Makongoro: Nasubiri kipyenga cha mwamuzi tu

Makongoro: Nasubiri kipyenga cha mwamuzi tu

Yericko....

Kila Mtanzania mwenye sifa ana haki/uhuru wa kugombea nafasi yoyote ile bila kujali anatoka familia/ukoo/kabila/kanda/mkoa gani......

Binafsi sioni tatizo hapo mradi tu wahusika wanashiriki michakato ya Kidemokrasia (uchaguzi ndani ya vyama na baadae uchaguzi mkuu)...Ingekuwa hao akina Ridhwan, Makongoro et al wanarithishwa madaraka pasipo michakato ya uchaguzi hapo kungekuwa na tatizo....

Hata nchi ambazo tunazoona zimekomaa kidemokrasia (role models wetu) nazo zina huu mtindo unaouita wa 'kifalme'...Mfano mzuri ni Marekani ....George H.W. Bush -> George W. Bush ma sasa John Ellis 'Jeb' Bush....

Pia Bill Clinton na sasa Hilary R. Clinton....

Mifano ni mingi tu...Hata India anzia kwa Jawaharlal Nehru ->Indira Gandhi->Rajiv Gandhi na inaonekana Rahul Gandhi ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa INC atakuja kuwa PM wa India miaka ijayo....Achilia Mbali mama yake Sonia Gandhi ambaye ni Rais wa INC....

Pia Argentina imeongozwa na mtu na mkewe....Nestor Kirchner (mume) na Cristina Fernandes De Kirchner ambaye ni Rais wa sasa.....

Vilevile Thaksin na Yingluck Shinawatra ambao ni mtu na mdogo wake wamewahi kuwa PMs wa Thailand kwa nyakati tofauti.....

So hata hao akina Makongoro, Ridhwan, Vita, Hussein Mwinyi wana haki ya kikatiba ya kugombea uongozi wa nchi na ndani ya vyama vyao....Na hili halipo ndani ya CCM pekee....Hata ndani ya vyama vingine vya siasa Tanzania utakuta baba, mama na mtoto au kaka na dada wanashika nafasi ndani ya vyama au za uwakilishi...Mfano Philemon Ndesamburo na Lucy Owenya (binti yake) na Grace Sindato Kihwelu (Mkwewe) ama Tundu Lissu na Christina Lissu n.k....Hapa hakuna ufalme wa aina yoyote, ni kwamba hawa watu wametumia haki yao ya Kikatiba kugombea uongozi ndani ya vyama vyao na baadae kuchaguliwa na watanzania(wa maeneo wanakotoka) na kuwa wawakilishi wao bungeni.....

Kinachotokea Tanzania ni tofauti na kilichotokea Togo, DR Congo na kwingineko ambako watoto wa marais wamerithishwa madaraka ya wazazi wao mara baada ya baba zao kufariki....

Tuiache Demokrasia ichukue nafasi yake.

Bala.
safi mkuu, natumaini Yeriko ni mwelewa...asifikiri kwa kutumia tumbo.
 
Shida ni jinsi CCM ilivyoona kuwa inaweza wa abuse km ilivyo abuse wanawake na kumweka makinda.Muda wote CCM ilikuwa akilumbana na kuikebehi hii familia vibaya.Kwa nini hawakufikiri kuhusu madaraka?
Sijaona sehemu ambayo Yericko amezungumzia 'kuabuse' familia ya Mwalimu....Na sidhani kama familia au Makongoro angekuwa abused angeweza hata kushika nafasi ya Uenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mara kuanzia 2007 na baadae kuangushwa mwaka 2012...

Kwa uelewa wangu mdogo nimesoma na kuona 'Theme' ya thread ya Yericko ni 'ufalme'......Kwamba CCM wanatumia utaratibu wa kifalme wa kurithishana madaraka...

Bala
 
Amefanya nini hasa katika nchi hii kama raia wa kawaida? Hawa watu wanadhani Urais ni kitu Rahisi eti? Wamuulize Kikwete!!!!!
 
Wanajamvi,

Mtakumbuka huko nyuma niliwajuza hali ya siasa ndani ya ccm na matarajio ya ccm kutegemea familia ya mwasisi wa taifa hili kushinda uchaguzi hapo octoba,

Makongoro kupitia gazeti la mtanzania anasema sasa anasubiri tu kipyenga cha mwamuzi, na kwamba familia ya mwasisi huyo wamemeza siri kubwa kuhakikisha mtoto huyu wa Julius Kambarage Nyerere anafuata nyao za akina Uhuru Kenyata, Aman Karume, Kabila, nk.

Siasa za ufalme sasa zajichomoza wazi ndani ya ccm hii ni baada ya ubunge wa akina Ridhiwani, Mgimwa, Vita Kawawa, Husein Mwinyi kuukwaa

Sasa mtoa mada hpo utawala wakisultani upo wapi kama uwezo anao?.....Tundu Lisu dada yake ni mbunge wa kuteliwa,mzazi wa dr. slaa ni mbunge wa kuteuliwa mbona hauongei...mbowe kapewa uenyekiti na mkwewe au haujui na hilo?.....George H.W Bush 1982 alikuwa Seneta wa Texas na 1990 akawa rais wa marekani huku mwanae George W. Bush akiwa Seneta wa Jimbo na 2001 akawa rais wa Marekani na mdogo wake JEB BUSH akiwa governor wa Florida na ametangaza nia ya kugombea uraism mwakani....pia futilia Familia ya JF KENEDY ujue....kuwa na baba kiongozi hakiondoi haki yake ya kikatiba ya kuchagua au kuchaguliwa so hakuna tatizo na wewe tafuta hoja nyingine kwa hii umefeli
 
kwani wewe si mmoja wao?
 
Amefanya nini hasa katika nchi hii kama raia wa kawaida? Hawa watu wanadhani Urais ni kitu Rahisi eti? Wamuulize Kikwete!!!!!
Kikatiba hata wewe una haki ya kugombea Urais mradi tu uwe ni Mtanzania wa kuzaliwa na umefikisha miaka 40....Na sifa nyingine zilizoainishwa......

Ndo maana hata TLP juzi wamemteua Mackymilan Lyimo kuwa mgombea Urais.....Ni kama ilivokuwa kwa Fahmi Dovutwa, Hashim Rungwe et al.
 
Sasa mtoa mada hpo utawala wakisultani upo wapi kama uwezo anao?.....Tundu Lisu dada yake ni mbunge wa kuteliwa,mzazi wa dr. slaa ni mbunge wa kuteuliwa mbona hauongei...mbowe kapewa uenyekiti na mkwewe au haujui na hilo?.....George H.W Bush 1982 alikuwa Seneta wa Texas na 1990 akawa rais wa marekani huku mwanae George W. Bush akiwa Seneta wa Jimbo na 2001 akawa rais wa Marekani na mdogo wake JEB BUSH akiwa governor wa Florida na ametangaza nia ya kugombea uraism mwakani....pia futilia Familia ya JF KENEDY ujue....kuwa na baba kiongozi hakiondoi haki yake ya kikatiba ya kuchagua au kuchaguliwa so hakuna tatizo na wewe tafuta hoja nyingine kwa hii umefeli
FaizaFoxy akiuliza mnakosomea huu ujinga mnasema kawatukana! Ni mzazi yupi huyo wa Dr Slaa ambaye ni mbunge?
 
FaizaFoxy akiuliza mnakosomea huu ujinga mnasema kawatukana! Ni mzazi yupi huyo wa Dr Slaa ambaye ni mbunge?
Inawezekana amekosea katika uandishi...Nadhani alimaanisha 'mzazi mwenzie' na alimlenga ex wa Dk. Slaa ambaye ni Mhe. Rose Kamili, ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa.
 
Hivi wewe Yericko ni wa ukoo upi? Ule wa Matombo Morogoro au? Halafu ninyi Chadema kweli siasa zimewashinda, sasa kila anaetajwa ndani ya CCM mnamponda mbaya, tuambieni sasa ninyi mnamtaka nani ndani ya ccm au hilo jukumu mnamtaka tuwape mtutaftie mgombea urais ndani ya ccm? Basi rudisheni kadi za Chadema tuwape za ccm mmependekeze mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi
CCM wote wezi
 
Wanajamvi,

Mtakumbuka huko nyuma niliwajuza hali ya siasa ndani ya ccm na matarajio ya ccm kutegemea familia ya mwasisi wa taifa hili kushinda uchaguzi hapo octoba,

Makongoro kupitia gazeti la mtanzania anasema sasa anasubiri tu kipyenga cha mwamuzi, na kwamba familia ya mwasisi huyo wamemeza siri kubwa kuhakikisha mtoto huyu wa Julius Kambarage Nyerere anafuata nyao za akina Uhuru Kenyata, Aman Karume, Kabila, nk.

Siasa za ufalme sasa zajichomoza wazi ndani ya ccm hii ni baada ya ubunge wa akina Ridhiwani, Mgimwa, Vita Kawawa, Husein Mwinyi kuukwaa

Tunaangalia sifa za kikatiba kama mtu anazo anagombea,mfano mzuri upo huko chadema kuna wafuatao wamekidhi "vigezo na wamepata ubunge"
Mbowe=Edwin Mtei mkwe
Rose Kamili=Dr.Wilbroad slaa wife
Christina Lissu=Tundu Antipas Lissu dada
Grace kiwelu Ndesamburo=Philemon ndesamburo mkwe
Lucy Owenya=Philemon Ndesamburo binti
Anna Komu=Anthony Komu mke

Mkuu toa boriti kwanza kwenye jicho lako halafu uanze kulaumu CCM
 
Sijaona sehemu ambayo Yericko amezungumzia 'kuabuse' familia ya Mwalimu....Na sidhani kama familia au Makongoro angekuwa abused angeweza hata kushika nafasi ya Uenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mara kuanzia 2007 na baadae kuangushwa mwaka 2012... Kwa uelewa wangu mdogo nimesoma na kuona 'Theme' ya thread ya Yericko ni 'ufalme'......Kwamba CCM wanatumia utaratibu wa kifalme wa kurithishana madaraka... Bala
by that time iliangukia wakati THE TEACHER ametutoka..kwa hiyo CCM haibu hawakuwa nayo tena.
 
by that time iliangukia wakati THE TEACHER ametutoka..kwa hiyo CCM haibu hawakuwa nayo tena.
Mkuu.....

Makongoro hakuanguka kwa sababu Mwalimu hayupo....Alishindwa kidemokrasia katika uchaguzi, na alikubali matokeo na bado ameendelea kuwa mwana CCM mtiifu...

Alianguka kwa sababu ya kura zake kutotosha katika uchaguzi wa viongozi wa ndani wa CCM mwaka 2012....Ikumbukwe kwamba alichaguliwa mwaka 2007 , miaka 8 tangu Mwalimu afariki...Kama kigezo ni uwepo wa Mwalimu basi asingechaguliwa na wan CCM wa mkoa wa Mara katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM mkoa mwaka 2007.

Pia kumbuka kwamba Charles Makongoro Nyerere ni mtoto pekee wa kuzaliwa na Maria na Julius Nyerere kuwahi kuwa mwanachama na Mbunge wa chama cha upinzani(I stand to be corrected).... Makongoro alikuwa Mbunge wa Arusha kwa tiketi ya NCCR - Mageuzi kuanzia mwaka 1995 (Mwalimu alikuwa hai, yet mwanae alikuwa upinzani).
 
Wanajamvi,

Mtakumbuka huko nyuma niliwajuza hali ya siasa ndani ya ccm na matarajio ya ccm kutegemea familia ya mwasisi wa taifa hili kushinda uchaguzi hapo octoba,

Makongoro kupitia gazeti la mtanzania anasema sasa anasubiri tu kipyenga cha mwamuzi, na kwamba familia ya mwasisi huyo wamemeza siri kubwa kuhakikisha mtoto huyu wa Julius Kambarage Nyerere anafuata nyao za akina Uhuru Kenyata, Aman Karume, Kabila, nk.

Siasa za ufalme sasa zajichomoza wazi ndani ya ccm hii ni baada ya ubunge wa akina Ridhiwani, Mgimwa, Vita Kawawa, Husein Mwinyi kuukwaa

CCM hata wamsimamishe nani,mwaka huu lazima wakae
 
Hivi wewe Yericko ni wa ukoo upi? Ule wa Matombo Morogoro au? Halafu ninyi Chadema kweli siasa zimewashinda, sasa kila anaetajwa ndani ya CCM mnamponda mbaya, tuambieni sasa ninyi mnamtaka nani ndani ya ccm au hilo jukumu mnamtaka tuwape mtutaftie mgombea urais ndani ya ccm? Basi rudisheni kadi za Chadema tuwape za ccm mmependekeze mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi

Mbona nyie kutwa kucha kutuchagulia UKAWA mgombea
 
Ama kweli neno msaliti fits many people, I thought u were part of the Nyerere family, kumbe wewe ni FAKE product.

Swadakta Mkuu mimi nilijua huyu jamaa kwa namna ambavyo anakazania kulitumia jina la ukoo wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere basi sie wengine MAGT humu ndani tukaenda kichwani huku tukiendelea kuunganisha dot kidogo kidogo labda zile hekaya za wahenga wetu kuwa kitanda akizai haramu/inazaniwa/uenda/labda/kwa watu wazima uwa inatokea/kiafrika ni jambo la kawaida/kwa watoka koo za kichifu wanajua kuna utapanyaji wa damu ata kwa mtapanyaji asivyotalajia binafsi/kwa asivyojua anakuta imetoke labda huyu ni sehemu hiyo ya utokeaji/na maswali mengine mengi ya kujiuliza na kujijibu binafsi kwingi sana kunakowapitia wanajf humu ndani kuhusiana na huyu jamaa na kama kawaida ya mambo ya koo za kichifu huwa hayana majibu kwa watu wengine ila kwa wenye viti wa koo husika.

Kuna picha yake moja watu walijaribu kulinganisha kutafuta vinasaba vya kimwili na kuona kama kweli ana vinasaba hivyo kwa muhusika na hata kwa mtoto wa muhusika huyo mwingine ukimkusanya na yeye kiasi fulani wana kimwonekano kinacho elekea manake mtu apotezi chake ata kucha, au unyayo sembuse paji la uso, midomo na pua ndio usiseme.

Sasa najiuliza inakuaje dogo anakuja kwa bro na kauli ya hivi.............Itabidi mkuu wa kaya kwa Mwalimu wamkarishe huyu dogo kama kweli anahusika manake vinginevyo kwa kauli za hivi huyu dogo ni tatizo kwake na anapaswa kufahamu mila za kwao kuwa MKUBWA anachaguliwa ajichagui..Sasa kauli zake za ajabu ajabu kama vile ajajua anatoka koo za machifu basi ajifunze koo za machifu uwa azichezewi anavyojaribu kutuonyesha humu ndani.

Basi vinginevyo yeye anayelazimisha matumizi ya jina hilo atakuwa CHIFU dom ishakataa kuwa si damu yao na kilichotekea ni kufanana kwa mapenzi ya Mungu, kama ambavyo waswahili useme Mwanaume asiye kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanamke, na ni marafiki wa kawaida na akawa na mimba akizaa mtoto basi mtoto yule kwa uumbaji wa ajabu wa Mungu, Mtoto anaweza kutoka anafanana na jamaa husika.Sasa kama hizo ni ngano za wahenga basi hadithi hizi zilikua na mifumo ya kustahi na kuhifadhi mambo mazito ya watu wazima.

Nikilejea kauli za Yericko, kama haku baatika kupewa fursa ya kuijua familia ya anakojitanabaisha nayo basi ni fursa ya kumuomba mkuu wa kaya hiyo [Msemaji Mkuu wa Ukoo] wampe mwongozo hasa linapokuja kwenye mambo mzito na makubwa ya kuelekea kuomba kupewa kiti cha kuitumia Nchi kama RAIS.

Kama ni wa damu na tayari anaonyesha kuoppose kama mtu ambae hayuko kwenye mahusiano ya kidamu,basi mtoaji ANAJITAFUTIA MATATIZO na ndio ishara ya WANAUCCM mara wanaona si mtu sahihi kwa familia tajwa.

Wazungu awakukosea kusema Ukarimu Uanzia Nyumbani [Charity begins At Home] sasa ukarimu wa huyu jamaa kwa familia anayojinasabisha nayo mpaka watu wanafikia kumuona kama kweli ni kiumbe wa mtu husika anatoa wapi povu kuonge maneno ya ajabu kumuhusu mwanafamilia mwingine.

Au ndio ile tukose......wakati issue hapa ni Mzaliwa aliyechaguliwa kwenye familia ...mie nilimchukulia mleta thread kama mambo ya Rais wa Ufaransa marehemu Francois Mitterand na binti yake Mazarine au kijana anae semekana wa kwake Mwanasiasa wa Sweden Hravn Forsne na kuwa kuna siku atajitambua na kubeba image ya kweli kweli na huko siku za mbele itamsaidia.

Yericko kama unavinasaba na Mwalimu au vinginevyo iwe vyovyote ama ulichaguliwa na Mwalimu kuwa mtoto wake wa kuhasi basi acha mchezo linapokuja swala la mambo ya VITI na liheshimu sana sana.Tena koma koma koma nakuomba kwa kuwa kama ujui habari za machifu tafuta chifu yoyote yule umuulize huo ni muziki mwingine hizo habari za Ujah men kwa pande hizo kaa mbali kabisa isije ikawa hadithi....paukwa pakawa..alitokea deshi deshi kapanda naniliii.

Lakini kama una tofauti zako na mtaka nafasi na unatumia lugha hiyo kujenga mazingira mabovu basi jua ni SIFURI na itakura kwako kwa kuwa Tanzania bado ina wazee na yakiwafikia na wakakuona wewe ni tatizo maweeeeeeeee......lugha ya Mtani wa mtu hiyo...ni .manche ga nyansa mie simo....

Usifuate uchifu wa kupeana kwenye viti vya siasa hiyo uwa ni maigizo uchifu uwa unaflow na damu baba.....waombe wakufundishe ujifunze tofauti zako na watu wa ndani ya nyumba zifute linapokuja jambo la kuongoza Taifa na hata maswala ya viti.
 
Tunaangalia sifa za kikatiba kama mtu anazo anagombea,mfano mzuri upo huko chadema kuna wafuatao wamekidhi "vigezo na wamepata ubunge"
Mbowe=Edwin Mtei mkwe
Rose Kamili=Dr.Wilbroad slaa wife
Christina Lissu=Tundu Antipas Lissu dada
Grace kiwelu Ndesamburo=Philemon ndesamburo mkwe
Lucy Owenya=Philemon Ndesamburo binti
Anna Komu=Anthony Komu mke

Mkuu toa boriti kwanza kwenye jicho lako halafu uanze kulaumu CCM
Mleta mada nimwelewa sana...nadhani alitaka kufikisha ujumbe kwa wakubwa wake kupitia Makongoro.
 
Back
Top Bottom