Makosa 10 aliyotenda Mungu


Naona kama majibu yako yana utata pia mfano namba 2. Mungu yupo kila sehemu mpaka hapo alipo mleta mada halafu hapo hapo unasema Mungu hakai karibu au walipo wadhambi!!!!!!!
 
Mkuu hata mi ni msabath ila kuna wakati namuachia tu Mungu kwasababu kuna maswal hayajibiki na binadam
 
Unajua mi ni mfia dini, ila jibu lako linanipa ukakasi.
Mkuu hata kabla ya kusoma hiyo post yako nimejikuta nacheka sana...hata kama tunaamini, bado tuna haki ya kuuliza.
 
Tanzania nchi huru kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake na akiamua kujamba ana jamba wakati wote.
Mleta mada umejamba sana, tena sii kidogo.
Uwe na uwoga hata robo
Uwoga hata robo???Mbona maandiko yanasema usiogope???...ina maana unapingana nayo???
 
Kwa nini Mungu alimuumba shetani.
Jibu la kisiasa. Yeye ni Mungu muumbaji. Ameumba vingi tu.

Kama maelezo ya kisiasa ya biblia uliyotumia kusema Mungu alimuumba shetani. Jibu ni kuwa shetani alikuwa Lucifer. Malaika mkuu. Alikuwa na sauti nyingi.
Alikuwa mkuu sana.
Alitamani kuwa mkuu kama aliyemuumba.
Akawashawishi malaika wenzake kuwa Mungu si mwenye haki. Wakapanga mapinduzi ila mapinduzi yakashindwa. Simulizi uliyonukuu inaeleza wakaadhibiwa kwa kutolewa huko palikokuwa makazi yao. Ila bado nguvu walikuwa nazo. Mungu akaona haitoshi aliwaacha waranderande. Sasa binadamu hawa waasi wakatushawishi tuendelee kuenda kinyume na mamlaka ya iliyotuweka.
Simulizi inaeleza kuwa by default tunakuwa sehemu ya vita hii ya haki baada ya babu yetu kushiriki.
Mwisho wa hii vita ni atakapoona Yeye imetosha.
Sasa akisema imetosha washiriki by default wataeleza viumbe vingine ubaya wa ukaidi against yeye. Na hapo ameonesha mchezo utahitimishwa kuwa Yeye ni wa haki na waasi wote na shetani habari yao itakuwa imeishia hapo.

Kukosea au kutokosea kwake ni tafakuri ngumu kwangu maana kufuatana na hizo simulizi uwepo wetu naona hauna maana ukilinganisha na nyota tu ninazo ziona na zote kaumba Yeye.
 
Ee Mwenyenzi Mungu muumba mbingu na nchi tunakuomba utusamehe bure
 
Ndo madhara ya meditation hayo mnk ndo Dini yenu mpya vijana
 
MUNGU MKUU sisi sote sio wema kwako nakusihi kwa upendo na unyenyekevu msamehe ndugu yangu anayehoji uwezo wako
 
Hii thread ipo kwenye forum ya Jamii intelligence, ila most of the contributors wapo SIMPLE MINDED, yaan mada nzito kama hii watu wanajibu kiwepesi kabisa bila tatizo lolote, watu hawapo tayari kabisa kuumiza akili.
Huyu jamaa anachokiandika anakijua na biblia inavyosema anajua vizuri. ila kama kuna vitu vinamtatiza hana budi kuhoji, kwa mfano mimi pia KUNA VIPENGELE VINGI SANA NAVIJUA KWENYE KITABU CHA LUKA, YESU ANASEMA NGUVU ZAKE NA MAMLAKA YAKE YANATOKA WAPI, NA ALIKATAA KABISA KUITWA MWEMA NA KUSEMA HAKUNA ALIYE MWEMA ILA MUNGU PEKEE. Sasa sielewi kwanini sisi wakristo tunamuita Yesu Mungu, na kumuita Maria mama wa Mungu, huku si kukufuru? kweli Mungu amezaliwa kupitia kinena cha mwanamke? yani pale panapopita KIKONG'OTEO ndo Mungu alipopita?

Mungu hana birthday kwa sababu yeye yupo, alikuwepo, na ataendelea kuwepo, sasa hii tarehe 25 December imetokea wapi wakati Mungu hakuzaliwa? na kama hakuzaliwa hii birthday ya nini?

siwezi kuwalaumu coz MISHIPA YA FAHAMU IMESHALEGEZWA NA MZUNGU KUPITIA INJECTIONS MBALIMBALI. Ndo mana watu wanafeli mashuleni na vyuoni kwa kukosa ujasiri wa kuhoji, mwalimu anafundisha huelewi kipindi kikiisha unalamu ah mwalimu simuelewi, uliuluza swali class? pepa linakuja unafeli..

TUTUMIE UTASHI TULOPEWA KUFIKIRI NA KUHOJI SIO KUWA NA WOGA USIOKUA NA TIJA.. YAAN NI SAWASAWA NA MTU YULE ANAYEOGOPA KUIKOSOA SERIKALI YA CCM PALE INAPOFANYA MAAMUZI AMBAYO NI UNTHINKABLE KISA UNAOGOPA VIRUNGU NA KUFUNGWA.

AMKA.
 
MUNGU MKUU sisi sote sio wema kwako nakusihi kwa upendo na unyenyekevu msamehe ndugu yangu anayehoji uwezo wako
Mkuu ipo hivi,...nina mambo yanayonitatiza kuhusiana na imani, kati ya hayo ni hayo kumi hapo juu. Sasa nimekuja humu jf kutafuta mawazo ya watu wanaoweza kunijibu, then watu wananihukumu....mnaona mimi mkosaji kiasi cha kuanza kuniombea toba....Kwani kosa langu liko wapi??? mbona kwenye maandiko Mungu anasema...haya basi njooni tuhojiane, tusemezane....Ebu tafakari upya.
 
Mkuu umenena yote kabisa...Mimi nilidhani jf Intellegence wanakuwepo ma critical thinkers but nikagundua kumbe wapo ambao hawajui namna ya kufikiri....Hayo mambo 10 ni baadhi ya vitu vinavyo nitatiza ktk imani, nimeleta humu ili watu nondo wanijibu....badala yake nakutana na vitoto vinatoa vitisho na hukumu....vinajipa majukumu ya Mungu...Kama mtu hana jibu tulia tujulishwe coz bado naamini kuna miamba wa imani humu ndani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…