SoC02 Makosa ni Yangu

Stories of Change - 2022 Competition

Ibika

New Member
Sep 14, 2022
1
2
Makosa ni Yangu

Majira ya kiangazi nchi Tanzania katika viunga vya jiji la kitalii Arusha ,Nikiwa katika mitaa ya Njiro ambako wenyeji wanapaita ni mitaa ya kishua nami nikiwa nimekaa katika kibaraza cha mzee wa kipemba nikipigwa na vumbi ambalo tunaishi nalo kila siku maana barabara za mtaani kuwa na lami ni ndoto inayosadikika naamua kupita pita mitandaoni na habari kubwa inayogonga vichwa vya habari vingi na kuleta gumzo ni juu ya wawekazaji wa JATU PLC kuwa hawajalipwa hela baada ya kuwekeza .

Moja ya vitu ambavyo vinanichukua akili ni tangazo la waziri wa kilimo kupitia ukurusa wake wa twiter nikimnukuu. “Naomba niwataarifu wakulima walioleta Malalimiko yao kuhusu JATU PLC kuwa team ya Wizara imekamilisha kazi yake, ripoti itakabidhiwa kwenye vyombo vya dola wiki hii kwa hatua zaidi”.

Kwangu mimi nazidi kujiuliza ni makosa yanani? tumefikaje hapa? nani wakulaumiwa ?nani wakuchukuliwa hatua? mbona kumekuwa na malamiko mengi juu ya uwekazaji katika namna mbalimbali.

Labda nikurudishe nyuma kidogo inawezekana tunakuwa wepesi wa kusau ,Tunakumbuka ile hadithi ya Mr Kuku 2020 aaah tuache nasikia amerudi kivingine sasahivi anasema anakuakishia faida ya 10% kwa mwezi yani faida ya asilimia 120% kwa mwaka.

Duuh! mbona wakinamama wanaofuga kuku kule Salasala hawajawa mamilionea hadi leo? nataka nikwambie kuwa hata ukiwekeza Bank, UTT au kwenye Hati fungani huwezi pata faida ya 10% kwa mwezi, Je ndipo hapo waziri anasema tunatakiwa tujiridhishe kwanza ?au ni makossa yetu kutokujua nini maana ya uwekezaji na tunapotoshwa na hadithi za mitandaoni kwa kuona mafaniko ni kazi ya uwekezaji asubuhi na jioni ni wakati wa kuvuna mamilioni.

Hiyo inaweza kuwa ya juzi sana wacha nikurudishe nyuma tena kidogo unakumbuka ile biashara ya Q-net, Ahh! nasikia wale walimu hawajanunua magari yao mpaka leo .Mwisho si haba nimalizie kwa kukupelaka kwenye ile hadithi ya upatu na kampuni ya DESI ambapo watu walikuwa wanapanda hela wakisubiri kuvuna utazani ni shamba la karanga .

Inawezekana siifahamu bibilia vizuri lakini ule mstari wa mwana mwenye hekima humfurahisha babaye na mwana mpumbavu ni mzigo kwa mamaye, naona unamaana zaidi kweli Maisha yanaenda kasi sana tulipofika si tulikotoka ,Tunakoenda si tukujuapo maana tulipo jikwaa hatukung’oa kisiki bado tunaendelea kujifuta mavumbi. Mimi si mtwana wa maneno bali jabali wa maarifa, ili tuweze kujua tulipo jikwaa acha tusiwe na taswiswii tuchukue mfano wa JATU PLC kama somo letu kwa ufupi.

JATU PLC(Jenga Afya Tokomeza Umasikini) mnamo mwishoni mwa mwaka wa 2020 kampuni hii ilinza kugonga vichwa vya habari hasa zile za biashara baada ya kutaka kuuza hisa zake katika soko la hisa la Dar es Salaam, Yani kwa kwa lugha ya darasa la nne B pale shule ya msingi Mabonde ,Kampuni hii ilikuwa inatoka kuwa kampuni binafsi na kuwa kampuni ya umma, Hii ilikuwa ni habari kubwa kwa sababu soko letu la hisa yani DSE ni soko changa likiwa limeanzishwa 1998 tu , Pia kutazama idadi ya makampuni ambapo mpaka naandika maakala hii soko hili lina jumla ya kampuni 28 huku kampuni za ndani zikiwa 22 tuu, Lakini mtaji wa jumla wa soko hili bado ni mdogo sana ambapo mpaka 29/08/2022 inajumla ya wastani wa Tsh Trilioni 15.8 (29/08/2022) .

Mwisho inadi ya wawekezaji katika soko la hisa la Dar es Salaam ni chini ya million moja ambapo uwekezaji mkubwa zaidi ni kutoka nje ya nchi. Kwa hiyo kuongezeka kwa kampuni mpya ilikuwa ni habari kubwa kwani inakwenda kupanua zaidi wigo wa uwekezaji katika soko la hisa na kama vile falsa ya fedha inavyosema pale ambapo kunakuwa na kapu lenye bidhaa tofauti za uwekezaji basi ndipo viashiria vya hatari ya uwekezaji vinapungua.

Naomba utambue katika soko la hisa kuna kampuni zinaingia moja kwa moja kwenye soko kuu la uwekezaji na nyingine zinaingia kupitia programu maalumu ya Endeleza.

JATU PLC kama kampuni nyingine ilikizi vigezo vyote, Ambapo yenyewe ilingia kupitia dirisha la pili la Endeleza Programu yani ambapo makampuni machanga na ya kati ambayo yana hatari kubwa kutokana na kutokuwa na takwimu za kuridhisha, hupita na kuandaliwa ili yaweze kukizi vigezo vya kuingia katika soko la hisa, lakini pia ilikuwa na sifa ya ziada moja wapo hii kampuni haikuanzia katika hatua za awali za kuingia DSE ambazo ni IPO kama ilivyofanya kampuni ya Vodacom mnamo mwaka 2017.

IPO kwa tafsiri isiyo sahii sana inamaanisha kuwa Ni toleo la awali kwa umma, Nikifafanua hapo ni wakati ambapo kampuni inakuwa inauza hisa zake kwa mara ya kwanza kwa umma, Kabla haijaingia kwenye soko la hisa, Sasa hapo utagundua kuwa Kampuni ya JATU PLC ilingia kwenye soko la hisa mnamo tarehe Novemba 23, 2020, kwa mara ya kwanza ambapo hisa zilizokuzimelipwa ni 2,164,349 zikiwa na thamani ya Tsh1.08 bilioni. kwa sababu teyari ilikuwa na wanachama Zaidi ya 200.

Kutokana na idadi ya hisa za JATU PLC kuwa chache sokono, hii ilipelekea thamani yake kupanda kwa haraka sana na zilikuwa na uhitaji mkubwa sana sokono, JATU PLC wakaona wauze hisa kwa umma kwa sababu walikuwa na hisa chache sokoni ambazo zilikuwa zinapandisha thamani zaidi ya kampuni kutoka kwenye thamani halisi .Ikafuatiwa na Tangazo la tarehe 31 Mei 2021.

Hapa JATU PLC walikuwa wanalenga kupata mtaji Tsh 7.5 Billion ambao ungewawezesha Zaidi kufikia malengo yao ya uwekezaji katika kilimo na mnyororo wake wote wa thamani, Mpenzi msomaji mpaka tunafika hapa kumbuka hii kampuni ilikuwa na miaka mitatu tuu.

Huku faida yake kuanzia mwaka 2017, 2018 hadi 2019 ilikuwa kama ifuatavyo Tsh 6,325,770 kisha Tsh 15,985,735 ,kisha Tsh 40,088,024 na mwisho Tsh 97,409,952 hii inaonyesha faida yao haikuwa haba ilikuwa inaongezeka kila mwaka ingawa ni faida ndogo sana kwa kampuni ambayo imeorodheshwa kwenye soko la hisa ,maana hii ni sawa na faida ya mangi pale kariakoo.

Wakati huhohuo jambo la kukumbuka na muhimu zaidi ni kuwa JATU PLC walikuwa na jumla ya hisa 250,000,000 huku hisa za awali zikigawanywa mara mbili kutoka hisa 2,164,349 mpaka hisa 4,328,698 alafu JATU PLC ikauza hisa 15,000,000 maana yake JATU PLC ilikuwa inabakiwa na hisa ambazo hazijauzwa kuwa ni 230,671,302.

Hii inamaana kubwa sana yani mlinganyo wa mtaji na thamani ya hisa hazikuwa zinalingana, JATU PLC bado hawakuwa na thamani halisi ndomaana waliingia sokoni kupitia Endeleza programu kwa sababu kulikuwa na viashiria vingi vya hatari ingawa wakiwa na matarajio chanya, Kwa kumalizia hili utaona kila kitu JATU PLC walifanya kwa mujibu wa sheria huku wakifwata taratibu zote .

Kitu ambacho napenda tuzungumzie ni modali ya JATU PLC katika kufanya kazi naomba ujue JATU PLC ilikuwa inaendesha shughuli zake kwa niaba ya wanachama wake yani kwamfano mkulima anataka kulima JATU PLC ilikuwa inalima kwa niaba yake kisha inaondoa garama zote baaadaye wanagawana faida na mkulima, huu mfumo uliendelea pia baada ya JATU PLC kuingia kwenye soko la hisa.

Sasa changamoto iliyotokea nikuwa hawa watu ambao walikuwa wanatoa hela kwenda kwa JATU PLC ili iweze kuwafanyia uwekezejaji na mwisho wao kuweza kupata faida kupitia huo uwekezaji ,Hawajaweza kulipwa hela zao na hivyo kupelekea serikali kuchukua hatua ilizozichukua hadi sasa. Swali la kujiuliza ni nani mwenye kosa mpaka hapo,Je JATU PLC walikuwa na uwezo wa kutekeleza huo mfumo ?, Mfano tuchukue wawekezaji kwa ujumla wao walitaka kulimia hekari laki tano, Je kwa kutazama mtaji wa JATU PLC ulikuwa toshelevu kuwezesha hilo?

Tutagundua wenye makosa mpaka sasa ni sisi wawekezaji ,Kwanini? kwa sababu tunawekeza kwa kufuata Tamaa ya faida ,Hisia na Msukumo wa Makundi.Pia swali ni mamlaka husika nazo huwa zinakuwa wapi kushindwa kuchukua hatua mapema kabla maafa haya hayajatokea.

Kwa kumalizia nataka niseme kuwa sisi kama watanzania tunawajibu wa kukuza na kuendeleza biashara zetu zile zinafuta sheria na taratibu hata kama zinachangamoto kwa sababu kupitia biashara hizi ndipo ndoto na maono ya vizazi vijavyo zinazaliwa.
 
Attachments

  • Makosa Ni Yangu (1).docx
    25.8 KB · Views: 10

Yametimia.

Mkurugenzi mtendaji yupo ndani sasa!

9599b44b-6064-41e6-861b-9893cd156d81.jpg

34edb3ca-ae49-444d-b2c8-83aed0be49ed.jpg
 
Back
Top Bottom