Tetesi: Makundi MANNE ya URAIS 2025

Tetesi: Makundi MANNE ya URAIS 2025

Griss

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2025
Posts
337
Reaction score
1,945
Wasalaam!!

1: Kundi la kwanza ni kundi la pure wazalendo wa nchini lenye ushawishi ni kundi linaloongozwa na Tundu Lissu,John Heche, Lema na umma wa wapenda mabadiliko ya kweli, Hawa ni wale ambao hawajawai kuwa serikalini lakini serikali wanaijua nje ndani na uozo wao wote na wakiingia wataleta mabadiliko ya kweli ya kikatiba na kisheria na kujenga uchumi shirikishi.

2: Kundi la Pili ni linalo-ongozwa na wazalendo ndani ya CCM waliochoshwa na kuporwa kwa rasilimali za Taifa ambao ni Warioba, Butiku, Mwinyi, Polepole, Dr bashiru, Majaliwa, Pinda,Mpango, Mpina na Gwajima.

3.Kundi la tatu ni CCM maslahi ya ambao ni Rostam Azziz, Nchimbi, Kigwangala, Makamba,Bashe na Nape, Ndungai, Kinana. Hawa ni masalia ya wanamtandao na watumishi wa mtu sio wananchi.

4. Kundi la nne kundi maslahi pia, ndio kundi la wanamtandao JK,Samia,Riz, Muchengerwa, Rajabu, Abood, Msukuma, Shabibi, Mavunde,Mwigulu, Zitto na Mbowe hili ndio kundi hatari zaidi kuwai kuwepo nchi hii.

Namba moja na namba mbili wanaongea lugha moja ingawa wapo pande mbili tofauti.

Namba nne ni matokeo ya ugomvi wa kimaslahi na namba tatu.

Wazalendo tupambane baada ya Reform mpaka kieleweke ili namba 1 na 2 waingie kwenye uchaguzi ili akishinda yeyote nchi inakuwa imeshinda.

Mungu ibariki TANZANIA.
 
Walinda mipaka Wana wa sapoti kundi lipi!!?hao ndio wanaweza kutusaidia kuliko maneno matupu ya wanasiasa!!

Tunataka kuona wakionyesha msimamo wao!

Kwa muda mrefu wamenikera sana!!hasa kujifanya ya wanasiasa hayawahusu wakati nchi wanayoilinda inaharibiwa vibaya sana!!

Kama wangekua active ufisadi na mengineyo yasingekuwepo kabisa!

Unalindaje mipaka wakati ndani unawaacha wezi waibe vya kutosha!!!!?

Time to step up!
 
Basi nikajuaga bwana sabufa ni muumini wa namba 2.
 
Kati ya makundi hayo in Nani walizima mtandao yote ya kijamii wakati Polepole anaongea na wananchi?
 
Kundi la kwanza ni kundi la pure wazalendo wa nchini lenye ushawishi ni kundi linaloongozwa na Tundu Lissu,John Heche, Lema na umma wa wapenda mabadiliko ya kweli, Hawa ni wale ambao hawajawai kuwa serikalini lakini serikali wanaijua nje ndani na uozo wao wote na wakiingia wataleta mabadiliko ya kweli ya kikatiba na kisheria na kujenga uchumi shirikishi.
Nimeishia hapa.
Asante sana DJ
 
Hii nchi watu wengi wanaojielewa sana hawang'ang'anii siasa mi nashangaa mwenyekiti wa kijiji ni maskini wa kutupwa ila anaongoza watu sasa najiuliza yeye maisha yake yamemshinda je atayaweza ya watu na diwani wa kata kaachishwa kazi selikarini sababu ya uharibifu wa fedha za umma je uongozini si ataharibu vya kutosha
 
Hivi ni kweli Roast na jamaa ake wa ujanani ni mahasimu kwasasa?
 
Namba 1. Hawajawahi kupata nafasi ya kuongoza hivyo kusema wataleta mabadiliko ya kweli ya kikatiba ni nadharia tu. Wanaweza wakaleta au wasilete. Huwa haiwi mpaka iwe.
 
Back
Top Bottom