Ameomba aelimishwe,kejeli za nini?Yawezekana wapo wengi wanaojiuliza swali hilo.Ni sawa na hadithi ya Uchumi kukua kwa 7% lakini mwananchi wa kawaida anakufa kwa kukosa mlo wa siku.
Kwa kawaida mtu hutumia mazingira yanayomzunguka katika kufikiri na kujenga hoja,tangu ashike hatamu,Magufuli amefanya mambo kadhaa ya msingi ambayo impact yake imeelekezwa DSM tu,1:Fedha za tafrija ya wabunge imetumika kununulia Vitanda na magodoro Muhimbili,2:Fungu lililokuwa litumike ktk maadhimisho ya Uhuru(sh.4bl)Zitatumika katika upanuzi wa barabara DSM,sasa unafikiri mwananchi wa kawaida anayekaa vijiji vya Ilyamchele,Kankanshe,Nyabilezi,Buzirayombo au Mabira Jimbo la Chato Mkoa wa Geita atawezaje kuona faida za maamuzi hayo bila ya kuelimishwa?
Hivi ni kweli watu wa Nyengedi,mahumbika,Kiwalala,mbekenyela hadi kule Lukuledi kusini mwa Tanzania wanaweza kujisifu kwamba Rais amewasaidia kwa maamuzi hayo? Basi kama ndivyo,siasa itakuwa ni ushabiki tu kama tunavyoshabikia Simba na Yanga.