KWA UFUPI
Kwa mujibu wa habari za uhakika zilizozaga maeneo mbalimbali ikiwemo makao makuu ya CCCM mjini Dar es salam zinasema kuwa Makongoro Nyerere anapigiwa chapuo na watu mbalimbali ndani ya chama ili kuwa mgombea Wa chama hicho ktk Uchaguzi mkuu ujao kumrithi Rais Jakaya Kikwete ambaye ana maliza muda wake kikatiba.
Kwa mujibu Wa vyanzo mbalimbali vya habari vinasema mkakati huo unasukwa na kusimamiwa na baadhi ya makada waliowahi kufanya Kazi na Baba Wa Taifa, Hayati Mwal Nyerere, ambaye ni baba Wa Makongoro Nyerere, "Hii ndio taarifa mpya ninayokupa, alisema mmoja Wa viongozi wa juu wa Ccm anyefanyia Kazi zake kwenye ofisi za chama zilizopo barabara maarufu ya Lumumba jijini Dar, "Hivi tunavyoongea Makongoro ameongezewa ulinzi, na tayari maafisa usalama wanaratibu kila kitu na sehemu anayo kuwepo" alisema afisa huyo aliyekataa kutajwa jina.
Naye mmoja vijana ambaye naye anaonekana kuwa na ukaribu na baadhi ya viongozi wa chama hicho aliimbia Mwanaapolo kuwa mkakati wa kumtaka Makongoro Nyerere achukue fomu ya kugombea uraisi kupitia Ccm ni mpango unaosukwa na kusimamiwa na mahasimu wa Edward Lowassa, akiilezea mpango "mkakati" huo, anasema kuwa maadui Wa kisiasa Wa Edward Lowassa "wameshaona" Nguvu za Mbunge huyo Wa Monduli, kuwa ni kubwa na kuna uwezekano mkubwa Wa kuwabwaga iwapo majina yatafikishwa kwenye ngazi za Juu ndani ya chama hicho, mwanzo inasemekana wapinzani hao walikuja na mkakati Wa kuhakikisha Edward Lowassa anafukuzwa ndani ya chama mkakati ambao pia ulimuhusisha Makongoro Nyerere wakati huo akiwa Mwkiti Wa Ccm mkoa Wa Mara ambapo inasemekana wazo la "kuvua gamba" lilitiliwa mkazo na kuungwa mkono na wajumbe baada ya hotuba aliyotoa Makongoro Nyerere, na kusisitiza kufukuzwa kwa baadhi ya watu kwenye chama hicho "kwa madai ya kuchnganya siasa na biashara.
Hata hivyo mkakati huo unasemekana ulikwama baada ya wajumbe wengi kubaini uwepo Wa "MchezoMchafu" uliokuwa na lengo la kuwakandamiza baadhi ya watu kama njia ya kuelekea ikulu.
"Mimi sishangai ikiwa Makongoro atachukua fomu ya uraisi atakuwa anakamilisha mkakati wa kundi lake baada ya kushindwa kwa mkakati Wa kwanza wa "VuaGwanda" alisema mdau mmoja ambaye yeye anaonekana anatoka kambi inayomuunga mkono Mbunge Wa Monduli, Edward Lowassa.
Akiendelea kueleza anayeonekana wazi kuwa mmoja wa watumishi ndani ya ofisi ndogo ya chama Lumumba, na ambaye hafichi "Ushabiki" wake kwa Mbunge Wa Monduli Mh Edward Lowassa.
"Ingekuwa Makongoro anachukua fomu kwa kujipima mwenyewe na kuona anaweza kuvaa viatu vya Jk, Mimi ningemuunga mkono Sana ila ninachookiona ni kwa Makongoro kutumika aidha kwa kwa heshima ya muasisi ambaye ni baba yake au kwa yeye mwenyewe kutumika na baadhi ya makundi ili kujifaidisha kwenye huu mchakto alisema mdau huyo.
Wachambuzi Wa mambo ya kisiasa kwenye maeneo maeneo mbalimbali wamekuwa wakilijadili suala hili kwa mtizamo tofauti wako wale ambao wanamuona Makongoro Nyerere Kama nyota inayong'aa iliyofunikwa na mwanga mkali Wa mwezi, Mh Makongoro ni mtu anayefaa kuwa mgombea Wa chama chetu kwa sasa alisema Mzee Mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Ramadhani, chama chetu kinahitaji mtu Wa kukiunganisha na huyu bwa Makongoro anaweza kwakuwa yeye hayupo ndani ya makundi hayo ambayo yanakaribia kukigawa chama alisema Mzee huyo.
Wadau mbalimbali waliongea nasi wameonyesha kushtushwa kidogo na habari hii ila walio wengi wanakubaliana kuwa litakuwa tukio litakalobadili "Upepo" kwa sehemu kubwa iwapo itafikia wakati Wa kuchukua fomu hizo na jina la Makongoro Nyerere likawepo, wengi wameegemea zaidi kwenye jina na uhusiano wake na muasisi Wa chama hicho Mwlm Nyerere, Makongoro ni Mtoto mkubwa kwa familia ya Mwlm Nyerere, "Kwangu binafsi sina ninachojua Juu ya utendaji wake Ila naamini kwakuwa anatokana na Mwalm Nyerere basi ni rahisi sana kuuzika alisema Bw Nikas Marinda.
Wakati huohuo:
Arusha. Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika ya Mashariki (Eala) wamemchagua Makongoro Nyerere kuwa mwenyekiti wao mpya baada ya Adam Kimbisa kumaliza muda wake.
Uchaguzi huo uliofanyika juzi, Twaha Taslima alichaguliwa kuwa katibu, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Shyrose Bhanji.
Viongozi hao wapya watashikilia nyadhifa hizo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu. Uchaguzi kama huo pia umefanyika katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Kimbisa na Shy-Rose walikuwa makamishna kuanzia Juni 5, 2012 hadi Desemba 2014.
Taarifa za kuchaguliwa kwa Makongoro Nyerere zinaonyesha kudhibitisha "kinachoitwa Mkakati wa Kujenga" ili kumuandaa kuwa mgombea wa nafasi ya uraisi kupitia ccm, walipoulizwa baadhi ya wadau Juu ya kupanda huko kwa Makongoro Nyerere ktk jukwaa la Afrika Mashariki kama sehemu ya mkakati walio wengi walishindwa kukataa au kukbali lakini kubwa linaloonekana kukubaliwa na wengi ni pamoja na uungwaji mkono Wa mgombea kutoka kwa serikali za eneo ni jambo muhimu na linaloongeza Nguvu za mgombea.
Wako waliokwenda mbali na kumfananisha Makongoro Nyerere na Rais Uhuru Kenyatta ambaye Kama ilivyo kwa Makongoro wote ni watoto Wa familia za marais Wa kwanza ktk nchi zao, huwenda ikawa ni rahisi kwao kupeana ushirikiano.