Tarehe 29/ Disemba/2014,nilisafiri na gari la saa 6 mchana toka Mtwara kuja Dsm to Morogoro Chuo naposoma.Nilikaa na mtu mmoja ambaye ni mtoto wa Kada Mmoja maarufu wa CCM ,jina ninalo na no yake ya simu ninayo ila sitaweka jina lake kwa sababu za msingi kabisa,Nahisi pia atakuwa usalama wa Taifa,sikutaka kuhoji shughuli zake,mazungumzo na alivyokuwa deep ilitosha ku predict yeye ni nani, na anafanya nini,anaishi Dsm ni mwenyeji wa Mtwara. Tuliongea mambo mengi sana yaliniyoyastajabisha mno kuhusu nchi hii. Moja nitalileta soon nikimaliza Mitihani yangu.Mojawapo kuhusu Makongoro Nyerere kuwa MGOMBEA WA CCM.Na kwamba kila kitu kimeshafanyika.
Kifupi kulikuwa na kizuizi kikubwa toka mama Maria Mjane wa Mwalimu,hakuwa tayari kwa mwanae.Lakini Baadae aliridhia.
- Kinachosubiriwa ni yeye kuchukua form wakati ukifika.
- Atakuwa wa mwisho kuchukua fomu baada ya wagombea wote,na Tanzania itasimama kwa Muda.
- Yeye ndiye aliyepangwa kupitishwa kuwa mgombea wa ccm.
- Lengo ni kurestore/kurudisha nidhamu na maadili ya chama na serikali dhidi ya ufisadi,wizi.
- Hoja ni kuwa hana kashfa yoyote ile,malezi waliyokulia ni tofauti na watoto wa marais wengine,spirit ya Ujamaa iko ndani ya akili ya familia ya Nyerere.
- Ataungwa mkono na watu wengi ndani ya chama,upinzani kwa ajili ya uadilifu,lakini pia kupata kura toka watu wanaomwabudu Mungu kupitia kupitia denomination fulani.
Mnyetishaji huyo pia alisema kuwa wagombea wengine waanlijua hilo lakini hawamini sawasawa, pesa wanazotumia kuingia ikulu watajilaumu baadae.
Mnyetishaji huyo alinaimbia maneno Haya ''Brother Utanitafuta siku moja na kurejea maneno yangu,wakati jina la Makongoro litakapoteuliwa kugombea kupitia CCM'' Lets wait.
Nawasilisha.
UKANA SHILUNGO. MASOMONI MOROGORO CHUO.
Mitaa ya Kola Morogoro.
Kura nyingi tulimpa sisi wabunge wa upinzani! kuwa kimya tu kuliko kumwaga porojo!Mnapenda sana Hadithi za Vijiweni.Huu uoga wenu wa Usalama wa Taifa unatoka wapi? Kila mtu siku hizi anakuja na mambo ya ajabu,baada ya kuangaliwa kama yeye watu wanajiuliza kama ni Usalama wa Taifa.Who is Usalama wa Taifa? Hakuna yeyote leo anayeweza kusimama na kujitapa kuwa yeye ni Usalama wa Taifa?.Idara hiyo imekufa kitambo,kazi zote za Idara hiyo zinafanywa na TAKUKURU.Kwenye Idara kumebaki Walinzi wa Viongozi tu,ambao kwa kawaida hawawezi kujenga Hoja kwa sababu wamejengewa tabia ya kutojiamini na kuwa watu wa NDIO Mzee.Wanakimbizana kwenye Ma-corridor ya MOFA kutafuta safari za kwenda nje ili wainue kipato chao.Hapa tulipofikia inabidi tujenge Upya Uzalendo na kuijali Nchi kuliko Umimi uliopitiliza Kiwango.
Makongoro hawezi kuchaguliwa hata ndani ya CCM kubeba bendera ya CCM katika mbio za kinyang'anyiro cha Urais.CCM wanajua fika kwa kufanya hivyo itakuwa kuwapa njia rahisi Wapinzani kushinda Uchaguzi wa Rais.Makongoro hata hii nafasi aliyonayo sasa ya Ubunge wa EA ameipata ili kutoa nafasi kwake na familia ya Mwalimu kujisikia kuwa bado CCM inawakumbuka,kama si hivyo asingeweza kuipata,sifa zake za Uongozi ni hafifu mno.
nimewahi kumuona katika majukwaa ya siasa anaweza siasa za majukwaani , siasa za uenezi hasa zile za kisisiem za propaganda .Alimnyanyua sana mrema wakati akimpigia kampeni. Ikabidi nyere jk atumie nguvu nyingi kumkabili wakati mwingine alimponda hata nyerere jk kiaina katika namna ya vichekesho ,he is good.Kumsikia ni katika magazeti kwamba aliwakabili kina Lowasa na Chenge na Rostam kwenye kikao cha kuvuana magamba bila woga wala noma akawataja kwa majina kwamba bwana flani unaonaje uachie ngazi,pia amewahi kumkabbili mwenyekiti katika namna ya kujenga chama ,issue ni kwamba ni jasiri kuliko ccm yeyote na anaishi maisha rahisi kuliko mwiguli,makamba na wengine wanaojifanya wanyonge. Sitampa kura kwa kuwa tu ni ccm labda na uwezo kiutendaji.mI nitachagua ukawa ila akipata sitosononeka sana ni jasiri huyu bwana na hana makuu
hivi jamaa anafaa?
KWA UFUPI
Kwa mujibu wa habari za uhakika zilizozaga maeneo mbalimbali ikiwemo makao makuu ya CCCM mjini Dar es salam zinasema kuwa Makongoro Nyerere anapigiwa chapuo na watu mbalimbali ndani ya chama ili kuwa mgombea Wa chama hicho ktk Uchaguzi mkuu ujao kumrithi Rais Jakaya Kikwete ambaye ana maliza muda wake kikatiba.
Kwa mujibu Wa vyanzo mbalimbali vya habari vinasema mkakati huo unasukwa na kusimamiwa na baadhi ya makada waliowahi kufanya Kazi na Baba Wa Taifa, Hayati Mwal Nyerere, ambaye ni baba Wa Makongoro Nyerere, Hii ndio taarifa mpya ninayokupa, alisema mmoja Wa viongozi wa juu wa Ccm anyefanyia Kazi zake kwenye ofisi za chama zilizopo barabara maarufu ya Lumumba jijini Dar, Hivi tunavyoongea Makongoro ameongezewa ulinzi, na tayari maafisa usalama wanaratibu kila kitu na sehemu anayo kuwepo alisema afisa huyo aliyekataa kutajwa jina.
Naye mmoja vijana ambaye naye anaonekana kuwa na ukaribu na baadhi ya viongozi wa chama hicho aliimbia Mwanaapolo kuwa mkakati wa kumtaka Makongoro Nyerere achukue fomu ya kugombea uraisi kupitia Ccm ni mpango unaosukwa na kusimamiwa na mahasimu wa Edward Lowassa, akiilezea mpango mkakati huo, anasema kuwa maadui Wa kisiasa Wa Edward Lowassa wameshaona Nguvu za Mbunge huyo Wa Monduli, kuwa ni kubwa na kuna uwezekano mkubwa Wa kuwabwaga iwapo majina yatafikishwa kwenye ngazi za Juu ndani ya chama hicho, mwanzo inasemekana wapinzani hao walikuja na mkakati Wa kuhakikisha Edward Lowassa anafukuzwa ndani ya chama mkakati ambao pia ulimuhusisha Makongoro Nyerere wakati huo akiwa Mwkiti Wa Ccm mkoa Wa Mara ambapo inasemekana wazo la kuvua gamba lilitiliwa mkazo na kuungwa mkono na wajumbe baada ya hotuba aliyotoa Makongoro Nyerere, na kusisitiza kufukuzwa kwa baadhi ya watu kwenye chama hicho kwa madai ya kuchnganya siasa na biashara.
Hata hivyo mkakati huo unasemekana ulikwama baada ya wajumbe wengi kubaini uwepo Wa MchezoMchafu uliokuwa na lengo la kuwakandamiza baadhi ya watu kama njia ya kuelekea ikulu.
Mimi sishangai ikiwa Makongoro atachukua fomu ya uraisi atakuwa anakamilisha mkakati wa kundi lake baada ya kushindwa kwa mkakati Wa kwanza wa VuaGwanda alisema mdau mmoja ambaye yeye anaonekana anatoka kambi inayomuunga mkono Mbunge Wa Monduli, Edward Lowassa.
Akiendelea kueleza anayeonekana wazi kuwa mmoja wa watumishi ndani ya ofisi ndogo ya chama Lumumba, na ambaye hafichi Ushabiki wake kwa Mbunge Wa Monduli Mh Edward Lowassa.
Ingekuwa Makongoro anachukua fomu kwa kujipima mwenyewe na kuona anaweza kuvaa viatu vya Jk, Mimi ningemuunga mkono Sana ila ninachookiona ni kwa Makongoro kutumika aidha kwa kwa heshima ya muasisi ambaye ni baba yake au kwa yeye mwenyewe kutumika na baadhi ya makundi ili kujifaidisha kwenye huu mchakto alisema mdau huyo.
Wachambuzi Wa mambo ya kisiasa kwenye maeneo maeneo mbalimbali wamekuwa wakilijadili suala hili kwa mtizamo tofauti wako wale ambao wanamuona Makongoro Nyerere Kama nyota inayongaa iliyofunikwa na mwanga mkali Wa mwezi, Mh Makongoro ni mtu anayefaa kuwa mgombea Wa chama chetu kwa sasa alisema Mzee Mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Ramadhani, chama chetu kinahitaji mtu Wa kukiunganisha na huyu bwa Makongoro anaweza kwakuwa yeye hayupo ndani ya makundi hayo ambayo yanakaribia kukigawa chama alisema Mzee huyo.
Wadau mbalimbali waliongea nasi wameonyesha kushtushwa kidogo na habari hii ila walio wengi wanakubaliana kuwa litakuwa tukio litakalobadili Upepo kwa sehemu kubwa iwapo itafikia wakati Wa kuchukua fomu hizo na jina la Makongoro Nyerere likawepo, wengi wameegemea zaidi kwenye jina na uhusiano wake na muasisi Wa chama hicho Mwlm Nyerere, Makongoro ni Mtoto mkubwa kwa familia ya Mwlm Nyerere, Kwangu binafsi sina ninachojua Juu ya utendaji wake Ila naamini kwakuwa anatokana na Mwalm Nyerere basi ni rahisi sana kuuzika alisema Bw Nikas Marinda.
Wakati huohuo:
Arusha. Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika ya Mashariki (Eala) wamemchagua Makongoro Nyerere kuwa mwenyekiti wao mpya baada ya Adam Kimbisa kumaliza muda wake.
Uchaguzi huo uliofanyika juzi, Twaha Taslima alichaguliwa kuwa katibu, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Shyrose Bhanji.
Viongozi hao wapya watashikilia nyadhifa hizo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu. Uchaguzi kama huo pia umefanyika katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Kimbisa na Shy-Rose walikuwa makamishna kuanzia Juni 5, 2012 hadi Desemba 2014.
Taarifa za kuchaguliwa kwa Makongoro Nyerere zinaonyesha kudhibitisha kinachoitwa Mkakati wa Kujenga ili kumuandaa kuwa mgombea wa nafasi ya uraisi kupitia ccm, walipoulizwa baadhi ya wadau Juu ya kupanda huko kwa Makongoro Nyerere ktk jukwaa la Afrika Mashariki kama sehemu ya mkakati walio wengi walishindwa kukataa au kukbali lakini kubwa linaloonekana kukubaliwa na wengi ni pamoja na uungwaji mkono Wa mgombea kutoka kwa serikali za eneo ni jambo muhimu na linaloongeza Nguvu za mgombea.
Wako waliokwenda mbali na kumfananisha Makongoro Nyerere na Rais Uhuru Kenyatta ambaye Kama ilivyo kwa Makongoro wote ni watoto Wa familia za marais Wa kwanza ktk nchi zao, huwenda ikawa ni rahisi kwao kupeana ushirikiano.
Kwa hiyo akitoka makongoro anayemfuata ni RIZI ONE si ndio maana yake?
Naona kama Makongoro ananishawishi kuweka kura yangu kwa mara ya kwanza maishani mwangu kwa mgombea wa CCM tangu nianze kupiga kura mwaka 1995!
mtu yeyote mwenye akili fupi anashabikia ruksa ...sera iliyouwa ubunifu ,..uzalendo ..viwanda vyote ..na kutufanya wavaa chupi za mitumba ....
Kujenga uchumi kunahitaji uvumilivu ....hadi miaka ya 90 china walikuwa wanavaa kaunda suti nchi nzima ...na mchina wa kawaida hakuwa na nguo zaidi ya tatu....waliweza kuvumilia bila kuangalia nje nchi za ulaya wanavovaa na kula ..
Miaka ya 2000 kuja mbele uchumi wa china ukajitosheleza ndani na wakanza kwenda nje pamoja na kufungua milango ..ya uwekezaji ......ndio china ya leo wanavaa wanachokitaka na kula wanachokitaka ..
Mimi ni kati ya wanaoamini kuwa kama tungeweza kuvumilia kuvaa midabwada na kusikiliza radio ya mkulima na kujitegemea kiviwanda ...kuogea sabuni za mbuni na kupaka shanti na dawa za meno bonamed ,.....basi ni dhahiri leo tungekuwa kila kitu tunazalisha na kuuza nje wenyewe
typical tabia yetu sisi ni wavivu na kutaka kuiga ...na hatuna uvumilivu ...tukaanza kutamani kuvaa dingris jeans kama za wazungu ....kimantiki ...tukakubali kukaa na kuwa walaji wa vitu vinavozalishwa nje .....hiyo ndio adhari ya ruksa ..
Mzee mwinyi mwenyewe kwa maneno yake anatoa kasoro kwa sera yake ya ruksa ....na kukiri angepata wasaa wa kutawala tena ..asingeitekeleza kama alivyofanya ..." tulikuwa na shida tukafungua madirisha ..lakini tulisahau kuweka wavu....kwa hiyo kila kitu kikaingia ..mbu..,inzi..hadi wanyama ..." anasema mzee mwinyi
kimsingi tunaweza pia kuwalaumu washauri wake ....kwani mzee yeye alitoa mwelekeo wa kisiasa ..ilikuwa ni kazi ya wataalamu kuweka utaratibu wa sera ya ruksa ...mfano ingeruhusu tu kupokea vitu ambavyo tulikuwa na uhaba na ingeweka time frame ya kuweza kufanya mambo wenyewe ...na ingeendelea kusisitiza kujitegemea
lingine ni kuwa ..world bank na imf hawakutaka tanzania ijitegemee ..walitaka tuwe soko ...walimuhujumu nyerere na wakamlazimisha mwinyi kufunga baadhi ya mashirika ..ili watoe misaada ...
Nyerere pia alimshauri mwinyi kujadiliana na imf ....akimpa mfano wake kuwa yeye alikuwa na kiburi cha kubishana nao huko huko ...lakini yeye hangeweza kuendelea kubishana nao
Ujinga mtupu kwani nchi hii haina watu wazuri komeni kumbania lowasa
Timu EL chupi zinawabana, hawapendi kusikia jina linguine zaidi ya EL