Wanajamvi,
Mtakumbuka huko nyuma niliwajuza hali ya siasa ndani ya ccm na matarajio ya ccm kutegemea familia ya mwasisi wa taifa hili kushinda uchaguzi hapo octoba,
Makongoro kupitia gazeti la mtanzania anasema sasa anasubiri tu kipyenga cha mwamuzi, na kwamba familia ya mwasisi huyo wamemeza siri kubwa kuhakikisha mtoto huyu wa Julius Kambarage Nyerere anafuata nyao za akina Uhuru Kenyata, Aman Karume, Kabila, nk.
Siasa za ufalme sasa zajichomoza wazi ndani ya ccm hii ni baada ya ubunge wa akina Ridhiwani, Mgimwa, Vita Kawawa, Husein Mwinyi kuukwaa
Yericko....
Kila Mtanzania mwenye sifa ana haki/uhuru wa kugombea nafasi yoyote ile bila kujali anatoka familia/ukoo/kabila/kanda/mkoa gani......
Binafsi sioni tatizo hapo mradi tu wahusika wanashiriki michakato ya Kidemokrasia (uchaguzi ndani ya vyama na baadae uchaguzi mkuu)...Ingekuwa hao akina Ridhwan, Makongoro et al wanarithishwa madaraka pasipo michakato ya uchaguzi hapo kungekuwa na tatizo....
Hata nchi ambazo tunazoona zimekomaa kidemokrasia (role models wetu) nazo zina huu mtindo unaouita wa 'kifalme'...Mfano mzuri ni Marekani ....George H.W. Bush -> George W. Bush ma sasa John Ellis 'Jeb' Bush....
Pia Bill Clinton na sasa Hilary R. Clinton....
Mifano ni mingi tu...Hata India anzia kwa Jawaharlal Nehru ->Indira Gandhi->Rajiv Gandhi na inaonekana Rahul Gandhi ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa INC atakuja kuwa PM wa India miaka ijayo....Achilia Mbali mama yake Sonia Gandhi ambaye ni Rais wa INC....
Pia Argentina imeongozwa na mtu na mkewe....Nestor Kirchner (mume) na Cristina Fernandes De Kirchner ambaye ni Rais wa sasa.....
Vilevile Thaksin na Yingluck Shinawatra ambao ni mtu na mdogo wake wamewahi kuwa PMs wa Thailand kwa nyakati tofauti.....
So hata hao akina Makongoro, Ridhwan, Vita, Hussein Mwinyi wana haki ya kikatiba ya kugombea uongozi wa nchi na ndani ya vyama vyao....Na hili halipo ndani ya CCM pekee....Hata ndani ya vyama vingine vya siasa Tanzania utakuta baba, mama na mtoto au kaka na dada wanashika nafasi ndani ya vyama au za uwakilishi...Mfano Philemon Ndesamburo na Lucy Owenya (binti yake) na Grace Sindato Kihwelu (Mkwewe) ama Tundu Lissu na Christina Lissu n.k....Hapa hakuna ufalme wa aina yoyote, ni kwamba hawa watu wametumia haki yao ya Kikatiba kugombea uongozi ndani ya vyama vyao na baadae kuchaguliwa na watanzania(wa maeneo wanakotoka) na kuwa wawakilishi wao bungeni.....
Kinachotokea Tanzania ni tofauti na kilichotokea Togo, DR Congo na kwingineko ambako watoto wa marais wamerithishwa madaraka ya wazazi wao mara baada ya baba zao kufariki....
Tuiache Demokrasia ichukue nafasi yake.
Bala.