Kinachowarejesha wapinzani kwenda CCM ni ulafi wa madaraka tu

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,753
Wanazengo
Umofia kwenu.

Katika muhula wa awamu mbili zilizopita tulishuhudia wimbi la wanasiasa kambi ya upinzani hasa wawakilishi Bungeni wakihamia CCM kwa wingi. Yalisemwa mengi yakiwemo ya wapinzani kununuliwa na hata wengine kuda wananusuru maisha yao na familia zao kwa kuhamia CCM.

Kuna moja kubwa nimeliona kwenye hili sakata.

Tuanze na mjumbe wa Kamati Kuu mzee Wasira ambaye kupitia mchakato wa ndani ya CCM kuomba kuiwakilisha akajikuta anatupwa nje mwaka 1995. Kulimsababisha atimkie NCCR Mageuzi ambako akiwa huko alipigiwa debe na marehemu Baba wa Taifa akashinda Ubunge. Hatimaye alipohakikishiwa mazingira ya ushindi chamani alihamia CCM chaguzi zinazofuata akaendelea kushinda.

Hili linaweza lisiwe na maana kubwa kwa wanaoichukulia siasa kijuu juu na kishabiki. Lakini kwa wadadisi na wachambuzi mtaelewa kuwa motivation kubwa nyuma ya hama hama za wanasiasa kutoka chama hadi chama siyo kwa lengo la kuwatumikia wananchi bali ulafi wa madaraka.

Ukichunguza wanasiasa wengi karibia wote waliotemwa kwenye michakato ya ndani ya CCM kuwania uteuzi kuwakilisha chama kwenye chaguzi za dola huwa wanakimbilia vyama pinzani wakiwa na uhakika wanaweza kuwin. Tukikumbuka sakata la Lowasa, Nyalandu, Sumaye, makongoro na wengineo utaona hii dhana ni dhahiri haina ubishani.

Vyivyo hivyo, wapo wanasiasa assets wa upinzani ambao wanalishwa hofu ya kukosa madaraka na hivyo wanakuwa wepesi kuvikimbia vyama vyao na kuhamia CCM. Bahati inakuwa upande wao ambapo hata wakihamia katikati ya muhula wanapitishwa kuwania maeneo yao na lazima watashinda, na wengine waliendelea na ubunge wao huku wakiwa wanazengwe na vyama vyao. Dola imekuwa ikitumika kama tawi la CCM kuhakikisha mazingira yote yanayotishia continuity ya utawala wa CCM yanakuwa neutralized.


Ndugu yangu, kwa hapa ni budi utambue kwamba kipaumbele cha kwanza cha CCM siyo maslahi ya nchi bali ni kupata uhakika wa kutawala milele na milele. Wananchi hutumika very dramatically kipindi cha kuelekea uchaguzi na baada ya hapo mchwa wanarudi mzigoni to do what they are doing best. Angalia akina Silinde na wenzake waliotokea upinzani, wapo tayari kuhaini ama kuzikana fikra zao za kimaendeleo walizokuwa wanazisimamia huko upinzani. Tukifanya tafiti ndogo tu utagundua hakuna mwanachama wa CCM ambaye ameshinda chaguzi za ndani za chama bila rushwa. Hao ndiyo wanaenda kupitisha majina ya wagombea wa chama.

Kwa mantiki hiyo, tunahitaji kama jamii kuanza kuzalisha wanasiasa wenye kuweka mbele maslahi ya Taifa kuliko ya vyama ama familia zao. Jamii ihamasishe upatikanaji wa Katiba ya Wananchi ambayo itasimika mifumo imara inayowatema viongozi wanaoitumia siasa kama mtaji wa maisha yao.

CCM imepoteza dira na mwelekeo hadi kufikia kuanzisha vita vya kigaidi na wananchi wowote wanaoonesha ni tishio la maslahi yao. Jiulize kuhusu Ben Saanane, Azory, Akwilina, Mwangosi ambao wote ni wahanga wa matukio ya uhalifu wa kisiasa.

Tundu Lisu ni ushuhuda mwingine wa matukio yanayoianika dhamira ya CCM kuangamiza ama kufifisha juhudi za yeyote anayepambabia maslahi ya nchi. Vyama mbadala wanapaswa kuasisi sera na misimamo yao kama urithi kwa wananchi kuliko kuendeleza mitafaruku ya madaraka na mapambano ya maslahi binafsi

Najua, ninakuwa nimejiweka rehani kwa kuweka huu uzi lakini bora ukifa ukiwa umesimamia ukweli kama alivyofanya Mtume Stephano nyakati za Matendo ya Mitume.

20220812_211745.jpg
 
Mkuu uzi wako una ukweli mwingi sana, ila hapo kuwa umejiweka rehani kwa uzi huu nimeshindwa kuelewa. Hapa unatumia fake I'd, huo ni urehani ni upi?

Isitoshe uzi wako hauna kitisho cha maslahi ya mtu zaidi ya maoni yako wanasiasa. Toa hilo neno rehani, labda kama umecopy huu uzi mahali na kuuhariri.
 
Mkuu uzi wako una ukweli mwingi sana, ila hapo kuwa umejiweka rehani kwa uzi huu nimeshindwa kuelewa. Hapa unatumia fake I'd, huo ni urehani ni upi? Isitoshe uzi wako hauna kitisho cha maslahi ya mtu zaidi ya maoni yako wanasiasa. Toa hilo neno rehani, labda kama umecopy huu uzi mahali na kuuhariri.
Msanii ni verified member.
 
Mkuu uzi wako una ukweli mwingi sana, ila hapo kuwa umejiweka rehani kwa uzi huu nimeshindwa kuelewa. Hapa unatumia fake I'd, huo ni urehani ni upi? Isitoshe uzi wako hauna kitisho cha maslahi ya mtu zaidi ya maoni yako wanasiasa. Toa hilo neno rehani, labda kama umecopy huu uzi mahali na kuuhariri.
Sina mashaka kabisa na usalama wangu kupitia JF as platform lakini marafiki wanaonifahamu tuliokutana humu ndo rehani yenyewe.
 
Hilo liko wazi kijani imeshapoteza mwerekeo..sasa imebaki kikundi cha walaghai na maharamia wachache wenye uchu na ufusadi mkuu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nikikumbuka hangaiko la ndugu Humphrey Polepole baada ya kutemwa Uenezi CCM alisimamia sana kaulimbiu ya Kataa Wahuni lakini kumbe ilikuwa ni shinikizo apewe madaraka ambapo hivi sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Malawi. Hasikiki tena akikosoa mwenendo mbaya wa Chama chetu dhidi ya wananchi

Shida ni madaraka.
Shida ni njaa

Nina mashaka hata sisi wapiga mbiu inawezekana tukapata madaraka tukageuka kuwa far worse kuliko waliopo sasa.

Point yangu ni kwamba, bila kuwa na mikakati collectively na kusimamia maslahi ya nchi bila ubaguzi na visasi hakuna jipya litakalokuja. Tuwaandae viongozi wa kesho positively
 
Back
Top Bottom