Hayo ni makubaliano ya muhammad na watu waanzishe taeehe zao
Mfano leo ni al hamisi lakini wewe unao uhakika gani kama leo al hamisi
Embu nipe alama za siku ya al hamisi ili nijue kama leo al hamisi
Ukisema leo al himisi maana yake kuna sifa zimefanya mpaka iwe al hamisi nipe hizo sifa ili nijue al hamisi ina sifa hizi
Nikisema leo ijumaa utaweza nipinga?
Utatumia logic gani kunipinga mm kama leo nikiuambia ijumaa?
Bro nimeiona comment yako hii muda mrefu sana,nikawa najishauri nikujibu au nisikujibu,maana unaonekana hufikiri mambo vile inavyotakiwa na unajidai unajua hali ya kuwa hujui. Tunapoelekea nitakuuza kama nilivyo mpuuza mwenzako Kiranga kwa kujidai mjuaji wakati hajui chochote zaidi ya kutupotezea muda tu.
Nakujibu sasa swali lako kama ifuatavyo. Historia ya kalenda ya kiislamu inafahamika wazi,kalenda ya kiislamu ilikuja baada mtume kufariki. Yalipita makubaliano kadhaa. Maswahaba wa mtume Allah awaridhie walitoa maoni kadha wa kadha,wapo waliosema kalenda ya kiislamu ianze pindi pale mtume alipopewa utume,wengine wakasema ianze pale mtume tu alipozaliwa,wengine wakasema ianze baada ya kifo cha mtume,lakini makibaliano ya mwisho kufikiwa ni kwamba ianze ile siku ambayo mtume alifanya hijira kutoka Makka kwenda Madina.
Hapa unatakiwa utulize akili mzee,siku hazikubadilia wala masaa kadhalika,bali namba tu za tarehe ndio zilibadilika.
Allah aliye juu anasema katika Qur'an "Hakika idadi ya miezi ni kumi na mbili tangu alipo umba mbingu na ardhi..."
Kaka hauwi mwezi bila masiku,aidha uwe mwezi wenye siku 29 au siku 30.
Siku ya sabato ilikuwa inajulikana tangu na tangu.
Mabadiliko ya siku yanajulikana tangu na tangu,huu wote ni muda.
Sasa nataka uniambie wewe bro,ni lini mtume Muhammad amani ya Allah iwe juu yake alifanya makubaliano ya kubadili siku au jina la siku na muda wake ?
Unajua kazi za Nyota ? Huu wote ni muda tu bro.
Sasa ukitaka ukitaka nikueleze siku ya alhamisi ina sifa gani,hili ni swali la kijinga lenye kudhihirisha ujinga wako. Sawa sawa uniambie njaa ina muonekano gani.
Sifa za siku zinajulikana. Kwetu sisi waislamu siku mpya ina badilika pindi jua linapo zama.
Sasa ukija uje na hoja na maswali ya maana si maswali ya kitoto.
Bado nipo........