Swali kwa Mnyika:
Mkuu, wewe ni msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni katika kamati ya Nishati na Madini; hebu FUNGUKA; Tanzania haina tishio la mgao wa umeme?
Nikiisoma hotuba yako bungeni (ref. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nzani-wizara-ya-nishati-na-madini-2012-a.html ) napata shaka kuwa tunakoelelea si kuzuri. Labda tutarajie Bil 357 zilizotolewa na Ujerumani kwa Tz ndizo zitatuokoa? Ref. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...mani-yaisaidia-tanzania-sh-bilioni-357-a.html
Mnyika ni Jembe linalolima mpaka lami..Fina kamchomekea swali la kama anampango au maono ya kuutaka urais iwapo katiba itabadilishwa na umri kumruhusu.
Amelijibu kikomavu sana..anasema kwa sasa kipaumbele chake ni wana Ubungo na kuhakikisha Chadema inashika dola 2015.
Jembe Mnyika anatisha..ni kijana asiyekurupuka,asiyeropoka,asiye na tamaa wala majivuno,amejaa maono na kabeba matumaini ya vijana wa TZ,anajua taifa linataka nini...kwa kweli ukikaa chini kumsikiliza unapata picha ya kiongozi shupavu na mstaharabu..ni full package ya kiongozi tunaemtaka sisi kama vijana wa kitanzania..
Kamaliza interview,na ameifanya siku yangu kuwa supa,
ngojea nijipange nikale bata sasa...wazee wa bata leo nitakuwa Seanage Lounge Oyerstabay kwenye the Legend iz Back na Dj John Dilinga..ukiwa pale si vibaya ukani PM tufahamiane.