A
Anonymous
Guest
KERO: MATUMIZI MABAYA YA MAKUNDI YA WHATSAPP WILAYANI SIHA
Mimi ni mkazi wa Wilaya ya Siha. Nina kero kuhusu uwepo wa makundi ya WhatsApp yanayotambulika kwa majina ya Siha Development, Siha Unity na Sauti ya Siha. Makundi haya ambayo awali yalikuwa yakitumika kujadili maendeleo ya wananchi, kuhimiza umoja na kutoa nafasi kwa wananchi kutoa maoni yao, kwa sasa yamegeuzwa na baadhi ya watu kuwa sehemu ya kudhalilisha, kubeza, kutukana, kushusha heshima za watu na kukiuka maadili pamoja na sheria za nchi.
Kwa kipindi kirefu, makundi haya yalikuwa na mchango mkubwa katika kujadili hoja za msingi na kutatua kero za wananchi. Hata hivyo, hivi sasa yamekuwa yakitumika kujadili maisha binafsi ya watu, hususan viongozi wa kisiasa, viongozi wa kijamii pamoja na watumishi wa umma. Baadhi ya wanachama wamekuwa wakitumia majukwaa hayo kueneza chuki, kudhalilisha watu na kutweza utu wa watu wengine.
Aidha, kumekuwa na vitendo vya baadhi ya wanachama kuweka hadharani ujumbe wa faragha kwa njia ya “screenshots” na kuzisambaza kwenye makundi hayo kinyume na sheria za Tanzania pamoja na maadili ya jamii yetu. Lengo la vitendo hivyo limekuwa ni kuwachafua, kuwavunjia heshima na kuwaumiza watu mbele ya jamii.
Ni muhimu kutambua kuwa kila mtu ana haki ya kulindwa utu, heshima na faragha yake kwa mujibu wa sheria za nchi. Hakuna mtu mwenye haki ya kutumia mitandao ya kijamii kumdhalilisha mwenzake au kuvamia maisha yake binafsi. Watu wanaoficha utambulisho wao na kutumia majina ya kificho kufanya vitendo hivyo wanapaswa kutambua kuwa kufanya uhalifu kwa kujificha hakuwafanyi kuwa salama mbele ya sheria.
Aidha, haki ya mtu mmoja huishia pale haki ya mwenzake inapoanzia. Uhuru wa kutoa maoni haupaswi kutumiwa kama njia ya kutukana, kudhalilisha, kutengeneza chuki au kuvunja sheria za nchi. Inasikitisha kuona baadhi ya watu wakifanya vitendo hivyo kwa kujiamini kana kwamba wameweka serikali na vyombo vya dola mfukoni mwao na hawawezi kuchukuliwa hatua.
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba viongozi wa makundi hayo wamekuwa hawachukui hatua zozote kuzuia vitendo hivyo, jambo linalozua hisia kuwa baadhi yao wanatoa ushirikiano au kunufaika na hali hiyo. Wakati huo huo, makundi hayo yanajumuisha viongozi mbalimbali wa kisiasa, kijamii na hata wa serikali ambao wanaendelea kushuhudia hali hiyo bila kuchukua hatua madhubuti za kukemea.
Imefikia hatua baadhi ya wananchi husubiri kuona nani atakayefuata kudhalilishwa kwenye makundi hayo. Vilevile, kuna tuhuma kuwa baadhi ya watu huwatumia wanachama fulani kwa kuwapa fedha ili kuwachafua au kuwadhalilisha mahasimu wao. Pia, yapo madai kuwa baadhi ya watu wanaotumia majina ya kificho huwatishia watu kuwa watawaandikia taarifa za kuwachafua endapo hawatatoa fedha.
Kutokana na hali hiyo, naiomba Jeshi la Polisi pamoja na TAKUKURU kuchunguza na kuwachukulia hatua watu wote wanaohusika na vitendo hivyo vya ukiukwaji wa sheria na maadili ya matumizi ya mitandao ya kijamii.
Vilevile, naiomba jamii ya wananchi wa Siha kusimama pamoja katika kulinda maadili ya Kitanzania, kuheshimiana na kutumia majukwaa ya kijamii kwa kujadili hoja za maendeleo badala ya kushambulia maisha binafsi ya watu. Tusimwache peke yake Dorothy Gwajima katika kukemea mmomonyoko wa maadili. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha utu wa watu unaheshimiwa na sheria za makosa ya mtandao zinazingatiwa.