McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,089
- 3,444
Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, imeanza kufuatilia kwa kina malalamiko ya wananchi kuhusu matangazo ya huduma za massage yanayosambazwa mitandaoni, hususan Instagram.
Waziri Dkt. Dorothy Gwajima ameeleza kuwa hatua hiyo inakuja baada ya kubainika kuwa baadhi ya matangazo hayo yanachochea mmomonyoko wa maadili na hayazingatii utamaduni na misingi ya Kitanzania.
Dkt. Gwajima amebainisha kuwa Serikali itafanya uchunguzi wa kina ili kubaini usajili wa vituo hivyo pamoja na uhalali wa maudhui wanayochapisha kwa mujibu wa sheria na kanuni za maadili.
Licha ya Waziri kukiri kutoyaona matangazo hayo moja kwa moja kwenye kurasa zake, amewapongeza wananchi kwa kuendelea kuwasilisha vielelezo na ushahidi wa picha na video ambao utasaidia katika hatua za kisheria zinazofuata.
Aidha, Serikali imetoa onyo kali kuwa haitasita kuvifunga vituo na kuwafungulia mashtaka wahusika wote watakaobainika kukiuka taratibu, ikirejea hatua kali zilizowahi kuchukuliwa hapo awali.
Wananchi wamehimizwa kuendelea kuwa walinzi wa maadili kwa kuhifadhi na kutoa ushahidi wa matangazo yoyote yanayokiuka utu na heshima ya jamii ili kudumisha nidhamu na utulivu ndani ya nchi.