Makubwa haya nayo

Mbona hii imekaa kinegative sana, au jamaa anaoa kwa shingo upande?? Dah.....inatia wasiwasi kwa kweli!!
 
bwana harusi alikua kachomoa, kuchelewa ilisababishwa na vikao vya kumshawishi.
 
Nahisi huyo Bwana harusi mtarajiwa ana mahusiano au amesababisha mimba nje ya huyo mkewe mtarajiwa kwa hiyo siku ya 'send off' alienda kusuluhisha yeye na hao ndugu zake, haiingii akilini wote kuwa hawapatikani kwa simu.
 
Lol! Chasing a man is a serious bt useless business! Dada ataandika kitabu,manake baba huyo ataharibikiwa na gari ijumaa jioni litengemae jumapili mchana ndo arudi home.
 
Habari za asubuhi mabibi na mabwana.poleni na hongereni kwa kazi.

Jana nimehudhuria Send Off ya ndugu yangu.sherehe ilipangwa kuanza saa kumi na mbili na nusu jioni .lakini tuli lazimika kuanza sherehe saa nne na nusu usuku baada ya bw harusi mtarajiwa na wajumbe wake kuchelewa kufika ukumbini.wageni hao pia walikuwa hawapatikani katika simu zao.ikawa patashika kwa ndugu wa bi harusi na bi harusi mwenyewe.mpaka make- ups zilianza kufutika kwa machozi.
cha kushangaza wageni walipofika walisema kuwa gari liliharibika njiani sasa nikajiuliza.
-kutoka kimara mpaka mbezi beach siyo porini kwanini usitafute usafiri mwingine hata bajaj kwa muhusika mkuu afike?
-wageni wote hawakutumia gari moja kwanini wasije wachache kwanza ukumbini.


kwakweli tulijisikia vibaya sana.uzembe gani huo na disorganisation kwa kijana anayetarajia kutunza family.


This is africa, simple answers to critical questions!!!
 
From Kimara to Mbezi Beach
Hilo Foleni lake .... Shukuru Mungu alifika maana mi nisingekuja kabisa
 
Ni kukosa uungwana na ustaarabu. Pia ni indicator kuwa huendi ndg hawamkubali sana bi harusi.
 
I cant imagine kichwa cha bibi harusi kilivyoenda resi...pole zake kwa kuchagua hicho kimeo...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom