Baada ya kuvuma sana kwa taarifa za kwamba CCM infikiria kumsimamisha Makongoro Nyerere kuwa mrithi wa raisi kikwete, Mh Makongoro Nyerere ameamua kuweka wazi bila kkupinga kwamba ana nia au hana nia ya kuwania uraisi.
Vyombo vingi vya habari na mitandao ilitoa taarifa za bwana makongoro kuombwa agombee nafasi hiyo katika uchaguzi ujao ili aweze kusaidi kurudisha mshikamano, umoja na nidhamu ndani ya chama cha CCM, japo wengi wanalichukulia hili kama sehemu ya muendelezo wa siasa za minyukano ndani ya chama na Mh. Makongoro anatumika kupunguza kazi ya baadhi ya wagombea ndani ya chama chake.
Alipoulizwa juu ya taarifa zilizozagaa juu yake, bwana makongoro alisema " hizo ni taarifa za watu ila mimi bado sijatangaza rasmi nia ya kugombea uraisi na muda utakapofika basi nitatamka.." aliendelea kusema " chama chetu kina utaratibu mzuri wa kupata mgombea wake na mimi naheshimu taratibu hizo".
Mh. Makongoro ambaye ni mstaafu wa jeshi na msomi mahili, kwa sasa ni mbunge wa bunge la africa mashariki na ni mtu anayesemekana kuwa na misimamo thabiti haswa juu ya vita dhidi ya rushwa, anaheshimika sana kwa misimamo isiyo ya kimakundi.
katiba maelezo yake Mh. Makongoro amesema, juu ya wanachama waliojitokeza kugombea nafasi hiyo kwa sasa, na kusema wapo baadhi wanaouwezo wa kuiongoza Tanzania yetu na chama chetu lakini wapo wengine itabidi chama kiwe makini kuhakikisha hawapati nafasi kwani hawa wakipata pamoja na kwamba chama kitashinda kwa taabu lakini uadilifu wao hautatupa matumaini ya huko tuendako, alisema wapo viongozi wengi bado hawajatangaza nia yao na ni wazuri na waadilifu na wazalendo kwa nchi yao watatufaa wakipata nafasi lakini sio hawa wanaendeleza vijembe na kushawishi watu kwamba wao ndio zaidi ya wengine na kutujengea makundi ndani ya chama chetu na kufikia kugawa watu, vijana lazima wawe makini na kuendeleza fikra za watu kwa kutumia kupita na kunadi wagombea kabla hawajajiridhisha kuwa mtu wanayempigania ni sahihi, alisema.
Kwa nchi yetu hapa tulipofika mtu yoyote anaweza kuja na kusema yeye ndio atakuwa mkombozi wetu na kuisema vibaya serikali iliyopo, hiyo ni kawaida lakini haimfanyi yeye kuwa sahihi, serikali imefanya mengi bado changamoto haziwezi kukosekana.
Akiwachambua baadhi ya wagombea ambao wameshitokeza, alisema, wagombea hawa mi naona wengi wamekurupuka sana, haswa hawa vijana wetu, bado wana kazi ya ziada ya kuijua nchi hii na kuendelea kuwepo katika system ya nchi yetu kiungozi kabla ya kutamani kuwa maraisi wa nchi hii, inashangaza sana kuona sasa kuwa raisi imekuwa rahisi hivi kiasi kila mtu anaona anaweza, ujana sio sifa bali inaweza kuwa sifa ya ziada, nawasihi wasubiri wakati wao utafika.
akiongelea kuhusu wazee, alisema katika hawa wapo ambao tuna imani nao sana, uadilifu wao na utumishi wao ndani ya serikali na chama umejidhihirisha kabisa, na wengine bado tuna mashaka nao lakni wengine wanonekana itakuwa ni sababu ya kujenga makundi ndani ya chama chetu.
Bila kutafuna maneno Mh. Makongoro amesema viongozi wanaonekana kuwa na uadilifu ndani ya chama chetu na uzalendo wakweli wanaongozwa na Mzee Wasira, Samuel Sitta, Fredrick Sumaye na wengine tu hawa wengine bado ni mashaka tu.
Akimzungumzia Mh. Wasira, Mh. Makongoro alisema huyu ni mtu ambaye anijua nchi yetu na amekuwa kwenye mifumo ya uongozi toka enzi za nyerere na ni nguzo imara ya chama na serikali yetu, ameonyesha uzalendo wa juu na kuwa kiongozi muadilifu. chama chetu kikiweka mtu kama huyu tutakuwa hatuna kazi ya kumsafisha kabisa na ushindi wetu utakuwa wa wazi kabisa, simpigii debe kwakuwa anatoka mkoa mmoja na mimi ila ni wazi tu huyu ni kiongozi mchapakazi bado anaonekana kuwa na nguvu za kuitumikia nchi.
Akimzungumzia Mzee Sumaye, alisema kweli huyu ni kiongozi pia mwenye uwezo ila tatizo linalokuja amekaa sana nje ya serikali na mfumo wa nchi, ameitumikia nchi kama waziri mkuu kwa miaka 10 kwa heshima kubwa, sasa kurudi sasa ulingoni naona kama itakuwa shida, angeendelea kuwa mshauri wetu tu, Kuhusu Samuel Sitta, anasema uimara wa kiungozi aliouonyesha Mh Sitta kwenye bunge la katibu imempa sana heshima, lakini mizozo ya suala la katiba mpya itaendelea kumfunika kwa sasa, kwani wengi wanaamini ushirikishwaji wa wananchi na baadhi ya makundi haukuzingatiwa sana.
Mh. Makongoro anaamini bado CCM itaendelea kutawala Tanzania na kushinda uchaguzi ujao, ila lazima apatikane kiongozi anayeuzika kwa wananchi kwani upinzani sasa umekuwa sana nchini.
source:Raia Tanzania