Kiprotokali ni Rais ndiye alitakiwa atangaze kupokea barua ya Emmanuel Nchimbi kujiuzulu umakamo wa Rais na siyo Nchimbi kutangaza kuwa amemuandikia Rais barua ya kujiuzulu.
Hili kosa la Kiprotokali alilifanya pia Edward Lowassa alipojiuzulu uwaziri Mkuu toka kwenye Serikali ya Jakaya Kikwete.
Mkuu Aleni,
Allen Kilewella
Kwanza naunga mkono hoja,
Ukiteuliwa ni unateuliwa kwa barua, hivyo ukijiuluunaandika kwa mamlaka yako ya uteuzi kuomba ruhusa ya kujiuzulu.
Barua ya kukuruhusu ikiisha kujibiwa kuwa ombi lako la kujiuzulu limekubaliwa, ndipo sasa mamlaka yako ya uteuzi itatoa taarifa kwa umma kuwa Mhe rais amepokea barua ya ombi la kujiuzulu, ameridhia, na baada ya hapo ndio wewe unaweza kutoa taarifa yako kwa umma.
Kilichotokea ni VP aliwekwa Kiti Moto na kikao cha NEC akalazinishwa kujiuzulu, akagoma.
Akaandikiwa barua ya mashitaka kuhudhuria mashitaka kuhudhuria kamati ya maadili, akagoma, akijua analindwa na katiba ya JMT, rais na VP wana kinga ya kikatiba ya kutokushitakiwa na mamlaka yoyote ndani ya JMT.
Kikao cha maadili kikatoa mapendekezo yake in absentia, kuamua kumfuta uanachama, kikakabidhi kwa Secretariat, hoja ikaingizwa kwenye CC, ikapita, ikatishwa NEC kubariki
Kabla NEC haijakaa kumfukuza, yeye akatangulia kumwandikia barua mamlaka yake ya uteuzi kuomba ruhusa ya kujiuzulu.
Mamlaka yake ya uteuzi ikala kobiz ili isubiri kumtimua, ndipo yeye alipoona kimya na NEC imeitishwa, akaamua yeye kutoa taarifa kwa umma kuwa umemuandikia rais barua ya kujiuzulu. Kitendo hiki ni kinyume na protocol, ila kimesaidia, Ikulu ikatoa taarifa ya rais kukubali ombi lake la kujiuzulu.
Hata hivyo licha ya kujiuzulu mwenyewe bado NEC ya CCM wakamfukuza kwa kujifurahisha, CCM ina mamlaka ya kumfuta uanachama mwanachama wake yeyote lakini haina mamlaka ya kumuondoa VP wa JMT, hivyo licha ya kufutiwa uanachama wa CCM, Dr Nchimbi ni makamu rais mstaafu ana haki zake zote za mafao ya kustaafu na haki pia ya the right to privacy ikiwemo kuamua kutulia na kujinyamazia kimya.
https://www.jamiiforums.com/threads...-iwe-rais-amepokea-taarifa-ameridhia.2466606/
P