naibu Waziri wa Ardhi

Kenny Kandodo ni Waziri mpya wa Kazi huku dada yake, Khumbize Kandodo akiwa ni Waziri mpya wa Afya. Mfanyabiashara Gospel Kazako amekuwa Waziri wa Habari huku Shemeji yake, Agnes Nkusa Nkhoma akiwa Naibu Waziri wa Kilimo

Baadhi ya Wakosoaji wameshangazwa na Baraza hilo kwani Rais Chakwera amefanya kile ambacho aliwahi kumkosoa nacho aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika kuhusu upendeleo na kuteua watu kutoka mkoani kwake

Wameongeza kuwa zaidi ya asilimia 79 ya Baraza jipya la Mawaziri wanatokea Mkoa wa Kati ambapo Rais Chakwera anawafuasi wengi
Yani nimekumbuka ile picha ya the last King of scotland, pale ambapo Idd Amina anawahutubia watu wanafurahi, kale kamzungu kakawwa aknamwambia yule mama mke wa mchungajikuwa inaelekea jamaa ni mtu mzuri na watu wanampenda sana.
Mama akakajibu kuwa Afrika kila uongozi mpya huanza kwa kushangiliwa ila baadae mambo uwa tofauti.
 
Rais mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera amekosolewa kwa kuteua Baraza la Mawaziri linalojumuisha Mtu na Mke wake pamoja na watu wengine ambao ni ndugu

Sidik Mia, ambaye ni Mgombea mwenza wa Rais huyo katika Uchaguzi wa mwaka 2019 amechaguliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi huku mke wake, Abida Mia akiwa Naibu Waziri wa Ardhi

Kenny Kandodo ni Waziri mpya wa Kazi huku dada yake, Khumbize Kandodo akiwa ni Waziri mpya wa Afya. Mfanyabiashara Gospel Kazako amekuwa Waziri wa Habari huku Shemeji yake, Agnes Nkusa Nkhoma akiwa Naibu Waziri wa Kilimo

Baadhi ya Wakosoaji wameshangazwa na Baraza hilo kwani Rais Chakwera amefanya kile ambacho aliwahi kumkosoa nacho aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika kuhusu upendeleo na kuteua watu kutoka mkoani kwake

Wameongeza kuwa zaidi ya asilimia 79 ya Baraza jipya la Mawaziri wanatokea Mkoa wa Kati ambapo Rais Chakwera anawafuasi wengi
Mambo mengi africa hukwamishwa na uduni wa katiba zetu kwa nchi ya malawi cheo cha uraisi huchukuliwa kama cheo cha uchifu ni tofauti kidogo na siasa za east africa hasa Tanzania na Kenya Wamalawi hawajali sana teuzi wao wanaangalia utendaji wa mteule
 
Muhimu wawe na sifa na wafanye baaasi ila wakianza kuwa kama chadema walivyogeana nafasi pale chamani ndio shida.

Sio kama sisiemu na sera ya hakuna kanda ya kaskazini katika jambo lolote kwenye serikali na uongozi wowote wa maana jamaa kawapa kama sio ssem basi ni kanda ya kule kwetu kuule
 
Kavurunda huyu kuchagua ndugu kama kaka na dada. Pamoja na hao ndugu yeye binafsi hawamuhusu lakini KAVURUNDA sana.
Hahaha nilishangaa sana nilipoona CHADEMA wanampongeza kwa kushinda, nikauliza ikiwa majimbo yaliyo chini ya CHADEMA yakirudi ccm watapongeza pia?! Yani KANU kenya irudi madarakani CHADEMA inapongeza?!

Sasa ndiyo muone vyama tawala vikipotea vikarudi vinakuwaje.

Nchi nzima wapinzani atamteua nani asipomteua mke na shemeji zake?!
 
Ndiyo shida ya kuchagua upinzani. Watakoma. Huku sie ni ccm milele
 
Watanzania kweli Ni akili Hakuna kichwani Sasa hapo kosa liko wapi ?

Ukisoma comments utajua kwanini watanzania wengi uwezo wao wa kureason uko chini Sana ...

Kwanza hajateua ndugu zake. Wote alioteua ni wabunge wana sifa za kuwa mawaziri Sasa hapo kosa linatokea wapi ...

Ni sawa na pale Bungeni magufuli angemteua Riziwani Kikwete na Mama Salma Kikwete Wawe mawaziri halafu mijitu iseme haiwezekan eti ameteua ndugu.

Halima Bulembo na Baba Yake Mzee Bulembo wote ni wabunge na wana sifa za kuteuliwa kuwa mawaziri. Wakiteuliwa kuwa mawaziri mtasema eti hawapaswi kuteuliwa kisa Ni ndugu ???
 
Uwe unasoma kwa kituo. Hao ndugu aliowateua yeye hawamuhusu na pia Chadema kumpongeza kwa ushindi wake hakuna kosa lolote lile na akivurunda pia atapewa za uso na si Chadema tu bali vyama vyote duniani vyenye kuheshimu na kuthamini utawala BORA.

Hahaha nilishangaa sana nilipoona CHADEMA wanampongeza kwa kushinda, nikauliza ikiwa majimbo yaliyo chini ya CHADEMA yakirudi ccm watapongeza pia?! Yani KANU kenya irudi madarakani CHADEMA inapongeza?!

Sasa ndiyo muone vyama tawala vikipotea vikarudi vinakuwaje.

Nchi nzima wapinzani atamteua nani asipomteua mke na shemeji zake?!
 
Nani alikwambia hawa ni wapinzani? Walikuwa ndiyo chama tawala na kushindwa miaka 26 iliyopita hivyo wamerudi tena madarakani.

Ndiyo shida ya kuchagua upinzani. Watakoma. Huku sie ni ccm milele
 
Kakosa kabisa umakini na kufanya upuuzi mkubwa!
Kuna Mtu Mmoja aliwahi kuniambia Mzukulu kuwa Waafrika wengi ni Watu wa Kupenda sana Mabadiliko na Ujio wa Vyama vingi katika Kushika Dola za nchi zetu hizi ila hapo hapo Waafrika tumesahau kwamba tabia zetu za Kiafrika zinafanana hata kama tutakuwa tunampenda na Kumuamini Mtu fulani kutokea upande tuupendao na kuuchukia ule atokao.

Ni kwamba katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa na ambayo pia imepelekea hata Wananchi wa Malawi ambao walimpigia Kura sasa Kujutia Kumuweka Madarakani Rais Mteule wa Malawi Mwinjilisti Lazarus Chakwera ameanza Mazingaombwe yake na Upuuzi wake kwa Kuteua Baraza la Mawaziri ambalo humo humo lina Ndugu na Mashemeji ikiashiria anatanguliza Undugu Serikalini.

Kwa kuanzia tu ameteua Waziri wa Kazi na wa Afya ambao wote Wawili ni Ndugu moja kwa Baba na Mama. Kuona hiyo haitoshi Kateua Waziri wake mpya wa Habari ambaye kumbe nae ni Shemeji wa Naibu Waziri wa Kilimo. Na kwa Kumalizia Upuuzi wake Rais huyu Kateua tena Waziri wa Usafirishaji ambaye tena ni Mume wa Naibu Waziri wa Ardhi.

Ndiyo maana kuna muda Mzukulu huwa nasema ni kheri tu nchi za Afrika ziendelee Kuongozwa na Marais Wakongwe kuliko Wapuuzi kama hawa.

Kwa anayetaka Taarifa hii Kamili ipo katika Gazeti la Mtandao la The Citizen.
 
Back
Top Bottom